field marshall1
JF-Expert Member
- Sep 17, 2017
- 2,061
- 4,686
Huyo Nyahoza Sisti ni mpumbavu asiye na akili hata kidogo, Kwa hiyo CCM wakiomba msamaha wanasamehewa, wengine hawasamehewi? Acha upumbavu wewe Nyahoza, mnaionea sana CHADEMA. Mshenzi wewe Nyahoza.Kwa hiyo akikosea mtu chama kinafutwa???? Mbona CCM wanahusika na vurugu na kuua chama cha Mapinduzi hakifutwi?View attachment 3589086
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema barua waliyoiandikia CHADEMA imemaanisha kuwasimamisha kwa muda (suspension) au kuwatoza faini endapo watawakuta na hatia kulingana na maelezo watakayotoa na sio kuwafuta kwenye daftari la Msajili, kama ambavyo imekuwa ikijadiliwa.
Soma zaidi: Msajili wa Vyama vya Siasa Ailima barua CHADEMA na kuipa Siku 13 Kujieleza
Katika barua hiyo iliyoandikwa Mei 7, chama hicho kimetakiwa kutoa maelezo kuhusu kauli ya Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, aliyotangaza mpango wa kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Msajili pia amenukuu kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Oliver Kisaka, aliyekuwa akizungumzia matukio ya maandamano ya Oktoba 29, 2025, huku akiwasifu wananchi wa Kibamba, Dar es Salaam, kwa kushiriki maandamano hayo.
Akizungumzia adhabu itakayopewa CHADEMA, Nyahoza amesema itatetegemea maelezo yatakayotolewa na chama hicho, ndipo watawasimamisha au kuwatoza faini.
“Kusimamisha usajili sio kuwafuta, ni kusimamisha kwa muda. Itategemea maelezo yao, kama watakiri makosa tutaangalia. Huo muda wa kuwasimisha itategemea pia maelezo yao,” amesema.
Alipoulizwa kwa nini wasitumie busara katika kipindi hiki ambacho, Serikali imeahidi kuanza mchakato wa maridhiano, Nyahoza alijibu, “Busara inamaanisha kwanza wazingatie sharia. Chadema wana wanasheria na wana wasomi, kweli inawezekana wakae kamati kuu watoe kauli kama zile? Maridhiano haimaanishi watu wavunje sharia.”
Ameongeza: “Kwa mfano wewe umepata safari ya kwenda Ulaya kusoma, ukawa unaenda ubalozini kupewa visas, ukivunja sharia barabarani unataka polisi asikuchukulie hatua kwa sababu una safari ya Ulaya? Utataka usamehe kwa sababu unachelewa ubalozini? Umevunja sharia utachukuliwa hatua.”
Hata hivyo, amesema adhabu hizo zitategemea maelezo watakayotoa CHADEMA. “Tumewapa nafasi wajieleze, kwa hiyo tutaangalia walichoeleza, ndio tuchukue hatua.”
Kwa nini hawaichukulii hatua CCM?
Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya vyama vya upinzani kwamba Ofisi ya Msjili haiwachukulii hatua CCM, Nyahoza alisema wamekuwa wakiwaandikia barua mara kadhaa wanapokosea.
“CCM tunawaandikia barua sana na huwa wanajibu. Mfano ni wakati yule kijana wa UVCCM Mkoa wa Kagera (Faris Buruhani) aliyewataka Polisi wasiwatafute watakaopotea kwani watawapoteza watu wanaotumia simu zao kutukana viongozi. Tuliwaandikia barua na walijibu kwa kuomba radhi.
“Si mlimsikia Dk Emmanuel Nchimbi (Makamu wa Rais) wakati huo akiwa Katibu mkuu wa CCM, akimkemea? CCM wao tunapowaandikia barua huwa hawatangazi lakini wanakuja kuomba radhi na wanwakemea makada wao,” amesema.
Alisema pia hawajaichukulia hatua ACT Wazalendo kwenye tamko lao la kupinga ripoti ya Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani Oktoba 29 kwa kuwa hawakutoa kauli chafu.
“Umesikia tumewalalamikia ACT Wazalendo walipopinga ripoti ya Jaji Chande (Mohamed Othman Chande)? Godbless Lema amefanya mkutano Arusha, umesikia tumemlalamikia? Boniyai (Boniface Jacob) alikuwepo umesikia tumemlalamikia?
“Lakini CHADEMA wao unaona yule kiongozi wao akiwasifu walioandaa mandamano anaita mashujaa, hiyo ni sawa? Halafu tukiwaandikia barua hawawaonyi makada wao, wanawalinda.
“Heche ameitisha maandamano kutaka Lissu (Tundu Lissu) aachiliwe huru, tu aliye mahakamani anaachiliwaje huru kwa maandamano? Wanatakiwa wafuate sheria. Mahakama ina taratibu zake, wazifuate hizo.
