Nyakato, Mwanza: Wananchi walalamika kuzidiwa kwa TANESCO

Nyakato, Mwanza: Wananchi walalamika kuzidiwa kwa TANESCO

Ndokeji

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
698
Reaction score
476
Katika Jiji la Mwanza Tanesco Nyakato imeshindwa kutatua kero za wananchi. Wananchi wamelalamika kutofungiwa umeme kwa muda mrefu huku wakidai kupeleka form zao katika kituo hicho kwa mda mrefu wakiahidiwa surveyor kupigiwa simu bila Mafanikio

Manager wa Tanesco amedai wanagali mbili na surveyo wawili na hiyo ndio chamgamoto inayofanya washindwa kuwahudumia wananchi.

Waziri wa Nishati fatilia hiki kilio kimekuwa kikubwa sana.

Inasemekana surveyor akipewa hela siku hiyo hiyo anaenda na umeme unafungwa.

Hii Rushwa ya Tanasco inakuja kwa kasi.

Wako Mwanadiplamasia
 
Mh Samia Angaza jicho lako katika kitengo hicho
 
Nyakato ipi?

Kuna mecco, Kangaye, National, nundu, Nundu B , kivukoni.
 
Mh Samia Angaza jicho lako katika kitengo hicho

Balozi wa nyumba 10.

Mwenyekiti wa mtaa

Diwani wa Kata

Mbunge

Katibu tawala

Mkuu wa wilaya

Mkuu wa mkoa

Mkurugenzi

Katibu mkuu wizara

N waziri

Waziri

Spika wa Bunge

W/Mkuu

M/rais

Ndio unalipata Jicho la rais.
 
Lazima wazidiwe baada ya mama yetu Mpenda haki na mtetezi wa kweli wa Watu Wenye kipato duni kushusha bei kuwa 27000 ya ukweli.

Tuwe wavumilivu kwasababu nachokiona ni tactics za ku buy time maana hata wakipamabana Watu wote wafungiwe haraka umeme hautatosha, tusubiri bwawa likamilike
 
Tumepokea taarifa kwa ufatilijia na hatua zaidi, Tafadhali tusaidie namba ya mmoja wapo aliyedai kutoa rushwa au kumbwa rushwa tuifanyie kazi.Jm
Safi sana, kama kila taasisi itafuata mfano huu. Rushwa katika taasisi zinazotoa huduma kwa mwananchi itaenda kupotea.
itakuwa vema mkijulisha wananchi ni nani aliyehusika na rushwa hiyo ,pamoja na hatua za kinidhamu zilizochukuliwa dhidi yake.
 
Tumepokea taarifa kwa ufatilijia na hatua zaidi, Tafadhali tusaidie namba ya mmoja wapo aliyedai kutoa rushwa au kumbwa rushwa tuifanyie kazi.Jm
Naomba mnifahamishe kama siku hizi hamuunganishi mteja mwenye uhu
hitaji wa nguzo tatu maana suvyeyor alinijulisha kuwa siwezi pewa control number kwasababu Hadi kwangu zitahitajija nguzo tatu.

Nami nilimjulisha ninauwezo wa kulipia hata 2million lakini alikataa kunipa control ya kulipia.naomba tanesco ufafanuzi nina shida na umeme sana.
 
Naomba mnifahamishe kama siku hizi hamuunganishi mteja mwenye uhuhitaji wa nguzo tatu maana suvyeyor alinijulisha kuwa siwezi pewa control number kwasababu Hadi kwangu zitahitajija nguzo tatu.

Nami nilimjulisha ninauwezo wa kulipia hata 2million lakini alikataa kunipa control ya kulipia. Naomba tanesco ufafanuzi nina shida na umeme sana.
Wateja waliopo umbali wa zaidi ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu iliyopo wanapaswa kufikiwa kupitia miradi ya usambazaji umeme inayoendelea hivyo maeneo kama hayo yanategemea na hatua za utekelezaji wa mradi husika.

