Nyalandu aleta madaktari bingwa 50 kumuunga mkono Rais Samia

Nyalandu aleta madaktari bingwa 50 kumuunga mkono Rais Samia

Kasemea jimbo moja la kalifonia ndo wametoka hao, kua na madakitari 1.7m sio kigezo cha kua na specialists au madakitari bigwa hapa Tanzania tuna wa hudumu wa afya laki tisa na zaidi ila kuna wilaya na mikoa zaidi ya nusu zina kosa specialists au gynaecologist wa masuala ya magonjwa ya wanawake ambayo ni muhimu kwa kila kata........kwahiyo idadi kubwa ya wa hudumu wa afya aimanishi kua na idadi kubwa ya specialists tena mifupa tu.
2,406
California ranks among the highest states in the U.S. with 2,406 active orthopedic surgeons. The state has 800 more orthopedic surgeons than Texas, which is ranked second with 1,621.
 
Huyo ametuletea mateja sio dakitari
Tusidharau kila kitu.
Jamaa hiyo connection anayo.
Sio jambo gumu ukiwa na NGO kuoata madaktari wa kujitolea ni jambo dogo sana.

Kwa wakazi wa Arusha na Mugumu watanielewa.
 
2,406
California ranks among the highest states in the U.S. with 2,406 active orthopedic surgeons. The state has 800 more orthopedic surgeons than Texas, which is ranked second with 1,621.
Asante
 
Katika kuhakikisha afya za Watanzania hasa wanaosumbuliwa na maradhi mbalimbali, kundi la zaidi ya madaktari bingwa 50 kutoka Jimbo la Califonia nchini Marekani, watakuwa nchini kutoa matibabu na ushauri wa kitaalamu bure.

Madaktari hao ambao wamebobea kwenye tiba za mifupa, nyonga na mishipa ya fahamu wanatarajiwa kuwaona na kuwapatia matibabu wagonjwa zaidi ya 200 wenye uhitaji bure.

Waatalamu hao wanatarajiwa kuwasili nchini Agosti 10, 2023 na watapiga kambi kwa siku saba kwenye Hospitali ya Selia inayomilikiwa na Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT).

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Arusha jana, mratibu wa ujio wa madaktari bingwa hao Lazaro Nyalandu amesema huduma hiyo ya bure itahusisha wananchi kutoka maeneo mbalimbali nchini wanaosumbuliwa na maradhi hayo.

Nyalandu, waziri wa zamani wa Maliasili na Utalii na mdau wa afya nchini amesema madaktari hao watatoa huduma hiyo ya upasuaji kwa Watanzania bure kwa siku saba.

Amesema ujio wa madaktari hao ni sehemu ya kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassan katika kuwahudumia wananchi wake.

Amesema wagonjwa ambao watapewa kipaumbele ni kutoka familia masikini na wasiojiweza kulipia gharama za matibabu ya mifupa ambayo inakadiriwa kuwa kati ya Sh50 hadi Sh60 milioni, lakini kupitia mpango huo matibabu hayo yatatolewa bure.

Chanzo Mwananchi 7th August 2023

Hapa ndio neno maendeleo hayana chama linapoonyesha maana yake.

Nakupongeza sana Mh Lazaro Nyalandu.Sina uhakika uko chama gani kwa sasa.Nakumbuka kipindi kile cha ajali ya watoto wa shule ulitoa sana msaada watoto flani kwenda kutibiwa Marekani wakapona.

Huu ndio unaitwa Uzalendo mambo ya Siasa pembeni.

Mungu akujalie watanzania tuige mazuri ya Marekani mabaya yao tusiyaige. Mfano mzuri Marekani inapotokea kugombea vyama viwili Democrat na Republican vinanyukana kwenye majukwaa uchaguzi ukiisha uchaguzi wote wanaungana kuwa kitu kimoja kujenga nchi yao yaani ukiangalia wanatumia SOP(Standard Operating Procedure) moja kwa vyama vyote kwenye maamuzi kama taifa.

Hapa mhe Unalisaidia taifa bila kujali chama cha mtu,dini status ya kimaisha zaidi ya yote unamsaidia mhe Ummy Mwalim waziri wa afya na Mama Mhe Samia Suluhu.
WAPO WAPUUZI ETI WANAJIITA WAZALENDO WA TAIFA,😁😁😁 HUKU WAKILIPAKA TAIFA UCHAFU,NA KUTUSI VIONGOZI,HONGERA MZALENDO WA UKWELI, UNAUSHAWISHI HUKO UGAIBUNI KWA UZITO WAKE.
 
Back
Top Bottom