DOKEZO Nyagabona ni Afisa Elimu Taaluma (W) mla rushwa wilayani Magu

DOKEZO Nyagabona ni Afisa Elimu Taaluma (W) mla rushwa wilayani Magu

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Acheni majungu walimu Afisa Elimu yeye hana mamlaka ya kutoa Na kumpa mtu hiyo nafasi
Acheni unafiki walimu na majungu hizo nafasi zinatoka baada ya Mkurugenzi na Watu kutoka ofisi ya Mkuu wa Mkoa RAS kuzipitia na kumjua Mtu huyo kama ni sahihi ndio anapewa

Shida ya Walimu sifa zenu ni hizi kuchafuana,majungu,unafiki,waongo na watu waliokata Tamaa kbsa kbsa acheni mambo hayo

Ndugu niwaombe Tuu wachunguzeni sana walimu mtawajua kama una mtoto wako kaana nae taratibu na ulinza sifa za walimu wao atakachokuambia unaweza usiamini.
Usilolijua ni kama usiku wa giza!! Wewe hujui usemalo; na ninakushauri kuwa, kabla ya kusema chochote kwenye majukwaa kama haya fanya kwanza utafiti; acha kukurupuka.

NANI ALIKUAMBIA KWAMBA MWALIMU MKUU HATEULIWI NA AFISA ELIMU WA WILAYA?

Afisa Elimu wa Wilaya Msingi (kwenye mada iliyopo), ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mwalimu Mkuu kwenye shule zote za msingi za serikali kwenye Wilaya husika; ndiye Mkuu wa Idara ya Elimu msingi akiongoza maafisa wengine wa Elimu wilayani kama maafisa Taaluma, Vifaa na Takwimu, Elimu Maalum, Elimu ya Watu Wazima n.k.
Afisa Elimu wa Wilaya anaweza tu kuwashirikisha maafisa wenzake wilayani na mamlaka zingine za serikali (akipenda) katika uteuzi wa Mwalimu Mkuu, lakini siyo lazima.

Matatizo huanzia hapo kwenye ushirikiahwaji wa maafisa wengine idarani, hasa inapotokea kwamba kuna baadhi ya maofisa wasiokuwa waadilifu kama NYAGABONA anayetuhumiwa kwa rushwa, na wengine ambao hawajatajwa kwenye bandiko hilo kama JOHARI (ambaye pia anamyumbisha sana DEO Msingi aliyepo) kwa upendeleo kutokana na udini na jinsia.

JOHARI anapendelea sana waalimu wa dini yake, anapendelea pia waalimu wakuu wa kiume na kuwatweza waalimu wakuu wanawake wenzake kwa lugha chafu, dharau na vitisho vya kuwavua madaraka.

Ni kisiki cha mpingo hapo Idara ya Elimu Msingi Magu; yeye sasa amekuwa kama ndiye DEO Msingi, hasa kwa sababu ya kusimamia mfumo wa PREM.

Wakaguzi Ubora wa Elimu ni Idara inayojitegemea, haiko chini ya DED; lakini wanafanya kazi kwa karibu sana na Idara ya Elimu ya Wilaya kwa sababu ndio wanaosimamia shule zinazokaguliwa na Idara hiyo.

Tatizo lililopo hapo ni kuwa, kama kuna maofisa fulani wa idara ya Elimu wanataka kumkomoa Mwalimu Mkuu fulani ili wamng'oe madarakani lakini hawawezi kumshawishi DEO Msingi ili amng'oe Mwalimu Mkuu huyo, basi huwa wanawatumia maofisa wa idara ya ukaguzi ubora kwenda kwenye Kituo husika kufanya "ukaguzi Maalum" kwa lengo la kumkomoa Mwalimu Mkuu mlengwa; hata kwa kuja na ripoti ya ukaguzi yenye tuhuma za uongo dhidi ya Mwalimu Mkuu aliyekusudiwa kung'olewa kwa hila.

Mchezo huu ameufanya sana Nyagabona kwa kushirikiana na na wakaguzi wasiokuwa waadilifu kama Mkaguzi Mkuu Bwana KASWA aliyestaafu mwaka jana!! Mmoja wa waalimu waliofanyiwa mchezo huo na NYAGABONA akishirikiana na KASWA, ni mwalimu aliyewahi kuwa Mwalimu Mkuu pale shule ya msingi Itumbili na shule zinginezo.

