Nyakati Zinakuja Ambapo Hakuna Atakayependa Ajulikane Aliwahi Kuwa Mwanachama Wa CCM.

Uovu hata ulindwe namna gani, hauwezi kudumu.
Utawala wa makaburu ulikuwa na kila kitu, kuanzia silaha, tekinolojia, vituo vya tafiti za kisayansi mpaka utajiri wa pesa. Makaburu walifanya tafiti mpaka kuja na dawa ambazo watu weusi waliofika kwenye hospitali za Serikali walipewa ili wasiweze kupata watoto tena. Na akina mama wakienda kujifungua hospitali, huyo mtoto awe wa mwisho. Wakaenda mbali kutafuta makombora ambayo yangeweza kutambua rangi, ili yaue watu weusi pekee (hili hawakufanikiwa). Lakini pamoja na hayo yote, makaburu , katika muda ulio sahihi walinyosha mikono, haki ikashinda.

Serikali ya CCM ya sasa imejaa kila aina ya uovu, kuanzia kuwaua watu, kuwateka, kuwatesa mpaka kuwabambikia kesi za ajabu. Kwa kupitia vyombo vya Serikali na watu wake, wanafanya ubaguzi, wanatapanya na kuiba kodi za wananchi kadiri watakavyo. Wamejaa kiburi, tena wakitamka wazi kuwa watatawala milele, maana yake watanzania wataendelea kuuawa milele, kutekwa milele, kuteseka milele, kubambikiwa kesi milele, na kodi zao kuendelea kuibiwa milele. Kusema kwamba CCM itatawala milele maana yake CCM imejipa utukufu wa Mungu, kwani kwa dini zote, tunaamini Mungu pekee yake ni wa milele, hana mwanzo wala mwisho. Hii ina maana CCM imefikia kwenye kilele cha kiburi.

Lakini kwa hakika, nyakati zaja, tena hazipo mbali, CCM itapotea, CCM itaonekana ni alama kubwa ya uovu Tanzania. Mtu yeyote akiambiwa ni mwanachama, shabiki au mpambe wa CCM, atachukia na kuona ametukanwa tusi lisiloweza kuelezeka. Wale ambao walikuwa viongozi ndani ya CCM au Serikali yake, wataishi katika unyonge wa ajabu, maana ni wao pekee hawataweza kumdanganya yeyote kuwa hawakuwahi kuwa miongoni mwa madhulumati ya CCM.

UJUMBE MUHIMU:
Kushirikiana na muuaji, mtesaji na mdhulumu haki za watu, huku ukijua kabisa kuwa huyu ni muuaji mdhulumu haki, na wewe unakuwa ni sehemu ya uovu wake.

Jitenge na CCM, jitenge na uovu, uiepuke laana.
Mtu wa kwanza kujificha atakuwa Mulirro
 
tuanze kuwa note wapambe hasa wasanii+ ili siku table iki turn down tana anzanao ikiwa bado subuhi kabisa kwa maana hao ni miongoni mwa wanao tuchelewesha
 
Muomba Mungu hachoki, kila lenye mwanzo halikosi kuwa na mwisho.

Tulisema hivi wakati ule wa Jiwe tukaambiwa ni dua la kuku halimpati mwewe.
 
nyakati zijazo
wao ndio wataomba maridhiano
zile ngou za kijani na bendera yao zitachukiwa na jamii
uzuri watakao kuwa madarakani watawasamehe ili kuepuka chuki na
matabaka ktk jamii

yajayo yatafurahisha wote kwa usawa na haki pasipo upendeleo
 
Uovu hata ulindwe namna gani, hauwezi kudumu.
Utawala wa makaburu ulikuwa na kila kitu, kuanzia silaha, tekinolojia, vituo vya tafiti za kisayansi mpaka utajiri wa pesa. Makaburu walifanya tafiti mpaka kuja na dawa ambazo watu weusi waliofika kwenye hospitali za Serikali walipewa ili wasiweze kupata watoto tena. Na akina mama wakienda kujifungua hospitali, huyo mtoto awe wa mwisho. Wakaenda mbali kutafuta makombora ambayo yangeweza kutambua rangi, ili yaue watu weusi pekee (hili hawakufanikiwa). Lakini pamoja na hayo yote, makaburu , katika muda ulio sahihi walinyosha mikono, haki ikashinda.

Serikali ya CCM ya sasa imejaa kila aina ya uovu, kuanzia kuwaua watu, kuwateka, kuwatesa mpaka kuwabambikia kesi za ajabu. Kwa kupitia vyombo vya Serikali na watu wake, wanafanya ubaguzi, wanatapanya na kuiba kodi za wananchi kadiri watakavyo. Wamejaa kiburi, tena wakitamka wazi kuwa watatawala milele, maana yake watanzania wataendelea kuuawa milele, kutekwa milele, kuteseka milele, kubambikiwa kesi milele, na kodi zao kuendelea kuibiwa milele. Kusema kwamba CCM itatawala milele maana yake CCM imejipa utukufu wa Mungu, kwani kwa dini zote, tunaamini Mungu pekee yake ni wa milele, hana mwanzo wala mwisho. Hii ina maana CCM imefikia kwenye kilele cha kiburi.

Lakini kwa hakika, nyakati zaja, tena hazipo mbali, CCM itapotea, CCM itaonekana ni alama kubwa ya uovu Tanzania. Mtu yeyote akiambiwa ni mwanachama, shabiki au mpambe wa CCM, atachukia na kuona ametukanwa tusi lisiloweza kuelezeka. Wale ambao walikuwa viongozi ndani ya CCM au Serikali yake, wataishi katika unyonge wa ajabu, maana ni wao pekee hawataweza kumdanganya yeyote kuwa hawakuwahi kuwa miongoni mwa madhulumati ya CCM.

UJUMBE MUHIMU:
Kushirikiana na muuaji, mtesaji na mdhulumu haki za watu, huku ukijua kabisa kuwa huyu ni muuaji mdhulumu haki, na wewe unakuwa ni sehemu ya uovu wake.

Jitenge na CCM, jitenge na uovu, uiepuke laana.
CCM ni ya waTanzania wote.
Na Tanzania nzima ni CCM.

kinyume cha hapo ni ramli chonganishi, ushirikina na kafara za malofa waropokaji , vibaka na matapeli wa kisiasa nchini waliokosa angenda na kupoteza uelekeo.

CCM itatawala dola ya Tanzania mpaka ukamilifu wa dahari gentleman.
Kuhusu hili, tafadhali ukamueleze hata mwenyekiti wa chama chako bila kumficha :BASED:
 
  • Nzuri
Reactions: Tui
CHADEMA ina watabiri wangapi kwani? Kaeni chini mumteue mtabiri mmoja anayejielewa.
 
  • Thanks
Reactions: Tui
Nyakati Zinakuja Ambapo Hakuna Atakayependa Ajulikane Aliwahi Kuwa Mwanachama Wa CCM..
Hizo nyakati ndo zinapiga hodi sasa.

Imagine mafisadi wa ccm wanatumia mabilioni ya Watanzania maskini kufadhili maigizo ya kijinga sana ya CHAKUUMA wakati hispitali za serikali hazina dawa, na nchi ina matatizo chungu nzima!!!
 
Back
Top Bottom