Nusu Karne na CCM?

Nusu Karne na CCM?

Bibi Ntilie,
Chadema or CUF OR ANY OTHER POLITICAL PARTY with genuine interests to rid Tanzania of our current ENEMY who is CCM deserve our assistance!
Samahani dada yangu lakini maneno haya binafsi siyaungi mkono.. Siwezi kusema CCM kama chama ni adui yetu wananchi..
 
Mkandara,

Asante, maneno hayo ni ya Masanja mie nimemnukuu tu.


Nilimjibu Masanja kabla sijasoma yote tuliyoletewa na Asha.

Yaliyomo kwenye Orodha ya ITIKADI NA SERA ZA CHADEMA ni mengi na mema Sijui kama kuna cha kuongeza maana ‘kero’ zote zimeguswa.

Swali, utekelezaji wa orodha hiyo ndefu utakuwaje? Ni dhahiri itabidi mambo yafanyike hatua kwa hatua. Tunaanza na hatua gani na tunamalizia na ipi?

Mwisho wa bandiko la Asha kuna msisitizo kwamba TUNACHOHITAJI TANZANIA SIO UZURI WA SERA TU, TUNAHITAJI VIONGOZI WAZURI WATAOONGOZA TAIFA NA KWA MUJIBU WA MATAKWA YA UMMA-AMBAYO NI SERA ZA KWELI ZINAZOJALI WATU BADALA YA MAWAZO YAO BINAFSI WANAYOYAPA BARAKA KWA KUYAITA SERA ZA CHAMA.

Tunarudi kwenye hoja yangu ambayo naamini ilifanya Masanja ahamaki na kuita watu punguani, akitaka tujiunge tu maana CCM wameshindwa!

Asha anasema: Ili tuweze kukidhi matarajio ya wananchi chini ya uongozi wa CHADEMA tunahitaji “Viongozi Wazuri”.

Kama hivyo ndivyo, ni wazi ndani ya miaka 2 CHADEMA itabidi wafanye kazi ya ziada ya kutafuta na kupata ‘viongozi wazuri’ wa kutosha wanaotarajiwa kuifanya hiyo kazi kubwa ya kuibadili nchi. Vinginevyo, tusijeanza kuwazomea na kuwapopoa mawe akina Zitto kwa frustrations watakazotupa!

Halikadhalika, kama wasemavyo Waswahili “Shughuli ni Watu”, watu watakaotakiwa kufanikisha Sera za CHADEMA ni sisi Watanzania wote katika sehemu yeyote tuliyopo iwe shambani, ofisini, viwandani, kwenye biashara zetu ama jikoni. Je CHADEMA na Watanzania wazalendo tutatumia mbinu gani kubadili mawazo na mwelekeo wa baadhi ya viongozi na Watanzania waliokengeuka?

Kwa maoni yangu, bado KILIMO ndicho uti wa mgongo wa maendeleo ya Watanzania walio wengi. Kwa hiyo, ni vyema kabla ya jingine lolote, CHADEMA Kielekeze nguvu zake kwa wakulima vijijini. Endapo tutawapa uongozi, basi “Mabilioni” atakayotoa Rais wangu mtarajiwa MMwanakijiji kwa wananchi wake yote yaelekezwe kwenye sekta ya Kilimo. Wakulima vijijini wasaidiwe kwa hali na mali ili waweze kujikwamua kutoka hapo walipo.

Napiga picha na kuwaona wamachinga na akina jobless wakiondoka mjini taratibu kufuata mabilioni yatakayoelekezwa vijijini. Kwa maana hiyo, hata kama si wote watakaorudi vijijini lakini wapo watakaoshawishika kufanya hivyo. Na hao watakaokwenda kupokea mabilioni ya Rais wetu wawekewe vizingiti vya makusudi wasiweze kurudi tena mijini!

Kazi ya kubadili utendaji ndani ya Jeshi la Polisi, Usalama wa Taifa, TAKUKURU, Madaktari, Manesi, Makarani, Mahakimu uchwala wapenda rushwa, n.k. itategemea ‘Ukali’ wa kiongozi ama viongozi wa juu wa Serikali.

Sie wa mwaka 47 tunakumbuka viongozi wa watumishi serikalini kama akina Mzee Benard Mulokozi aliyewahi kuwa Katibu Mkuu ofisi ya Waziri Mkuu na baadaye Utumishi, alivyokuwa ‘strict’, hakucheka wala hakuwa na mchezo na mtumishi yeyote yule Wizarani kwake. Nani angelithubutu kuomba ‘chai’ kwa mgeni aliyetaka huduma ama aliyetaka kuonana na afisa yeyote yule? Katibu Mkuu gani sasa hivi anayeweza kusimama kwenye gate la kuingilia ofisini ili kuwabana watumishi wachelewaji?

