Hagwila
Member
- Apr 18, 2019
- 82
- 99
Ingekuwa ni amri yangu; huyu Afisa Elimu Taaluma (W) Magu angeondolewa mara moja kwa sababu ni mla rushwa aliyekithiri na ayependelea waalimu wa kabila lake (Wajita).
Amekula fedha kwa walimu wengi sana aliowaahidi kuwapa ualimu mkuu (hao nao wanastahili kushughulikiwa kwa sababu kutoa rushwa ni kosa vilevile).
Lakini wapo wengi waliopenya kupata ualimu mkuu kwa mkondo huo wa Nyagabona, ambao wengi wao hawana uwezo kusimamia Utawala na Taaluma kwenye shule alizowapiganishia mpaka wakapewa kuziongoza.
Kwa mfano Mwl. CHIGULU ambaye yuko Shule ya Msingi KISESA "A" hapa Kisesa.
Ni shule kubwa ambayo ina watoto wengi, hivyo inahitaji kuwa na Mwalimu Mkuu makini, tofauti na huyu aliyeingizwa na Nyagabona kwa rushwa na ukabila.
Mwl. CHIGULU hawezi kusimamia shughuli za Utawala na Taaluma ipasavyo.
Kwenye mtihani wa darasa la VII wa mwaka huu, ilibainika kuwa wanafunzi 42 wa darasa hilo katika shule hiyo hawakuwa na Continuous Assessment na hawakuwa kwenye mfumo wa NECTA.
Baada ya kasoro hizo kubainika, Maafisa Taaluma (W) Magu, walibaini kwamba mwalimu mkuu huyo hayuko makini hata kwa vitu nyeti Kama CA na Prem Nos. za watoto ambao walikuwa wanafanya mitihani yao ya mwisho ya kumaliza elimu ya Msingi.
Lakini huyu Nyagabona, alikuwa kinyume na maafisa wenzake wote akimtetea Mwalimu Chigulu asichukuliwe hatua, eti kwa sababu shule yake ina watoto wengi!! Hiyo ni sababu?
Mbona zipo shule zingine nyingine zenye idadi kubwa ya wanafunzi kwa mfano WITA Shule ya Msingi, upuuzi kama huo haujatokea?
Afisa Elimu na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mkoa wetu wa Mwanza na Taasisi zingine za Usalama na Takukuru, fanyeni uchunguzi juu ya Afisa huyu ambaye kwa namna moja au nyingine anazorotesha juhudi za kuinua elimu katika Wilaya yetu ya Magu kwa kuwapiganishia waalimu wasiokuwa na uwezo wa uongozi kwa rushwa.
Naamini kwamba tabia yake hii mbaya inaathiri pia sifa ya watendaji wazuri happy idarani.
Tuondoleeni Nyagabona hapa idara ya elimu Magu.
Salaam Aleukum.