"Ni sawa wewe uwe na mtoto wako, unaletewa mashitaka majirani kwamba ana tabia mbaya, utamwonya au utamtetea?" amehoji.
Watu kama huyu, rekodi yake inayojulikana waziwazi kuwa mtetezi wa maovu ndani ya nchi hii; hawa ndio watakaolipa sehemu ya maovu yao waliyowafanyia waTanzania nchi hii ikishapata uhuru wake kamili toka kwa waovu hawa."Ni sawa wewe uwe na mtoto wako, unaletewa mashitaka majirani kwamba ana tabia mbaya, utamwonya au utamtetea?" amehoji.
Don’t shoot the agent. Shoot the principal. Umesahau kwamba fazafaka wa Kizimkazi (MINO=Muslim in name only) ndiye yuko nyuma ya huu upumbavu?Huyu kiongozi anasahau kwamba kuna kufa ? Cuf yeye, nccr yeye, chadema yeye, Act wazalendo yeye, kila barua ya kuwakandamiza wapinzani ni yeye tu.Sisi waislam tunatakiwa kutenda haki maana siku ya hesabu ni siku ngumu sana kwa binaadam. Cjui imani nyengine zinasemaje
Ukweli ni kwamba kunahitajika kuwepo na njia mbadala za kupambana na hawa "maaskari" wanaotumika kuhakikisha kuwepo kwa uovu nchini.Kina Heche pamoja na Viongozi wengine wa Chadema wanzuiwa kuingia gerezani kumtembelea Mwenyekiti wao. Wamewatumia Mawakili wao kushinikiza Mahakama kuendelea na kesi ile bila mafanikio.
Sasa walitaka lugha gani itumike kwa Chadema ili kuweza kupaza sauti kwa magumu wanayoyapitia??
Kuna watu wa hovyo sana kwenye nchi hii utadhani wana hati miliki kwa raia wenzao. Upuuzi tena upuuzi unaoleta hasira.
Unamshikilia Kiongozi wao kwa siku 400+ bila kesi kuendelea halafu eti mnataka ndugu zake wafuasi wake waendelee kukaa kimya huku Mpendwa wao akisota gerezani bila sababu? Kama ana hatia kwanini kesi isiendelee ahukumiwe kwa HAKI??
Kuna suala la Uvccm Kagera, kiongozi wake kutoa kauli zile eti aliomba msamaha yakaisha. Kweli?? Watu wanatekwa wanapotezwa wanauawa nae na chama chake kimyaa Msajili kimyaa? Mungu yupo na atalipa kisasi ni suala la muda tu.
Kuna yule kama wao wa Longido aliyesema alikesha maporini kuhakikisha ccm inapata ushindi. Pamoja na kda huyo kusimamishwa Ukuu wa Wilaya, Msajili aliwahi kukiandikia ccm barua kutaka ufafanuzi kwenye hilo??View attachment 3589340
Uzuri Mungu ni wa haki... Haiwezekani UVCCM wametoa matamko mabaya ya kuondoa uhai wa watu hawajawahi option ya kufungiwa chama au kulipa faini.
Hivyo vyama vyengine ni watoto wa ccm na ofisi ya msajili ndie mtoto wa mwanzo wa ccm wa pili ni polisi na watatu ni mahakama. Huwezi mkuta mtoto akamgeuka mzee wake kwasababu ya jirani tu.Kila siku ni wao na Chadema tu, vyama viko zaidi ya ishirini ila wao ni Chadema tu, hopeless kabisa
Kwanini unauma maneno wakati inajulikana kabisa kuwa Act na Chauma ni mpango kando wa Ccm ama kwa lugha nyingine wanaitwa Ccm 'B'?Sioni dalili za hayo maridhiano yajayo.
Dalili ya mvua ni mawingu.
Nafikiri kutakuwa na exclusion ya Chadema kwenye hivyo vikao.
Badala yake Chauma na ACT watafanywa replacement ya chadema.
Halafi ionekane kama vyama vya upinzani wameridhiana na Chama tawala.......wakati Chauma na ACT hawajawahi hata kufokeana na CCM.
View attachment 3589086
Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa, Sisty Nyahoza amesema barua waliyoiandikia CHADEMA imemaanisha kuwasimamisha kwa muda (suspension) au kuwatoza faini endapo watawakuta na hatia kulingana na maelezo watakayotoa na sio kuwafuta kwenye daftari la Msajili, kama ambavyo imekuwa ikijadiliwa.