Najua mtasema ni majungu; lakini huo ndio ukweli mchungu wa idara ya Elimu Magu, waalimu wanajua.
Cheo ni dhamana; KASWA amestaafu, sasa ni mkulima; NYAGABONA umehamishwa Magu, kaendelee kuwatesa waalimu wakuu Misungwi; lakini kumbuka, KILA KUBWA INA KUBWA YAKE.
 
Hata Mimi ningefanya hivyo,Hawa Wana muda mwingi wa kuipiga mishe kuliko Watumishi wa kada nyingine lakini kutwa majungu na malalamiko tu.
Hii ndio kada yenye likizo zaidi ya nne Kwa mwaka lakini hawaitumii wangejua wenzao wanatamani kuwa na likizo japo mbili Kwa mwaka ili wafanye mishe zao.
Wewe "SamakiMfalme XXIII" waalimu wa shule za serikali wana likizo moja tu kwa mwaka kama watumishi wengine wa umma.

Siyo kila Mwalimu anakuwa likizoni kila mhula wanafunzi wanapofunga shule.

Mzunguko wa likizo ya mwalimu huwa mwezi wa 6 kwenye likizo ya nusu mwaka ya wanafunzi, (Mid term) au mwezi wa 12 kwenye likizo ya mwisho wa mwaka ya wanafunzi (Annual term); acha kulisha umma matango pori samaki wewe!!

Kwamba anakuwa busy kiasi gani wakati shule zikiwa zimefungwa hiyo siyo juu yako; hayo ni ya mwajiri na mwajiriwa.

Hata nurse au doctor anapokuwa kazini, hawi busy kazini kwake masaa yote, upo wakati kazi hupungua na kama ni night shift wanapata hata muda wa kulala angalau Kwa kuegesha.

Hata Polisi au Zima Moto vituoni, hawako busy kukamata wavunja sheria muda wote; wanakuwepo kituoni wakiwa wame-relax lakini wako ON.

Hayo yote huyaoni, unamwona Mwalimu tu!!

Kuku akijisaidia mnasema kanya; lakini bata akijisaidia mnasema kaharisha!!

Mada ya Hagwila ni nyeti sana; maana viongozi kama Nyagabona na Johari; (wastaafu kama Kaswa na Salyankanga), ni viongozi wabadhirifu, wajeuri na waonevu sana kwa waalimu, hasa waalimu wakuu hapo Idara ya Elimu wilayani Magu; utadhani wao siyo waalimu au hawakuwahi kufundisha darasani!!

DEO Magu amezingirwa na watu ambao wanamharibia taswira yake kwa waalimu anaowaongoza kwenye wilaya hiyo; na kiwango cha ufaulu wilayani Magu kimeshuka kwa sababu ya waalimu kuvunjika moyo, kuwekwa madarakani waalimu wakuu wasiokuwa na uwezo kwa rushwa Kwa njia ya rushwa kupitia kwa Nyagabona kama Njala S/M Magu na Chiguru Kisesa "A" S/M na wengine kama Itumbili n.k.

Ni heri sana kwa Nyagabona kuondoka Magu DC, lakini ni ole kwa Misungwi DC; DEO Misungwi na maofisa wengine kuweni makini sana na Nyagabona.
 
Nyaghabhona I hope nu mukurya intina ghose umuikoma tatigha chiyo
Nyagabona ni mjita; a.k.a "chikaka". Kuna kijana mwingine hapo ofisi ya Elimu Magu anashikilia nafasi ya Afisa Vifaa na Takwimu (SLO - Statistics and Logistics Officer) anaitwa Buhatwa nadhani ni naye ni "chikaka." Sina uhakika kama ameidhinishwa na TAMISEMI au anakaimu; au amepachikwa tu na DED baada ya aliyekuwepo kustaafu maana alikuja hapo Magu akiwa anamalizia tu utumishi wake (hakuhudumu hata miaka miwili)

Huyo kijana Buhatwa ni mwiba kwa waalimu kuhusu malipo yao yanapopofanyika kwa hundi kama hundi hizo zinapita kusainiwa kwa Buhatwa. (Achilia mbali tabia yake mbaya ya kulala na waalimu wenye rika la dada na mama zake).

Ili mwalimu asainiwe hundi yake na Buhatwa, lazima mwalimu huyo ampe hela Buhatwa kwanza kulingana na thamani ya hundi.