Siku hizi ni jambo la kawaida jijini Dar es Salaam kwa watumishi wa Serikali kufika ofisini saa 3 asubuhi badala ya saa 1.30 ana 2.00 kwa madai kwamba usafiri ni shida. Enzi za Mzee Mulokozi unaambiwa kama unataka kazi amka saa 10 ili uwahi kufika ofisini kwa wakati. Hao wachelewaji, wakiingia ofisini jambo la kwanza ni kuchukua birika na kuanza kuchemsha maji ya chai. Chai inaweza kunywewa kwa muda wa saa nzima huku watu wakitia stori. Kwa hiyo, hadi mtu aketi kitini kufanya kazi ni saa 5.00 mchana. Saa 7 au nane atatoka kwenda canteen kula lunch na kabla ya saa 9.30 kufika huondoka kwenda kuwahi usafiri wa kurudi nyumbani!

Mzee Mulokozi alikuwa na tabia ya kupita kila ofisi bila taarifa kuangalia kwamba kila mtumishi yuko mezani kwake anafanya kazi anayopaswa kufanya. Soga za yaliyotokea saloon ama disco weekend zilikuwa hazina nafasi maana hujui siku wala saa ambayo Katibu Mkuu ataamua kufanya ‘round’ zake! Leo hii, utakuta Katibu Mkuu au hata Waziri, kaketi juu ya meza ya Sekretari anatia stori! CHADEMA kazi ya kubadili watu mnayo!

Ni rahisi sana kuketi chini na kuweka sera na mikakati ya utekelezaji kwenye karatasi. Tatizo liko kwenye namna ya kutekeleza yaliyo kwenye karatasi. Wapo wanaosifu kwamba Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ilikuwa nzuri lakini utekelezaji ulikuwa mbovu katika kipindi ambacho uzalendo viongozi na wa wananchi ulikuwa hautiliwi shaka sana. Sembuse sasa? Hivi sasa wananchi wanategemea sana misaada na ufadhili na hakuna maadili yoyote ya kiutendaji yanayofuatwa.

Kazi ni ngumu, lakini kama kweli CHADEMA ama chama chochote kina nia ya dhati ya kutaka kuwaletea wananchi maendeleo yanayohitajika lazima kuwe na mipango mahususi ya kubadilisha fikra na kufufua uzalendo miongoni mwa wananchi wa nyanja zote.

‘Operesheni Sangara’ ikusanye wanachama lakini pia ianze kukusanya watakaokuwa viongozi wa kuweza kubadili fikra za wananchi zilizodumaa na kutekeleza yaliyomo kwenye orodha ndefu ya itikadi na Sera za CHADEMA.
 
Sina uhakika sana na kiwango cha uzito wa tafasiri zinazotolewa na wanasiasa juu ya kipimo cha umasikini na mwelekeo wa sera zao, lakini, ninaiamini methari; 'mwenzio akinyolewa wewe tia maji'. Amani ndani ya nyumba isipotambuliwa, huhalibiwa na wenye nyumba, na fundi asipokuwa mtutu umahili wake hutiliwa shaka. Zote ni harakati, yote ni mambo mema, 'ndugu zangu wenye wazo mbadara' tukomboeni katika mabaya, lakini mazuri bado tunayatamani. Ikiwezekana kauli zenu zitumike kwa maslahi ya taifa. Mkija kwenye majukwaa hatupendi matusi yenu, tunataka ukombozi kupitia fikra zenu. 'Ahsanteni na Mungu awabariki'
 
Huwezi kumuondoa JK madarakani kama huna tume huru ya uchaguzi...full stop!
 
Bhayanda,

Navyo elewa moja ya mikakati ya chadema kuwa wakiingia madarakani Nchi itakuwa na majimbo katika kumbukumbu zangu miaka ya nyuma nilikuwa nasoma sana makara ya Freeman Mbowe aliokuwa akiyatoa katika gazeti la RAI na moja kati ya hizo makara alipendekeza sana swala la majimbo na ninajua fika hilo swala atalitekeleza akiwa Rais,

Nikiwa na maaana gani kutokana na hiyo makara ya zito hapo juu ni wazi kuwa viongozi wetu wengi wao hawana mawasiliano ya karibu kwa jinsi ilivyo tajwa hapo, ni dhahili kuwa majimbo yataweza kutufanya tuka toka angalau kwenye hii hali na tukaenda mbele japo hatua hata mbili,
 
Naona vyama vya upinzani havina uelekeo wa kuwasaidia wananchi wa TZ, ni bora tumuenzi Nyerere kwa kukisafisha CCM kwani tayari kinawafuasi wengi hasa huko vijijini ambao wanaamini CCM just because of Mwalimu Nyerere.
Kuliko muda huu watu wanaanza kuumiza vichwa na vyama kama chadema ambavyo vimekosa hata internal ethics ndani ya uongozi wao, je tukiwapa nchi wataweza kweli hao wafanyabiashara?

I urge all Tanzanians to take part in reforming and cleaning CCM n we shall soon have a strong n progressive nation.

Remember Bob Marley said, "the truth is an offense but not a sin"

"The stone that a builder refuses will always b the head corner stone"
 
Back
Top Bottom