Mkuu nashkuru kwa kuniita kwenye mada nzuri hii labda nijibu kwa maoni yangu kutumia source tofauti maana sio kila kitu biblia inazungumzia
1.
maji, giza, Nuru, na upepo viliumbwa siku gani kati ya zile sita za uumbaji?
Maji yalitengenezwa siku ya kwanza ama kabla ya siku ya kwanza yalishatengenezwa.... Kuna story ndefu kidogo inaitwa Gap theory inayoeleza muda kati ya mwanzo 1 na 2 kuwa Mungu aliumba dunia ila baada ya kuvurugana na shetani, alivyotupwa aliamua kuivuruga dunia na kuiharibu mfumo wake mzima hivyo kilichobaki ni maji tu na hakukuwa na mwanga yaani GIZA sababu shetani aliharibu nyota zote
Nuru iliumbwa kabla ya mwanzo 2 ila baada ya kuvurugwa na shetani ndipo akaamua kutengeneza nuru siku ya kwanza
3
Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru.
4 Mungu akaiona nuru, ya kuwa ni njema; Mungu akatenga nuru na giza.
NB: ila cha kuzingatia hapa huu mwanga sio jua... Jua lilitengenzwa siku ya 4 ila huu mwanga ulikuwa unaangaza dunia but halina uhusiano wowote na jua au nyota nyingine yeyote
kuhusu upepo ulianza mwanzo 8:1 yaani Nuhu alipokuwa kwenye safina na maji yamejaa dunia nzima hivyo akaamua kuleta upepo ili kutawanya maji na ardhi hivyo upepo umetajwa mara ya kwanza hapa ila kama upepo ndio mara zote unatenganisha maji na ardhi basi tunaweza kusema kwenye zile siku 6 upepo uliumbwa siku ya tatu pale alipofanya kitendo kilekile cha kutenganisha maji na ardhi.
2.
swali binadamu karibia wote (sio wote) walioonekana kumchukiza Mungu juu ya uso wa dunia/nchi wangeamua kuingia safinani wangetosha?
Mkuu biblia inaonyesha kuwa alishadhamiria kumfanya Nuhu pekee aanzishe kizazi kipya ndio maana hata ukoo wote wa Seth yaani kina methuselah,kenan,mehujael n.k Mungu aliwachukua kupitia kifo miezi michache kabla ya gharika.... Piga hesabu utagundua ukoo mzima wa seth hakuna aliyekufa wakati wa gharika ila mwaka au miezi kabla ya gharika hata Methuselah naye alifariki miezi 6 kabla ya gharika yote haya ikimaanisha Mungu alishaona wanadamu hawana mpango wa kubadilika hivyo akaona aanze upya... So kujibu swali lako ni kwamba wasingetosha wote ila kama angejua wengi watabaki basi huenda asingeleta gharika kabisa au labda angewaficha tu kwenye Mlima au pango fulani na wakapona
3.
swali ilikua nchi au dunia?
kama ilikuwa nchi kwann mafundisho yaoneshe dunia iligharikishwa
Ni dunia nzima ila waliita nchi ikimaanisha arshi yote iliyo juu ya maji hivyo ni dunia maana
Mwanzo 7
22
kila kitu chenye pumzi ya roho ya uhai puani mwake kikafa, kila kilichokuwako katika nchi kavu.
4.kama ilikuwa dunia watu waliwasiliana kwa lugha ipi kutoka kizazi cha nuhu mpaka kwingineko duniani?
Biblia haielezi lugha gani ilioongelewa na Adam wenye biblia yao wanadai ni kiebrania ndio Adam aliongea yaani Adam naye alikuwa myahudi!!! Anyway kwa wasomi wengine wa elimu ya roho kama john dee et al wanadai lugha iliyoongelewa ilikuwa ''enochian'' yaani lugha ya kimalaika ilioongelewa kuanzia bustani ya edeni na waliipa hilo jina baada ya kuona ni Enock mtu wa mwisho kuongea lugha hii ila zaidi ya hapo ukweli haujulikani na kama upo umefichwa na wenye biblia yao.
5.kama ilikuwa nchi na sio dunia ni vizazi gani vingine vilisalimika tofauti na kizazi cha nuhu?
Kibiblia hakuna aliyesalimika kwenye gharika tukiachana na controversy ya mfalme Ogu aliyepona ili kuvusha damu ya wanefili ama mke wa Ham yaani neitamuk kubeba mimba ya shamael ili kuvusha kizazi cha Cain.... Hakuna jamii yeyote iliokuwepo kabla ya gharika ikapona na hii ni kwa mujibu wa biblia ingawa mpaka leo hakuna ushahidi wa kisayansi kuwa dunia iliwahi kufunikwa na maji.....
Ni hayo tu mkuu labda niite wataalam zaidi
Malcom Lumumba Son of Gamba Mshana Jr Nanaa jolie piteni huku mtie neno