Bila kumpa Buhatwa pesa, mwalimu atapigwa mikwala mingi ili mradi mwalimu huyo huamua kutoa pesa ili kuondoa udhia asainiwe hundi yake.

DED na DEO Msingi, mtupieni jicho huyo kijana; amekuwa kero kwa waalimu kuhusu hundi zao, hata na malipo mengine yanayowastahili waalimu kama malipo ya likizo, uhamisho na stahili zingine.
 
Ingekuwa ni amri yangu; huyu Afisa Elimu Taaluma (W) Magu angeondolewa mara moja kwa sababu ni mla rushwa aliyekithiri na ayependelea waalimu wa kabila lake (Wajita).

Amekula fedha kwa walimu wengi sana aliowaahidi kuwapa ualimu mkuu (hao nao wanastahili kushughulikiwa kwa sababu kutoa rushwa ni kosa vilevile).

Lakini wapo wengi waliopenya kupata ualimu mkuu kwa mkondo huo wa Nyagabona, ambao wengi wao hawana uwezo kusimamia Utawala na Taaluma kwenye shule alizowapiganishia mpaka wakapewa kuziongoza.

Kwa mfano Mwl. CHIGULU ambaye yuko Shule ya Msingi KISESA "A" hapa Kisesa.
Ni shule kubwa ambayo ina watoto wengi, hivyo inahitaji kuwa na Mwalimu Mkuu makini, tofauti na huyu aliyeingizwa na Nyagabona kwa rushwa na ukabila.

Mwl. CHIGULU hawezi kusimamia shughuli za Utawala na Taaluma ipasavyo.

Kwenye mtihani wa darasa la VII wa mwaka huu, ilibainika kuwa wanafunzi 42 wa darasa hilo katika shule hiyo hawakuwa na Continuous Assessment na hawakuwa kwenye mfumo wa NECTA.

Baada ya kasoro hizo kubainika, Maafisa Taaluma (W) Magu, walibaini kwamba mwalimu mkuu huyo hayuko makini hata kwa vitu nyeti Kama CA na Prem Nos. za watoto ambao walikuwa wanafanya mitihani yao ya mwisho ya kumaliza elimu ya Msingi.

Lakini huyu Nyagabona, alikuwa kinyume na maafisa wenzake wote akimtetea Mwalimu Chigulu asichukuliwe hatua, eti kwa sababu shule yake ina watoto wengi!! Hiyo ni sababu?

Mbona zipo shule zingine nyingine zenye idadi kubwa ya wanafunzi kwa mfano WITA Shule ya Msingi, upuuzi kama huo haujatokea?

Afisa Elimu na Afisa Tawala wa Mkoa wa Mkoa wetu wa Mwanza na Taasisi zingine za Usalama na Takukuru, fanyeni uchunguzi juu ya Afisa huyu ambaye kwa namna moja au nyingine anazorotesha juhudi za kuinua elimu katika Wilaya yetu ya Magu kwa kuwapiganishia waalimu wasiokuwa na uwezo wa uongozi kwa rushwa.
Naamini kwamba tabia yake hii mbaya inaathiri pia sifa ya watendaji wazuri happy idarani.

Tuondoleeni Nyagabona hapa idara ya elimu Magu.

Salaam Aleukum.
Poleni sana mkuu.Nina imani wenye dhamana wamekusikia.
 
Afisa Elimu Wilaya (Msingi) ni GLORY MTUI; alitokea Ilemela kuchukua mikoba ya SALYANKANGA aliyestaafu ambaye naye alikuwa mla rushwa, siyo ya pesa tu; mpaka na ya mwilini; cheo ni dhamana, sasa yuko mitaani.
GLORY yuko vizuri sana kwa maamuzi ambayo huwa anayafanya yeye mwenyewe maana ana uwezo mkubwa wa kutafakari, kuchambua na kusimamia mambo baada ya kuwa mamlakani angalau kwa muda sasa.
Tatizo analokabiliana nalo Glory ni hao maofisa vichomi waliomzingira hapo ofisini kwake; wengi wao siyo waadilifu; wala rushwa kama NYAGABONA aliyehamishiwa Misungwi; JOHARI MWASHA anaonea na kunyanyasa sana waalimu kwa lugha chafu zisizokuwa na staha; hasa wasiokuwa wa dini yake!! Kichomi mwingine aliyestaafu mwaka jana ni aliyekuwa Mkaguzi Mkuu KASWA; alikuwa anatumika na maofisa wa idara ya Elimu wasiokuwa waadilifu kunyanyasa waalimu wanaolenga kuwaumiza; hata kwa kuandika taarifa ya uongo ili kumwumiza mlengwa kama alivyofanyiwa mwalimu mmoja aliyekuwa mkuu shule ya Msingi Itumbili akang'olewa, badala yake akawekwa mwalimu aliyetoa pesa kwa NYAGABONA.
KASWA naye sasa wanapishana na SALYANKANGA mitaani; ama kweli cheo ni dhamana.
GLORY anapaswa kusimamia maamuzi yake kutokana na maono yake; asimwendekeze JOHARI MWASHA ambaye hapo idarani anaogopeka na waalimu kuliko DEO hata DED mwenyewe.
Afisa Elimu mkuu ktk hyo wilaya ni nani
 
