Nyakati zimegoma kuubusu upara wa Zidane

Nyakati zimegoma kuubusu upara wa Zidane

marcoveratti

JF-Expert Member
Joined
Sep 21, 2017
Posts
1,019
Reaction score
1,824
Mhenga mmoja wa kizungu, akiwa na ubongo uliovimbiwa hekima alishika kalamu nakuandika nukuu hii. "You can't be a champ for life. One day you will go off and some else will come. Alimaanisha hivi. "Huwezi kuwa bingwa milele, ni lazima siku moja uondoke ili bingwa mwingine aje."

Zidane angeamua kuiishi nukuu hii kwa vitendo. Wakati Frolentino Perezz alipompigia simu ya kumuhitaji arudi kuiokoa tena Real Madrid. Iliyokuwa inazama kwa kasi katikati ya bahari ya fedhea.

Zidane angemkatia simu perezz. Na msemo wa kwamba tajiri anuniwi, angeuacha ubaki kwenye notisi za somo la Kiswahili. Hii ndio njia aliyoitumia mwenzie Pep Guardiola. Kuilinda heshima aliyoitengeneza katalunya. Kwa msaada wa miguu ya mchawi mfupi "Lionel Messi."

Wakati Zidane anaandika history ya kuchukua uefa champions league mara tatu mfululizo. Dunia iligoma kusadiki yale ni matokeo ya ubora wa mbinu zake. Wengi waliamini Zidane anasafiria nyota. Itokanayo na miujiza iliyokuwa ikiishi kwenye viatu vya mtoto wa kireno. Mnyama Cristiano Ronaldo.

Ukiacha kumpiga kichwa Marco Materrazi, kwenye fainal za kombe la dunia 2006. Kwenye mechi kati ya Italy na Ufaransa. Dhambi mbaya aliyowahi kuitenda Zinedine Zidane katika maisha ya mpira. Ni aliporidhia kuirejea tena ardhi ya bernabeu kama mkufunzi.

Nafikiri wakati anafanya maamuzi ya kurudi. Zidane akushirikiana vema na halmashauri ya ubongo wake. Hili lilikuwa kosa kubwa la kiufundi.

Zidane angeitazama kesho kwa jicho latatu. Kama angeona kuna utata katika maamuzi yake. Angeomba hata msaada wa VAR. Kabla ya kukubali ombi la yule tajiri mjeuri anayenuka pesa. Huenda labda pia ukosefu wa ajira mpya. Ulimsukuma Zidane akubali wito wa Perezz bila kujua kwamba.

Anarudi bernabeu kufuata koleo. Kwaajili ya kuanzisha mradi wakuichimbia kaburi CV yake.

Matokeo mabovu na mpira usiovutia wanaocheza Real Madrid siku hizi. Hivi ni vitu viwili ambavyo vimegeuka kansa. Vinaitafuna kwa kasi heshima ya Zizzou. Kipigo toka kwa PSG na sare dhidi Club bruge pale bernabeu.

Hivi ni vitu vilivyoilaza I.C.U ndoa ya Perezz na Zidane. Nakama muda wowote Perezz atampungia mkono wa kwaheri Zidane. Haitakuwa simulizi ya kuisisimua dunia.

Mikono iliyo expire nakujificha kwenye glove's za Thibaut Cortour. Pamoja na miguu iliyokosa msaada toka kwa Heden Hazzard. Hivi ni baadhi ya vitu vinavyoashiria kifo cha ajira ya Zidane bernabeu.

Madrid kushika mkia kwenye kundi lenye timu za Galatasary, PSG na Club bruge. Hili ni tusi chafu zaidi ya nyeti ya mswahili. Hata miwani ya Perezz inasikitika inapoutazama msimamo wa kundi.

Hii ni ishara ya wazi zidane amefirisika maarifa. Amepoteza kitabu chenye mbinu za kushinda mechi za usiku wa ulaya. ubongo wake umepata ugumba. Hauna uwezo wa kushika mimba ya mawazo na kuzaa fikra mpya. Na nyakati za utukufu pia, zimegoma kuubusu upara wake."
PicsArt_10-03-11.48.08.jpeg
 
Baada ya zidane kutangaza kuoñdoka Madrid akili yangu ilijiuliza ni lini zizzou àtarejea tena bernabeu kutupinga sisi kua alikuta ubora akasafiria nyota? Lakini, kama ni nyota mbona wengine walishindwa na kikosi hiki hiki?
Sasa nipo na kalamu yangu ya sino mwekundu kujisahishia.
 
Madrid sio mbovu saana ila inahitaji muda tuu wa wachezaji kuelewana. Sio kwamba zidane ameishiwa mbinu bali ni players ndio wameishiwa nguvu wengi umri ushawapita wale aliobeba nao uefa tatu.

Naamini with time madrid itakaa sawa.
 
Madrid sio mbovu saana ila inahitaji muda tuu wa wachezaji kuelewana. Sio kwamba zidane ameishiwa mbinu bali ni players ndio wameishiwa nguvu wengi umri ushawapita wale aliobeba nao uefa tatu.

Naamini with time madrid itakaa sawa.
Kabisa yule Marcelo ndo mpira gani ule?
 
madrid inaongoza LaLIGA na hata mpira bado si wa hovyo kama kipindi kilichopita. Nimetizama mechi zote za RM kuna makosa ya wachezaji yanaigharimu timu, kama juzi MODRIC kwa mechi ya Brugge na kukosa striker wa maana. Zizzou ni kocha mzuri... NA atapindua hili grp
 
Back
Top Bottom