Nusura ya Tanganyika ni anguko la CCM

Nusura ya Tanganyika ni anguko la CCM

BREAKING: Tumepokea taarifa ya kuogofya kidogo kwamba kontena 72 za futi 40, zimefika Tanzania zikiwa na Shehena ya baiskeli za Rais Samia. Chanzo kinatutaarifu kwamba hizo baiskeli zimetolewa na kampuni ya Adani anayepewa kazi wizara ya Nishati na Tanesco. @TanzaniaLeaks
20241013_212235.jpg
20241013_212218.jpg
 
CCM imepagawa na uchaguzi mkuu mwakani.. Bado haijiamini licha ya kufanya maandalizi mengi ya mbinu chafu kushinda

CCM na viongozi wake wote wanatambua hawapendwi kabisa Tanganyika na huko Visiwani hali ni mbaya zaidi kuliko huku Bara! Lakini wanalazimisha kupendwa kwa namna yoyote ile.. Hii ni hatari sana!

Ogopa sana mtu aliyepagawa na jambo lolote lile.. Atafanya mambo ya ajabu bila ufahamu wake kamili.. Na yeyote atakayejaribu kumuasa anageuka kuwa adui na m'baya wake!

Wanaopagawa na mapenzi halafu waajua hawapendwi hulazimisha penzi kwa turufu ya pesa! Jamaa yangu mmoja alikuwa anahonga mpaka vitu vya mkewe wa ndoa

Katikati ya hii taharuki na kupagawa kwa CCM wamejiinua watu wenye uchu na nia mbaya na tunu zetu za taifa hasa ardhi na maliasili zake.. Hawa wanamwaga pesa balaa ili chama kishinde

Kwasasa wamevaa koti kubwa la wema na upole lakini rohoni ni wabaya shetani anasubiri.. Kila senti wanayotoa hata thumni wani document.. Hawanaga kazi za hasara hawa ndugu.. Mancha yao tutayaona baada ya uchaguzi na CCM ikishinda..

Juzi kwenye kongamano la TLS kuhusu watu waliopotea alihojiwa afande Murilo kama mbeba dhamana wa ulinzi na usalama wa uhai wetu.. Majibu yake kwenye hayo mahojiano badala ya kuleta tumaini yaliwaacha wengi na kihoro kikubwa

Kwa hali ilivyo na kwa yaliyokwisha tokea alipaswa awe ameshawajibika kwa vitendo.

Sasa huu ni mfano mmoja tu kuelekea uchaguzi mkuu. Hakuna palipoachwa salama kifedha.. Lakini hii mirija inayotiririsha mihela yote hiyo kwasasa kwa chama chawala..baada ya uchaguzi button itabadilika toka kwenye kutiririsha mpaka kwenye kunyonya na kufyonza

Na kama button ya kutiririsha Ilikuwa 4G ya kufyonza itakuwa 6G.

Kama button ya kutiririsha ilikuwa imefungwa engine ya carina ya kufyonza itafungwa ya semi trailer

Watanyonya kila kitu kisha watafyonza Mabaki.. Na hatutawafanya kitu kama mshirika wao atarudi mamlakani..!
Uko sahihi mkuu ila mpaka sasa kupigania vijana wa nchi hii kunahitaji moyo kizazi hiki cha kubeti,mpira na music ni kizazi kiovu kuwahikutokea. Ebu itisha maandamano ya kudai ajira kwa vijana,kupinga mfumko wa bei,mikopo %100 vyuo vikuu na mikopo kwa vijana waliomaliza shule alafu liwepo kongamano likitumbuizwa na Zuchu,Nandi,Diamond,Alikiba na wengine uone kundi tunalopigania litakimbilia wapi tena watatoa mpaka kiingilio
 
BREAKING: Tumepokea taarifa ya kuogofya kidogo kwamba kontena 72 za futi 40, zimefika Tanzania zikiwa na Shehena ya baiskeli za Rais Samia. Chanzo kinatutaarifu kwamba hizo baiskeli zimetolewa na kampuni ya Adani anayepewa kazi wizara ya Nishati na Tanesco. @TanzaniaLeaksView attachment 3124165View attachment 3124166
Mkuu usiangaike na wahuni awa nguvu tunayotumia kudai haki tuirudishe kuimarisha chumi zetu vijana wetu ni wapumbavu sana wakipewa baiskeli na pikipiki wanaona dunia imeisha.
 