Afisa Elimu Wilaya (Msingi) ni GLORY MTUI; alitokea Ilemela kuchukua mikoba ya SALYANKANGA aliyestaafu ambaye naye alikuwa mla rushwa, siyo ya pesa tu; mpaka na ya mwilini; cheo ni dhamana, sasa yuko mitaani.
GLORY yuko vizuri sana kwa maamuzi ambayo huwa anayafanya yeye mwenyewe maana ana uwezo mkubwa wa kutafakari, kuchambua na kusimamia mambo baada ya kuwa mamlakani angalau kwa muda sasa.
Tatizo analokabiliana nalo Glory ni hao maofisa vichomi waliomzingira hapo ofisini kwake; wengi wao siyo waadilifu; wala rushwa kama NYAGABONA aliyehamishiwa Misungwi; JOHARI MWASHA anaonea na kunyanyasa sana waalimu kwa lugha chafu zisizokuwa na staha; hasa wasiokuwa wa dini yake!! Kichomi mwingine aliyestaafu mwaka jana ni aliyekuwa Mkaguzi Mkuu KASWA; alikuwa anatumika na maofisa wa idara ya Elimu wasiokuwa waadilifu kunyanyasa waalimu wanaolenga kuwaumiza; hata kwa kuandika taarifa ya uongo ili kumwumiza mlengwa kama alivyofanyiwa mwalimu mmoja aliyekuwa mkuu shule ya Msingi Itumbili akang'olewa, badala yake akawekwa mwalimu aliyetoa pesa kwa NYAGABONA.
KASWA naye sasa wanapishana na SALYANKANGA mitaani; ama kweli cheo ni dhamana.
GLORY anapaswa kusimamia maamuzi yake kutokana na maono yake; asimwendekeze JOHARI MWASHA ambaye hapo idarani anaogopeka na waalimu kuliko DEO hata DED mwenyewe.
Hilo litazamwe, DEO ndio sauti ya mwisho ktk idara Hao wengine wote ni wadogo kwake kimamlaka yéyé ndiye final say inatakiwa awakemee
 
Kabla hujamshutuma nyagabona jiulize je wale wakurugenzi na madas hawana wakubwa waliowasaidia kupata hivyo vyeo?????
 
Ni haki ya mtumishi kupandishwa cheo na mamlaka inayomsimamia; lakini hilo linapaswa kufanyika kwa haki, si kwa rushwa na upendeleo.
Nyagabona anashutumiwa kwa kupokea rushwa Kwa waalimu na kushinikiza mamlaka za uteuzi za walimu wakuu kwa kigezo cha ukongwe wake katika idara ya Elimu Magu. Kwa kufanya hivyo, waalimu wakuu wanaoteuliwa kwa msingi ya rushwa, bila kujali elimu yao, uwezo wao na weledi wao wanashindwa kuleta mafanikio kwenye vituo vyao, badala yake mambo yanavurugika vituoni; mifano ni mingi kama shule ya msingi Magu, Itumbili, Kisesa "A" n.k; huko kote kuna waalimu wakuu ambao wamepata nafasi hizo kwa kutoa rushwa kwa Nyagabona; wao na wenzao wengine, WAMEANDAA SHEREHE MAALUM YA KUMUAGA NYAGABONA "WAKIMWOMBOLEZEA" KWA KUHAMISHIWA MISUGWI; wanajua nguzo yao imeng'olewa, wakaze misuli🤓🤓
Kabla hujamshutuma nyagabona jiulize je wale wakurugenzi na madas hawana wakubwa waliowasaidia kupata hivyo vyeo?????
 
Back
Top Bottom