Nyahoza: Barua yetu kwa CHADEMA inasema kusimamisha chama kwa muda, sio kufuta

Nyahoza: Barua yetu kwa CHADEMA inasema kusimamisha chama kwa muda, sio kufuta

View attachment 3589086


Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema barua waliyoiandikia CHADEMA imemaanisha kuwasimamisha kwa muda (suspension) au kuwatoza faini endapo watawakuta na hatia kulingana na maelezo watakayotoa na sio kuwafuta kwenye daftari la Msajili, kama ambavyo imekuwa ikijadiliwa.

Soma zaidi: Msajili wa Vyama vya Siasa Ailima barua CHADEMA na kuipa Siku 13 Kujieleza

Katika barua hiyo iliyoandikwa Mei 7, chama hicho kimetakiwa kutoa maelezo kuhusu kauli ya Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, aliyotangaza mpango wa kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Msajili pia amenukuu kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Oliver Kisaka, aliyekuwa akizungumzia matukio ya maandamano ya Oktoba 29, 2025, huku akiwasifu wananchi wa Kibamba, Dar es Salaam, kwa kushiriki maandamano hayo.

Akizungumzia adhabu itakayopewa CHADEMA, Nyahoza amesema itatetegemea maelezo yatakayotolewa na chama hicho, ndipo watawasimamisha au kuwatoza faini.

“Kusimamisha usajili sio kuwafuta, ni kusimamisha kwa muda. Itategemea maelezo yao, kama watakiri makosa tutaangalia. Huo muda wa kuwasimisha itategemea pia maelezo yao,” amesema.

Alipoulizwa kwa nini wasitumie busara katika kipindi hiki ambacho, Serikali imeahidi kuanza mchakato wa maridhiano, Nyahoza alijibu, “Busara inamaanisha kwanza wazingatie sharia. Chadema wana wanasheria na wana wasomi, kweli inawezekana wakae kamati kuu watoe kauli kama zile? Maridhiano haimaanishi watu wavunje sharia.”

Ameongeza: “Kwa mfano wewe umepata safari ya kwenda Ulaya kusoma, ukawa unaenda ubalozini kupewa visas, ukivunja sharia barabarani unataka polisi asikuchukulie hatua kwa sababu una safari ya Ulaya? Utataka usamehe kwa sababu unachelewa ubalozini? Umevunja sharia utachukuliwa hatua.”

Hata hivyo, amesema adhabu hizo zitategemea maelezo watakayotoa CHADEMA. “Tumewapa nafasi wajieleze, kwa hiyo tutaangalia walichoeleza, ndio tuchukue hatua.”

Kwa nini hawaichukulii hatua CCM?

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya vyama vya upinzani kwamba Ofisi ya Msjili haiwachukulii hatua CCM, Nyahoza alisema wamekuwa wakiwaandikia barua mara kadhaa wanapokosea.

“CCM tunawaandikia barua sana na huwa wanajibu. Mfano ni wakati yule kijana wa UVCCM Mkoa wa Kagera (Faris Buruhani) aliyewataka Polisi wasiwatafute watakaopotea kwani watawapoteza watu wanaotumia simu zao kutukana viongozi. Tuliwaandikia barua na walijibu kwa kuomba radhi.

“Si mlimsikia Dk Emmanuel Nchimbi (Makamu wa Rais) wakati huo akiwa Katibu mkuu wa CCM, akimkemea? CCM wao tunapowaandikia barua huwa hawatangazi lakini wanakuja kuomba radhi na wanwakemea makada wao,” amesema.

Alisema pia hawajaichukulia hatua ACT Wazalendo kwenye tamko lao la kupinga ripoti ya Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani Oktoba 29 kwa kuwa hawakutoa kauli chafu.

“Umesikia tumewalalamikia ACT Wazalendo walipopinga ripoti ya Jaji Chande (Mohamed Othman Chande)? Godbless Lema amefanya mkutano Arusha, umesikia tumemlalamikia? Boniyai (Boniface Jacob) alikuwepo umesikia tumemlalamikia?

“Lakini CHADEMA wao unaona yule kiongozi wao akiwasifu walioandaa mandamano anaita mashujaa, hiyo ni sawa? Halafu tukiwaandikia barua hawawaonyi makada wao, wanawalinda.

“Heche ameitisha maandamano kutaka Lissu (Tundu Lissu) aachiliwe huru, tu aliye mahakamani anaachiliwaje huru kwa maandamano? Wanatakiwa wafuate sheria. Mahakama ina taratibu zake, wazifuate hizo.

"Ni sawa wewe uwe na mtoto wako, unaletewa mashitaka majirani kwamba ana tabia mbaya, utamwonya au utamtetea?" amehoji.
Huyu baada ya miaka mitano utashangaa nae ni mbunge wa ccm
 
Mwanasheria wa chama gani kasema hadharani 'nchi inafffirwa' ukiacha wa chadema?.. kiongozi wa chama gani alisema nchi itawaka moto na hapatakua na uchaguzi na kweli vurugu zikatokea?..hicho chama kifutwe,ni janga kwa taifa
Yule wa cdm kuleta ebola chama chake kinafuywa lini? Cdm hakuna kujinyenyekeza kwa hayo majizi. Hakuna wajinga wa kudumu.
 
Well said Ndugu Nyahoza

Chadema kujifanya last born nchi hii na kuwaacha sio malezi
 

Attachments

  • IMG-20260515-WA0013.jpg
    IMG-20260515-WA0013.jpg
    271 KB · Views: 10
Uzuri Mungu ni wa haki... Haiwezekani UVCCM wametoa matamko mabaya ya kuondoa uhai wa watu hawajawahi option ya kufungiwa chama au kulipa faini.
 
Ofisi ya msajili wa vyama vya siasa ifutwe, vyama vya siasa visajiliwe Brela. Halafu ruzuku kwa vyama vya siasa pia ifutwe; kila chama cha siasa kiwe kinajitafutia mapato yake chenyewe; kikishindwa, basi kinajitoa kwenye siasa. Halafu mali za CCM ilizopata wakati wa chama kimoja, yaani majengo na viwanja vya mpira, zirudishwa serikalini.
 
Sheria zinasemaje kwani kuandamana kwa kitu chochote ni kosa?

Acha kukisimamisha hiyo tumeshazoea, wakifute kabisa.
 
Tumechokozwa sana sasa ni wakati wakuwa offensive na sio defensive! People's power lazima wasikie!
 
Yule wa cdm kuleta ebola chama chake kinafuywa lini? Cdm hakuna kujinyenyekeza kwa hayo majizi. Hakuna wajinga wa kudumu.
Kusema kuleta ebola na kusema nchi imefirrrwa ni sawa?
 
Taasisi zinaongozwa na maboga yaliyovaa suit, huyu na kina Chande hawana tofauti na type ya kina Mwijaku, generation ya hovyo kuwahi kutokea Tanzania, yatapita tuu
 
Back
Top Bottom