CCM imepagawa na uchaguzi mkuu mwakani.. Bado haijiamini licha ya kufanya maandalizi mengi ya mbinu chafu kushinda
Kwanza sii kweli kuwa CCM imepangawa na uchaguzi mkuu, kitu ni chako mwenyewe utapagawa vipi nacho?. Na kwenye kufanya maandalizi, please usiseme mbinu chafu, sema zile mbinu za kawaida za ki napenape!, kinyago ukichonge mwenyewe, hakiwezi kukutisha.
CCM na viongozi wake wote wanatambua hawapendwi kabisa Tanganyika na huko Visiwani hali ni mbaya zaidi kuliko huku Bara! Lakini wanalazimisha kupendwa kwa namna yoyote ile.. Hii ni hatari sana!
Sii kweli, CCM inapendwa sana na viongozi wake wanapendwa sana, usipime, ndio maana wanachaguliwa kwa kishindo, kila baada ya miaka mitano.
Ogopa sana mtu aliyepagawa na jambo lolote lile.. Atafanya mambo ya ajabu bila ufahamu wake kamili.. Na yeyote atakayejaribu kumuasa anageuka kuwa adui na m'baya wake!
Hakuna aliyepagawa, CCM haiwezi kupagawa wakati Tanzania ni yake ni mali yake!.
Katikati ya hii taharuki na kupagawa kwa CCM wamejiinua watu wenye uchu na nia mbaya na tunu zetu za taifa hasa ardhi na maliasili zake.. Hawa wanamwaga pesa balaa ili chama kishinde
CCM kushinda chaguzi zote haihitaji kumwaga pesa zozote balaa!, ile tshirt na kofia, kanga , dera na shibe ya siku moja zinatosha.
Kwasasa wamevaa koti kubwa la wema na upole lakini rohoni ni wabaya shetani anasubiri..
This is not fair comment, yaani CCM ni wabaya kuliko shetani!, not fair kabisa!.
Sasa huu ni mfano mmoja tu kuelekea uchaguzi mkuu. Hakuna palipoachwa salama kifedha.. Lakini hii mirija inayotiririsha mihela yote hiyo kwasasa kwa chama chawala..baada ya uchaguzi button itabadilika toka kwenye kutiririsha mpaka kwenye kunyonya na kufyonza
Duh...!.
Na kama button ya kutiririsha Ilikuwa 4G ya kufyonza itakuwa 6G.
Kama button ya kutiririsha ilikuwa imefungwa engine ya carina ya kufyonza itafungwa ya semi trailer
Duh...!.
Watanyonya kila kitu kisha watafyonza Mabaki..
Duh....!.
Na hatutawafanya kitu kama mshirika wao atarudi mamlakani..!
Duh...!, yaani unatumia neno "kama", as if kuna possibility asirudi!.
Hakuna kitu kizuri kama kuwa mkweli na kuukubali ukweli toka ndani ya nafsi yako, hata kama huupendi lakini lazima uukubali, kiukweli kabisa, CCM is there to stay!.
Rejea
Karibu