1.Unamteka mtoto wa kike kwa mtutu wa bunduki

2.Kundi la wanaume saba wakatili mnakubali kwenda kumteka, kumdalilisha, kumnyanyasa na kutweza utu wa mwanamke kwa ujira wa fedha?

3.Mnafunga kitambaa usoni mwanamke kisha mnamtoa nyumbani kwake Kibiti mnamsafirisha hadi mapori ya Kisarawe kwenda kumnyanyasa na kumfanyia ukatili

4.Mnajitambulisha kuwa ni maafisa wa chombo cha dola kisha mnatumia gari la kodi za wananchi, pingu na bunduki zilizonunuliwa kwa kodi zetu.

5.Mnachana nguo za mwanamke aliyefunzwa kujistiri kwa dini yake safi ya kiislamu tangu utotoni na kumuacha utupu.

6.Mwanamke mmoja anashirikiana na wanaume saba kumshambulia na kumdhalilisha mwanamke mwenzake kwa ujira wa pesa tu

7.Mmemaliza kumfanyia ukatili Mwanamke mnamtekeleza maporini mnaondoka na kujiona wajanja... mnajiona mmeyapatia maisha kweli.

8.Nawakumbusha yupo Mungu juu anayeona kila kitu muda wote na sehemu zote. Ipo siku kabla hamjazikwa na kufukiwa na udongo huu mnaotumia kumwaga damu, mtakumbushwa kila tukio moja mlilotenda.

9.Nawaonea huruma ninyi watekaji na wauaji, kwa kuwa najua hamjui watu makatili kama ninyi mwisho wenu unakuwaga vipi.

10.Lakini niwahakikishie akili za upinzani na harakati hazizimwi kwa mtutu wa bunduki na kufuli la Jela tulifikiri mmejifunza kwa Hayati Magufuli

Hamtoweza kuua watu wote,wapo watakaobaki nyuma yetu,wao watatulipia visasi vyetu.hilo mnatakiwa kulielewa siku zote.

Hakunaga Jambo linafanywa na watu zaidi ya wawili likabakia kuwa siri.
Credit: Boni yai Twitter
20241023_051623.jpg
 
BREAKING: Tumepokea taarifa ya kuogofya kidogo kwamba kontena 72 za futi 40, zimefika Tanzania zikiwa na Shehena ya baiskeli za Rais Samia. Chanzo kinatutaarifu kwamba hizo baiskeli zimetolewa na kampuni ya Adani anayepewa kazi wizara ya Nishati na Tanesco. @TanzaniaLeaksView attachment 3124165View attachment 3124166

Hawa Adani si ndiyo wamechukua nafasi ya TICTS bandarini. Yaani hii ni kampuni ya hovyo kuliko maelezo

Wameondolewa TICTS ili kuleta ufanisi bandarini lakini cha ajabu hiyo kampuni ni ya hovyo kuliko TICTS.

Wahindi wanajifanya wawekezaji kumbe ni wabongo humu humu ambao hawana hata uwezo wa kuoperate bandari.

Hii nchi ni ya ajabu sana.
 
CCM 's life is entirely dependent on state apparatus. Period!
On the contrary, how can such an organization be recognized to be a "state apparatus"?
Clearly, there should be a better term to describe such an rotten organization!
 
  • Thanks
Reactions: G4N
On the contrary, how can such an organization be recognized to be a "state apparatus"?
Clearly, there should be a better term to describe such an rotten organization!
You are very true. Instead, we should call it CCM apparatus
 
Utafiti gani umefanya mpaka ukakupa ujasiri wa kuandika ulichoandika nadhari yako kiuhalisia hali haipo hivyo!
Unataka utafiti kwa vitu vilivyo mbele ya macho yako, vilivyo kwenye ncha ya pua yako???🤣🤣
UJINGA MZIGO!!!
 
Shule ya Msingi UBUNGO NATIONAL HOUSING NYUMA YA UBUNGO PLAZA IMEUZWA.

Wazazi wameambiwa Wakachukue watoto wao wakawatafutie Shule.

Shule ya SERIKALI inauzwa kama Peremende.

Shule iliyojengwa kwa KODI za wananchi kuna watu wachache wamekaa huko juu wameamua WAUZE.

Maelfu ya WATANZANIA yanaenda kuumia kwa kukosa huduma ya Elimu kwaajili ya Maamuzi ya VIGOGO wachache.

Hapa ndio tulipofikishwa TAIFA na CHUKUA CHAKO MAPEMA (CCM).
 
Back
Top Bottom