Fascinating
Senior Member
- May 14, 2025
- 146
- 351
Vikwazo ni suala moja, lakini kuvitekeleza ni suala jingine kabisa. Wavuvi wanasema, “Paka hawezi kumjeruria Mpishi“ 😂 Wazee wa teknolojia! NVIDIA imetangaza kurudi China bana . Juzi (jumatatu), kampuni hiyo ilisema inawasilisha maombi ya leseni kwa serikali ya Marekani ili kuruhusu mauzo ya GPU za H20 nchini China, na inatarajia kupata vibali hivi karibuni huku ikitazamia kuanza Deliveries ndani ya mwezi huu, kulingana na taarifa yao.
Mkurugenzi Mkuu wa NVIDIA, Jensen Huang, akiwa Beijing Jumanne, alisema hii ni “habari njema sana.” “Tutaanza kuuza chip za H20 hivi karibuni. Niko na furaha kubwa!” alisema, akiongeza kuwa atahudhuria Maonyesho ya Kimataifa ya Ugavi ya China yanayofanyika leo Jumatano. Hatua hii inakuja wakati mvutano kati ya Washington na Beijing unapungua, huku China ikilegeza udhibiti wa biashara ya madini ya nadra (rare earth minerals) na Marekani ikiruhusu huduma za programu zinazotumika kubuni chip kurudi China.
Hekaheka zilianza Aprili 2025 na wakati Trump alipoanza kujifanya kilanja wa Dunia na kuja na sera zilisababisha NVIDIA ipate hasara ya karibia ya Tsh Trilioni 15 iliyotokana na kukwama kwa mauzo ya chip hizo, hisa za Nvidia zilishuka kwa 6–6.9% Aprili 16, sawa na anguko la zaidi ya 30% kutokea thamani ya Januari ambapo ilikuwa dola 153.
China ilikuwa inakadiriwa kuchangia 13% ya mapato yote ya NVIDIA kwa mwaka 2025, hii ni zaidi ya Tsh Trilioni 45, Ambapo mauzo ya chip za H20 yenye thamani zaidi ya Tsh bilioni 48 yalikuwa hatarini kupotea kama sera za Trump dhini ya China zingeendelea.
Baada ya tamko hili, hisa za NVIDIA zimepanda kwa 4.2–4.5% Julai 15, zikifunga kwa dola 170.92, karibu na kiwango cha juu cha mwaka cha dola 172.79. Hii inaweza kurejesha mapato ya dola bilioni 15–20 na kuiwezesha kamppuni ya Nvidia kabiliana na ushindani wa kampuni za ndani ya China kama Huawei kwenye soka Chip hizo.
Huang pia alitangaza rasmi uwepo wa chip mpya ya RTX Pro GPU, iliyoundwa kwaajili ya simulation kama za “digital twins,” na Akili mnemba. Huang pia alisifu soko la AI la China kuwa “kubwa na lenye nguvu,” huku akibainisha kuwa 50% ya watafiti wa Akili mnmba duniani wako huko.
Nvidia kurudi kwenye soka la China ni ukombozi wa kumpuni ya Nvidia kutoka kwenye hatari ya kupoteza ushindani wa soko hasa nchini China. Ila hapa swali linalokuja ni moja tu;
Unadhani China itaendelea kutegemea kampuni za Marekani kwa teknolojia au itashinikiza makampuni ya ndani kwa motisha ili yakidhi mahitaji ya soko la chip na kupata uhuru wa kiteknolojia?
Reuters
CNN
Tech Wire Asia