Nyahoza: Barua yetu kwa CHADEMA inasema kusimamisha chama kwa muda, sio kufuta

View attachment 3589086

Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema barua waliyoiandikia CHADEMA imemaanisha kuwasimamisha kwa muda (suspension) au kuwatoza faini endapo watawakuta na hatia kulingana na maelezo watakayotoa na sio kuwafuta kwenye daftari la Msajili, kama ambavyo imekuwa ikijadiliwa.

Soma zaidi: Msajili wa Vyama vya Siasa Ailima barua CHADEMA na kuipa Siku 13 Kujieleza

Katika barua hiyo iliyoandikwa Mei 7, chama hicho kimetakiwa kutoa maelezo kuhusu kauli ya Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, aliyotangaza mpango wa kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.

Msajili pia amenukuu kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Oliver Kisaka, aliyekuwa akizungumzia matukio ya maandamano ya Oktoba 29, 2025, huku akiwasifu wananchi wa Kibamba, Dar es Salaam, kwa kushiriki maandamano hayo.

Akizungumzia adhabu itakayopewa CHADEMA, Nyahoza amesema itatetegemea maelezo yatakayotolewa na chama hicho, ndipo watawasimamisha au kuwatoza faini.

“Kusimamisha usajili sio kuwafuta, ni kusimamisha kwa muda. Itategemea maelezo yao, kama watakiri makosa tutaangalia. Huo muda wa kuwasimisha itategemea pia maelezo yao,” amesema.

Alipoulizwa kwa nini wasitumie busara katika kipindi hiki ambacho, Serikali imeahidi kuanza mchakato wa maridhiano, Nyahoza alijibu, “Busara inamaanisha kwanza wazingatie sharia. Chadema wana wanasheria na wana wasomi, kweli inawezekana wakae kamati kuu watoe kauli kama zile? Maridhiano haimaanishi watu wavunje sharia.”

Ameongeza: “Kwa mfano wewe umepata safari ya kwenda Ulaya kusoma, ukawa unaenda ubalozini kupewa visas, ukivunja sharia barabarani unataka polisi asikuchukulie hatua kwa sababu una safari ya Ulaya? Utataka usamehe kwa sababu unachelewa ubalozini? Umevunja sharia utachukuliwa hatua.”

Hata hivyo, amesema adhabu hizo zitategemea maelezo watakayotoa CHADEMA. “Tumewapa nafasi wajieleze, kwa hiyo tutaangalia walichoeleza, ndio tuchukue hatua.”

Kwa nini hawaichukulii hatua CCM?

Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya vyama vya upinzani kwamba Ofisi ya Msjili haiwachukulii hatua CCM, Nyahoza alisema wamekuwa wakiwaandikia barua mara kadhaa wanapokosea.

“CCM tunawaandikia barua sana na huwa wanajibu. Mfano ni wakati yule kijana wa UVCCM Mkoa wa Kagera (Faris Buruhani) aliyewataka Polisi wasiwatafute watakaopotea kwani watawapoteza watu wanaotumia simu zao kutukana viongozi. Tuliwaandikia barua na walijibu kwa kuomba radhi.

“Si mlimsikia Dk Emmanuel Nchimbi (Makamu wa Rais) wakati huo akiwa Katibu mkuu wa CCM, akimkemea? CCM wao tunapowaandikia barua huwa hawatangazi lakini wanakuja kuomba radhi na wanwakemea makada wao,” amesema.

Alisema pia hawajaichukulia hatua ACT Wazalendo kwenye tamko lao la kupinga ripoti ya Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani Oktoba 29 kwa kuwa hawakutoa kauli chafu.

“Umesikia tumewalalamikia ACT Wazalendo walipopinga ripoti ya Jaji Chande (Mohamed Othman Chande)? Godbless Lema amefanya mkutano Arusha, umesikia tumemlalamikia? Boniyai (Boniface Jacob) alikuwepo umesikia tumemlalamikia?

“Lakini CHADEMA wao unaona yule kiongozi wao akiwasifu walioandaa mandamano anaita mashujaa, hiyo ni sawa? Halafu tukiwaandikia barua hawawaonyi makada wao, wanawalinda.

“Heche ameitisha maandamano kutaka Lissu (Tundu Lissu) aachiliwe huru, tu aliye mahakamani anaachiliwaje huru kwa maandamano? Wanatakiwa wafuate sheria. Mahakama ina taratibu zake, wazifuate hizo.