Soma zaidi: Msajili wa Vyama vya Siasa Ailima barua CHADEMA na kuipa Siku 13 Kujieleza
Katika barua hiyo iliyoandikwa Mei 7, chama hicho kimetakiwa kutoa maelezo kuhusu kauli ya Makamu Mwenyekiti wake, John Heche, aliyotangaza mpango wa kufanya maandamano nchi nzima kushinikiza kuachiwa huru kwa Mwenyekiti wa chama hicho, Tundu Lissu.
Msajili pia amenukuu kauli ya Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Korogwe, Mkoa wa Tanga, Oliver Kisaka, aliyekuwa akizungumzia matukio ya maandamano ya Oktoba 29, 2025, huku akiwasifu wananchi wa Kibamba, Dar es Salaam, kwa kushiriki maandamano hayo.
Akizungumzia adhabu itakayopewa CHADEMA, Nyahoza amesema itatetegemea maelezo yatakayotolewa na chama hicho, ndipo watawasimamisha au kuwatoza faini.
“Kusimamisha usajili sio kuwafuta, ni kusimamisha kwa muda. Itategemea maelezo yao, kama watakiri makosa tutaangalia. Huo muda wa kuwasimisha itategemea pia maelezo yao,” amesema.
Alipoulizwa kwa nini wasitumie busara katika kipindi hiki ambacho, Serikali imeahidi kuanza mchakato wa maridhiano, Nyahoza alijibu, “Busara inamaanisha kwanza wazingatie sharia. Chadema wana wanasheria na wana wasomi, kweli inawezekana wakae kamati kuu watoe kauli kama zile? Maridhiano haimaanishi watu wavunje sharia.”
Ameongeza: “Kwa mfano wewe umepata safari ya kwenda Ulaya kusoma, ukawa unaenda ubalozini kupewa visas, ukivunja sharia barabarani unataka polisi asikuchukulie hatua kwa sababu una safari ya Ulaya? Utataka usamehe kwa sababu unachelewa ubalozini? Umevunja sharia utachukuliwa hatua.”
Hata hivyo, amesema adhabu hizo zitategemea maelezo watakayotoa CHADEMA. “Tumewapa nafasi wajieleze, kwa hiyo tutaangalia walichoeleza, ndio tuchukue hatua.”
Kwa nini hawaichukulii hatua CCM?
Alipoulizwa kuhusu malalamiko ya vyama vya upinzani kwamba Ofisi ya Msjili haiwachukulii hatua CCM, Nyahoza alisema wamekuwa wakiwaandikia barua mara kadhaa wanapokosea.
“CCM tunawaandikia barua sana na huwa wanajibu. Mfano ni wakati yule kijana wa UVCCM Mkoa wa Kagera (Faris Buruhani) aliyewataka Polisi wasiwatafute watakaopotea kwani watawapoteza watu wanaotumia simu zao kutukana viongozi. Tuliwaandikia barua na walijibu kwa kuomba radhi.
“Si mlimsikia Dk Emmanuel Nchimbi (Makamu wa Rais) wakati huo akiwa Katibu mkuu wa CCM, akimkemea? CCM wao tunapowaandikia barua huwa hawatangazi lakini wanakuja kuomba radhi na wanwakemea makada wao,” amesema.
Alisema pia hawajaichukulia hatua ACT Wazalendo kwenye tamko lao la kupinga ripoti ya Tume ya Kuchunguza Uvunjifu wa Amani Oktoba 29 kwa kuwa hawakutoa kauli chafu.
“Umesikia tumewalalamikia ACT Wazalendo walipopinga ripoti ya Jaji Chande (Mohamed Othman Chande)? Godbless Lema amefanya mkutano Arusha, umesikia tumemlalamikia? Boniyai (Boniface Jacob) alikuwepo umesikia tumemlalamikia?
“Lakini CHADEMA wao unaona yule kiongozi wao akiwasifu walioandaa mandamano anaita mashujaa, hiyo ni sawa? Halafu tukiwaandikia barua hawawaonyi makada wao, wanawalinda.
“Heche ameitisha maandamano kutaka Lissu (Tundu Lissu) aachiliwe huru, tu aliye mahakamani anaachiliwaje huru kwa maandamano? Wanatakiwa wafuate sheria. Mahakama ina taratibu zake, wazifuate hizo.
"Ni sawa wewe uwe na mtoto wako, unaletewa mashitaka majirani kwamba ana tabia mbaya, utamwonya au utamtetea?" amehoji.
sema masalo mkuu itapendeza zaidWasomi wa awamu hii hawana tofauti na nyanya zilizooza.
Umeliweka vizuri, asante
“Busara inamaanisha kwanza wazingatie sharia.
ukivunja sharia barabarani
Umevunja sharia utachukuliwa hatua.”
"Sharia" ndiyo kitu gani??Maridhiano haimaanishi watu wavunje sharia.”
Sasa hapo ni sawa na kujamba na kujufunika shukaSioni dalili za hayo maridhiano yajayo.