Nusura ya Tanganyika ni anguko la CCM

Mshana Jr

Platinum Member
Joined
Aug 19, 2012
Posts
301,577
Reaction score
754,412
CCM imepagawa na uchaguzi mkuu mwakani.. Bado haijiamini licha ya kufanya maandalizi mengi ya mbinu chafu kushinda

CCM na viongozi wake wote wanatambua hawapendwi kabisa Tanganyika na huko Visiwani hali ni mbaya zaidi kuliko huku Bara! Lakini wanalazimisha kupendwa kwa namna yoyote ile.. Hii ni hatari sana!

Ogopa sana mtu aliyepagawa na jambo lolote lile.. Atafanya mambo ya ajabu bila ufahamu wake kamili.. Na yeyote atakayejaribu kumuasa anageuka kuwa adui na m'baya wake!

Wanaopagawa na mapenzi halafu waajua hawapendwi hulazimisha penzi kwa turufu ya pesa! Jamaa yangu mmoja alikuwa anahonga mpaka vitu vya mkewe wa ndoa

Katikati ya hii taharuki na kupagawa kwa CCM wamejiinua watu wenye uchu na nia mbaya na tunu zetu za taifa hasa ardhi na maliasili zake.. Hawa wanamwaga pesa balaa ili chama kishinde

Kwasasa wamevaa koti kubwa la wema na upole lakini rohoni ni wabaya shetani anasubiri.. Kila senti wanayotoa hata thumni wani document.. Hawanaga kazi za hasara hawa ndugu.. Mancha yao tutayaona baada ya uchaguzi na CCM ikishinda..

Juzi kwenye kongamano la TLS kuhusu watu waliopotea alihojiwa afande Murilo kama mbeba dhamana wa ulinzi na usalama wa uhai wetu.. Majibu yake kwenye hayo mahojiano badala ya kuleta tumaini yaliwaacha wengi na kihoro kikubwa

Kwa hali ilivyo na kwa yaliyokwisha tokea alipaswa awe ameshawajibika kwa vitendo.

Sasa huu ni mfano mmoja tu kuelekea uchaguzi mkuu. Hakuna palipoachwa salama kifedha.. Lakini hii mirija inayotiririsha mihela yote hiyo kwasasa kwa chama chawala..baada ya uchaguzi button itabadilika toka kwenye kutiririsha mpaka kwenye kunyonya na kufyonza

Na kama button ya kutiririsha Ilikuwa 4G ya kufyonza itakuwa 6G.

Kama button ya kutiririsha ilikuwa imefungwa engine ya carina ya kufyonza itafungwa ya semi trailer

Watanyonya kila kitu kisha watafyonza Mabaki.. Na hatutawafanya kitu kama mshirika wao atarudi mamlakani..!
 
Huu ujinga ukiendelea kuvumiliwa, hadi kufikia 2030, Tanganyika itakuwa iko hoi kiuchumi! Huku Zanzibar ikiendelea kuneemeka kupitia jasho la Watanganyika.
 
5. Muungano, Muungano
6. Lugha ya Kiswahili kufundishia
7. Uonga! Watu ni waoga kuliko
 
CCM imepagawa na uchaguzi mkuu mwakani.. Bado haijiamini licha ya kufanya maandalizi mengi ya mbinu chafu kushinda
Nimeshangaa kuona mgogoro wa kanisa na eneo huko arusha la muda eti juzi mchengerwa na makonda wamewarudishia kanisa na pesa juuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimejiuliza sana nikajua uchaguzi huooo!!!
 
Solution: Vijana ( umri 18- 45)wote bila kujali chama kumchagua Rais kutokea upinzani na makamu wa Rais .
Mengine yataangua automatically.
 
Nimeshangaa kuona mgogoro wa kanisa na eneo huko arusha la muda eti juzi mchengerwa na makonda wamewarudishia kanisa na pesa juuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimejiuliza sana nikajua uchaguzi huooo!!!
Ile ni takrima
 
Utafiti gani umefanya mpaka ukakupa ujasiri wa kuandika ulichoandika nadhari yako kiuhalisia hali haipo hivyo!

Nimeshangaa kuona mgogoro wa kanisa na eneo huko arusha la muda eti juzi mchengerwa na makonda wamewarudishia kanisa na pesa juuπŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ nimejiuliza sana nikajua uchaguzi huooo!!!
Hizo pesa zimetoka wapi?
 
Nipo tyar ila sio tundu wala asitokee CHADOMO huyo mpinzani
 
CCM imepagawa na uchaguzi mkuu mwakani.. Bado haijiamini licha ya kufanya maandalizi mengi ya mbinu chafu kushinda

!
katika bandiko hili lenye sura ya kiramli na tambiko,

CCM ambayo inapendwa zaidi na waTanzania mamilioni kwa mamilioni nchini, imetajwa katika paragraph karibu zote . Na hii ikimaanisha CCM inafurukuta pakubwa hata mojoni mwa mtoa hoja...

badala ya kujiandaa na uchaguzi, unaaanda sababu za kushindwa uchaguzi 🀣
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…