Nuru, maji, giza, upepo viliumbwa siku gani kati ya zile sita za uumbaji?

huu utata nwingine sikuwahi kuufikiria kabisa
upuuzi haukuishia hapo tu,soma hapa wanavyojaribu kujustify/kupromote utumwa

Ephesians 6:5
Slaves, obey your earthly masters with respect and fear, and with sincerity of heart, just as you would obey Christ.

haya ni maandishi yaliyoandikwa na watu to further their colonial agendas,usiyachukulie seriously hata kidogo​
 
Duh jambo jipya hili mkuu sikuwahi lisikia kwakweli theory ni nyingi siku ushushe hiyo nondo tujadili kwa mapana humu maana JF haikosagi majibu.
 
zitto junior hebu sema kitu juu ya fungu hilo hapo juu
Mkuu hilo swali la nyabhingi msomi Son of Gamba alisema ni kweli hiyo kitu ipo na ataleta majibu ya uzi maalum hivyo nisiwahi chakula kabla hakijaivishwa..... Soon atakuja na nondo zake atalijibu hilo otherwise na mmi nimeandaa uzi kuhusu utata na kukinzana kwa biblia umeshiba haswaa nafikiri huko ndipo majibu yote yatapatikana

Tuombeane uzima
 
tunaweza kuhitimisha kuwa giza sio kitu halisi na hivyo hakikuumbwa?

Unaweza kusema hivyo kama ukitoka nje ya mawazo ya vitabu vya dini...

Mfano: hakuna(giza) na kuna(Nuru)...
Unaposema hakuna,maana ni hakuna chochote, ukosefu... hakuna haitengenezwi na chochote ni hakuna tuu, empty... hakuna cha kuelezea...

Unaposema kuna(Nuru), kuna kitu, hiko kitu kina chanzo hicho chanzo kitakua na maelezo...

Giza lipo, lilikuwepo lakini halina maelezo. Huwezi kutengeneza giza, bali unawze kuondoa chanzo cha nishati mwanga (nuru) ili giza lichukue nafasi yake...


Cc: mahondaw
 
kwanza shukrani kwa kujibu

pili shukrani kwa kumtaja huyo ndugu hapo juuu kwa sababu itamkumbusha alete hizo nondo mapema

tatu nasubiri mada yako kwa hamu usisahau kuniita
 
nimekupata mkuu
 
Jamani eeeenh nanyoosha tena mkono... Naombeni majibu au mpaka niwape mjiiii....
 
Jamani eeeenh nanyoosha tena mkono... Naombeni majibu au mpaka niwape mjiiii....
kwakweli sina majibu maana nyabhingi kasema ilifunika futi 21 tu na akaongeza swali kuwa unajua urefu wa mlima kilimanjaro tukiacha ule mrefu zaid duniani Ev?
 
Jamani eeeenh nanyoosha tena mkono... Naombeni majibu au mpaka niwape mjiiii....
1. Safina ilitua mlima ararat huko uturuki/Armenia ya sasa na eneo hilo lipo hadi leo ingawa bado hakuna ushahidi wa kutosha ya uwepo wa safina hyo ingawa wanadai walikuta miti mirefu na mbao imejichimbia eneo hilo

2.Biblia inasema milima yote mirefu ilifunikwa kwa mikono 15 juu....

Mwanzo 7
19 Maji yakapata nguvu sana sana juu ya nchi; na milima mirefu yote iliyokuwako chini ya mbingu ikafunikizwa.
20 Maji yakapata nguvu, hata ikafunikwa milima kiasi cha mikono kumi na mitano

Hivyo sijui kma Mlima kilimanjaro ulifunikwa ila biblia inadai milima YOTE MIREFU ilifunikwa na maji

Ni hayo tu
 
Inakuwaje ifunike milima yote halafu utue kwenye mlima mfupi wa Ararat au ndio ulikuwa mrefu ila umeliwa na mmomonyoko wa udongo eti....
 
Inakuwaje ifunike milima yote halafu utue kwenye mlima mfupi wa Ararat au ndio ulikuwa mrefu ila umeliwa na mmomonyoko wa udongo eti....
Mvua ilipoisha ndio safina ikawa imekwamia hapo...... Ila wakati wa mafuriko hata huo Ararat ulikuwa umefunikwa na maji hyo ni kutokana na biblia
 
Kumbe uumbaji haukuisha katika zile siku sita tuu!
Wanasayansi wanatuambia " the universe is rapidly expanding,new stars and planets are in the making every day old stars are dying and others disappear in black holes every day
 



Inawezekana Mlima Kilimanjaro haukuwepo wakati huo.
 
View attachment 830457

Inawezekana Mlima Kilimanjaro haukuwepo wakati huo.
kwa mujibu wa biblia adam na eva(ambao wanadai ni binadamu wa kwanza) waliumbwa si zaidi ya miaka 4000 iliyopita,..iweje mlima kilimanjaro usiwepo!!!!
hata milima mbezi na goba ni zaidi ya futi 21..tusahau kuhusu k'njaro kwa muda
 
Ulisahau malaika, but still vilikuepo tu, naamini sayari Dunia wakati inaumbwa tayari kulikuwa na sayari zingine zilishaumbwa before
 
3.swali ilikua nchi au dunia?
kama ilikuwa nchi kwann mafundisho yaoneshe dunia iligharikishwa
Mkuu zitto junior umemjibu vyema sana isipokuwa hapa kwenye hili swali lake la 3 kuna kitu nataka nifafanue kidogo. Neno "nchi" ni tafsiri ya neno "Earth" au "Land", waliotafsiri Biblia ya Kiswahili waliitafsiri kutoka kwenye lugha ya Kiingereza. Hivyo neno Earth au Land likatafsiriwa kama "nchi" kwa Kiswahili.

Kwa mfano hebu soma GENESIS 7:22 "all in whose nostrils was the breath of life, of all that was in the dry land died".....hapa neno dry land likatafsiriwa kama "nchi". Pia tusome GENESIS 7:18 "And the waters prevailed and were increased greatly upon the earth, and the ark went upon the face of the waters".....hapa pia utaona neno "earth" limetafsiriwa vile vile kama "nchi" kwenye Biblia ya Kiswahili.

Mara nyingi sana "tafsiri" imekuwa ikiwasumbua watu wengi sana. Mimi huwa nasoma Biblia ya Kiswahili na ili kupata "tafsiri" bora zaidi ya maneno huwa nasoma Biblia ya Kiingereza pia na wakati mwingine huwa natafuta maana ya maneno ya Kigiriki ili kujiridhisha.
Cc. Mr Q
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…