Ikumbukwe kuwa usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo hiyo kitaalamu hatuiti service line. Tambua kuwa mteja halipii nguzo wala umbali bali analipia gharama halisi za kuunganishiwa umeme hivyo kutaja vifaa kama nguzo zitakazotumika sio sahihi kwa kuwa sio nguzo tu zinazotumika.Jm
 
Wateja waliopo umbali wa zaidi ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu iliyopo wanapaswa kufikiwa kupitia miradi ya usambazaji umeme inayoendelea hivyo maeneo kama hayo yanategemea na hatua za utekelezaji wa mradi husika.Ikumbukwe kuwa usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo hiyo kitaalamu hatuiti service line. Tambua kuwa mteja halipii nguzo wala umbali bali analipia gharama halisi za kuunganishiwa umeme hivyo kutaja vifaa kama nguzo zitakazotumika sio sahihi kwa kuwa sio nguzo tu zinazotumika.Jm
Na vipi kwa mtu anayetaka kuunganisha umeme kwa nyumba iliyo karibu na nguzo, ni kushusha waya uingie kwenye nyumba, gharama zake zikoje maana nimeenda ofisi za tanesco nikaambiwa nilipie laki 3 na elfu 30, na huku nasikia pia gharama zimeshushwa mpaka 27000/=, je kipi ni sahihi, naomba msaada wako
 
Je umeambiwa lini? Ofisi ya wapi? Tafadhali tambua punguzo hili lilianza tarehe 4 Juni 2021 hivyo kabla ya hapo bei ilikuwa 321000
 
Wateja waliopo umbali wa zaidi ya mita 120 kutoka kwenye miundombinu iliyopo wanapaswa kufikiwa kupitia miradi ya usambazaji umeme inayoendelea hivyo maeneo kama hayo yanategemea na hatua za utekelezaji wa mradi husika.Ikumbukwe kuwa usambazaji wa umeme maeneo mbalimbali unaenda kwa awamu mbalimbali hivyo hiyo kitaalamu hatuiti service line. Tambua kuwa mteja halipii nguzo wala umbali bali analipia gharama halisi za kuunganishiwa umeme hivyo kutaja vifaa kama nguzo zitakazotumika sio sahihi kwa kuwa sio nguzo tu zinazotumika.Jm
Shukran sana kwa maelezo yako mazuri , je kwa wale ambao tayari line ipo karibu kabisa ISIYO ZIDI mita 30 na tayari walishapewa control namba na kuzilipia tayari tangu February 2021 hadi sasa hawajaunganishiwa umeme Inakuwaje ? taarifa zipo TANESCO wilayani hawapati majibu ya kuridhisha, huko huko kanda ya ziwa unawashauri nini ?
 
Tanesco Hapa JF Mmekuwa Hai Muda Wote Kutoa Ufafanuzi
Ila Mahitaji Sasa Ni Makubwa Ongezeni Kasi Zaidi
 
Shukran sana kwa maelezo yako mazuri , je kwa wale ambao tayari line ipo karibu kabisa ISIYO ZIDI mita 30 na tayari walishapewa control namba na kuzilipia tayari tangu February 2021 hadi sasa hawajaunganishiwa umeme Inakuwaje ? taarifa zipo TANESCO wilayani hawapati majibu ya kuridhisha, huko huko kanda ya ziwa unawashauri nini ?
Tafadhali onyesha namba ya simu? Wilaya na jina ulilolipia tufanyie kazi taarifa zako mkuu wetu
 
Tafadhali onyesha namba ya simu? Wilaya na jina ulilolipia tufanyie kazi taarifa zako mkuu wetu
Shukran tena, Taarifa za watu si busara kuzianika hapa, aidha nipe means ya kukupata nikupe zote kikamilifu, unaweza ni box nipe namba zako nitakupigia mm mwenyewe.
 
Shukran tena, Taarifa za watu si busara kuzianika hapa, aidha nipe means ya kukupata nikupe zote kikamilifu, unaweza ni box nipe namba zako nitakupigia mm mwenyewe.
Ukurasa huu unaruhusu kuweka hapa kwenye wall au inbox karibu inbox tukuhudumia mkuu wetu
 
Back
Top Bottom