Tupo kwenye ugomvi kidogo namke wangu kuhusiana na suala langu la kuzidi kuwa namwili yaani big,,
Amemshirikisha na ndugu yakeupande wa baba yake suala hili.. mimi ni muungwana mno,aliniita na kuniambia nipunguze mwili namkera mkewangu
Sikupinga kwakuwa mimi nimtu mzima mwenye akili zangu... ila yeye alipokuwa akiongea aliongea nikama kwa shari hivi...
Kwanza nimemuona tu at first sight nikagundua ni MCHAWI... jicho lake la kushoto lilikuwa linawaka... ni mtu mwenyemaarifa tu ndiyo huona kitu hiki,na akajua kama nimemgundua...
Asubuhi yaleo nimeshindwa kwenda kazini kutokana na madhila niliyopata... nimeamka najiangalia kwenye kioo naona pingili za mgongo zimechomoza na mgongo umejipinda yaani curve
Nikasema nini hii? Mke wangu akawa ananiona normal tu...
Mara pua yangu ikadondoka chini... kwenye kioo nikaduwaa... badala ya kujiona mimi nikawa namuona huyo mjomba wa mke wangu
Huyu asili yake ni Germany na ana undugu wa mbali kidogo na mkewangu...
Namuona macho yanatema cheche huku anacheka sana
Mke wangu ananiuliza why umeduwaa? Namzuga tu ila nikawa ulimwengu mwingine kabisa...
Nikarudi kulala after kupiga simu yadharura ofisini... nikaamka saa sita mke wangu ananishangaa na kuniuliza kulikoni
Jamani nachoka kuandika mambo ni mengu mno... bado pingili hazijatoka zimekuwa ndefumno na mgongo umekuwawa kizee... mke wangu anaona kawaida tu hana macho ya kuona haya nipitiayo
Nitashinda vita hii kwa uwezo wake Yeye