Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,768
- 49,949
Uovu hata ulindwe namna gani, hauwezi kudumu.
Utawala wa makaburu ulikuwa na kila kitu, kuanzia silaha, tekinolojia, vituo vya tafiti za kisayansi mpaka utajiri wa pesa. Makaburu walifanya tafiti mpaka kuja na dawa ambazo watu weusi waliofika kwenye hospitali za Serikali walipewa ili wasiweze kupata watoto tena. Na akina mama wakienda kujifungua hospitali, huyo mtoto awe wa mwisho. Wakaenda mbali kutafuta makombora ambayo yangeweza kutambua rangi, ili yaue watu weusi pekee (hili hawakufanikiwa). Lakini pamoja na hayo yote, makaburu , katika muda ulio sahihi walinyosha mikono, haki ikashinda.
Serikali ya CCM ya sasa imejaa kila aina ya uovu, kuanzia kuwaua watu, kuwateka, kuwatesa mpaka kuwabambikia kesi za ajabu. Kwa kupitia vyombo vya Serikali na watu wake, wanafanya ubaguzi, wanatapanya na kuiba kodi za wananchi kadiri watakavyo. Wamejaa kiburi, tena wakitamka wazi kuwa watatawala milele, maana yake watanzania wataendelea kuuawa milele, kutekwa milele, kuteseka milele, kubambikiwa kesi milele, na kodi zao kuendelea kuibiwa milele. Kusema kwamba CCM itatawala milele maana yake CCM imejipa utukufu wa Mungu, kwani kwa dini zote, tunaamini Mungu pekee yake ni wa milele, hana mwanzo wala mwisho. Hii ina maana CCM imefikia kwenye kilele cha kiburi.
Lakini kwa hakika, nyakati zaja, tena hazipo mbali, CCM itapotea, CCM itaonekana ni alama kubwa ya uovu Tanzania. Mtu yeyote akiambiwa ni mwanachama, shabiki au mpambe wa CCM, atachukia na kuona ametukanwa tusi lisiloweza kuelezeka. Wale ambao walikuwa viongozi ndani ya CCM au Serikali yake, wataishi katika unyonge wa ajabu, maana ni wao pekee hawataweza kumdanganya yeyote kuwa hawakuwahi kuwa miongoni mwa madhulumati ya CCM.
UJUMBE MUHIMU:
Kushirikiana na muuaji, mtesaji na mdhulumu haki za watu, huku ukijua kabisa kuwa huyu ni muuaji mdhulumu haki, na wewe unakuwa ni sehemu ya uovu wake.
Jitenge na CCM, jitenge na uovu, uiepuke laana.