"Ni sawa wewe uwe na mtoto wako, unaletewa mashitaka majirani kwamba ana tabia mbaya, utamwonya au utamtetea?" amehoji.
CDMIkiwa huru inawakosesha Raha sana nadhani watafarijika wakiifungia wakisikia mahali tu inafanya mkutano hawalali lakini kuwanyamazisha watu ni jambo baya sana ukiziba njia zote zakupumilia Aidha huto mtu afe au atapetape
 
Katika mashtaka haya mlalamikaji ni nani? Je, wale makada wa CCM waliosema CCM inashinda kwa bao la mkono mbona hawakuandikiwa barua? Na kuna kada alisema wenyeviti wa CCM hawakuchaguliwa na CCM bali walipitishwa na CCM kwa mabavu. Mbona hakuandikowa barua. Mama Samuya alisema watakaoandamana tarehe 29 atapigwa risasi na kweli wakaua mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia. Mbona yeye hajawahi kuandikiwa barua?

Hawa wasjili wa CCM wanaudhi sana. Wanataka watu tuseme tuonekane wabaya. Wapuuzi wakubwa!
 
Mwanasheria wa chama gani kasema hadharani 'nchi inafffirwa' ukiacha wa chadema?.. kiongozi wa chama gani alisema nchi itawaka moto na hapatakua na uchaguzi na kweli vurugu zikatokea?..hicho chama kifutwe,ni janga kwa taifa

Kufikiri kukifuta CDM ndo muarobaini wa matatizo & migogoro ya kisiasa nchini ni wrong move na kujilisha upepo.

Kama ambavyo kukifungia hakukuleta nafuu yeyote kuelekea mo29, Hata kukifuta hakutaleta nafuu yeyote juu ya yajayo.
 
Futa hicho chama, maelezo ya kijinga jinga hayana maana
 
Katika mashtaka haya mlalamikaji ni nani? Je, wale makada wa CCM waliosema CCM inashinda kwa bao la mkono mbona hawakuandikiwa barua? Na kuna kada alisema wenyeviti wa CCM hawakuchaguliwa na CCM bali walipitishwa na CCM kwa mabavu. Mbona hakuandikowa barua. Mama Samuya alisema watakaoandamana tarehe 29 atapigwa risasi na kweli wakaua mamilioni ya raia wasiokuwa na hatia. Mbona yeye hajawahi kuandikiwa barua?

Hawa wasjili wa CCM wanaudhi sana. Wanataka watu tuseme tuonekane wabaya. Wapuuzi wakubwa!
Kwa zile kauli za CCM zilikuwa zina ujinai ilipaswa police wawaite viongozi wao na kuwahoji au kuwapeleka mahakamani ni vile tu vyombo vyetu vya Usalama havipo huru mtu anasema ni kiongozi wa chinjachinja alafu still yupo uraiani
 
Not long ago some of us warned CDM wajifunze kula na kipofu.

Hili sio zimwi walijualo (yaani CCM) alikuli likakwisha. Ambao wanajua mipaka ya kuvumiliana kisiasa.

La hasha hawa ni maafisa usalama hawajui siasa, wanajua kutumia katiba kwenye coaching yao. Muhimu kwao ni kushika mpini na hawajui ustaarabu wa siasa.

Empathy is not there thing hawa watu, muhimu kwao ni kuvizia uvunjifu wa legality ya kuumiza upinzani.

Hawa watu wamenogewa na utamu wa kutumbua kodi za watanzania na urahisi wa kupiga deal za serikali. Hawako tayari kuachia huu mteremko Samia aliowapa.

Sasa we endelea kuropoka lolote ambalo wanaloweza kulitumia kisheria uone kama watakuacha.

It has nothing to do with CCM Kinachoendelea Tanzania kwa sasa; but watu wenye tamaa kwenye vyombo vya usalama na ulinzi.
 
Hizi takataka mbili lazima ziunganishwe kwenye kesi ya ICC. Walishirikiana na Ibrahim Lipumba kuihujuma CUF hadi ikameguka,na baada ya kufanikiwa hilo wakamgeuka Lipumba kwani hawakua na matumizi naye tena, hawa ni washenzi kabisa.
Yaani wahuni sana. Alafu hakunaga ukomo kwenye hizo nafasi zao??
 
Back
Top Bottom