Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Missile of the Nation

JF-Expert Member
Joined
May 24, 2018
Posts
15,101
Reaction score
56,054
Nimesikiliza mahojiano baina ya Mtia nia wa kugombea uraisi wa Chadema ndugu Nyalandu na kituo cha redio cha wasafi.
Nyalandu ameulizwa swali kuhusu Twiga waliokuwa wakitoroshwa nje ya nchi kwa kupandishwa ndege.
Katika majibu yake Nyalandu anaonyesha kujibu huku akimrefer raisi Magufuli kama "Baba yetu".

Sikutegemea kusikia mgombea uraisi mmoja akimuita mgombea uraisi mwingine, wa chama kingine, tena wanaokaribiana umri kama "Baba"

Kauli hii ukiitafsiri kiundani, unaona wazi kuwa Nyalandu kamwe hawezi kuita sepetu ni sepetu pindi kama akiteuliwa kuwa mgombea, Kiufupi imemuonyesha Nyalandu kama mtu mwenye nidhamu ya woga, laini laini sana kuweza kupambana na rafu za Magufuli kwenye kampeni.

Lakini kitu kingine ni dhahiri Nyalandu kwa kauli hii ya kumuita mshindani wake "Baba" kamwe hatoweza kumshughulikia kwa matendo yake ya kuvunja sheria na katiba na maamuzi ambayo kayafanya nje ya utaratibu wa majukumu halali ya uraisi pindi akitwaa dola. Je ni nani anayeweza kumpeleka baba yake mahakamani?

Pengine mtu unaweza kusema kuwa Nyalandu alikuwa akijaribu kuwa muungwana au kufanya siasa za kistaarabu, Jivi siasa za kistaarabu ndo umuite rais aliyeko madarakani baba yako?, Kama unamheshimu kiasi cha kumuona kama baba yako kwa nini sasa uchukue fomu kumtoa madarakani?

Hizi tabia za wanasiasa kuleta mambo ya ubaba na umama katika kazi ndiyo mwanzo na wenyewe wakishika madaraka kutaka wapewe ufather au waonekana kama mababa ambao maamuzi yao hayapaswi kupingwa. Ndiyo maana nashangaa Mtia nia wa kugombea urais wa Chadema ndugu Nyalandu anamuona raisi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi kama baba!

Hata kwenye chama cha Mapinduzi, Rais na mwenyekiti wao hawamuiti baba huwa wanamuita ndugu, Iweje leo Mgombea wa Chadema ampe heshima ya ubaba mtu ambaye hata chama chake hakijawahi kumuita hivyo?

Nyalandu kama unamuita Magufuli ni baba yetu, ya nini sasa wewe utake kumchallenge baba?

Au unaogopa Magufuli asifukue madudu yako ulipokuwa serikalini akakushughulikia?

Mtu anayepaswa kumchallenge Magufuli ni mtu shupavu, asiye na nidhamu ya woga, mtu asiye softsoft, mtu mwenye kumuona Magufuli kama rais na siyo baba yetu.

Kwa sasa sijaona mgombea mwenye ujasiri huo wa kutosha kabisa kabisa kama Tundu Lissu na Bernard Membe

Sitegemei kumsikia Lissu au Membe wakimuita Rais Magufuli kuwa ni baba yao, kufanya hivyo ni nidhamu ya woga, kujilegezalegeza mbele ya mgombea wa chama kingine.

 
Ina maana hukuona dosari kubwa katika mambo aliyoyazungumzia ila hilo tu la 'Baba"?

Na kama ilikuwa ni "Baba" ya geresha je? Hiyo hukuiwazia?

Anyway, bado sijasikiliza hayo aliyosema Nyalandu, lakini naona umefyatuka kivyako tu katika hili.

Nitajitahidi kufuatilia aliyosema Nyalandu, na kuona uzito wa hiyo "baba" iliyokuondoa wewe kwenye reli, ili nami nijiridhishe juu yake.
 
Ina maana hukuona dosari kubwa katika mambo aliyoyazungumzia ila hilo tu la 'Baba"?

Na kama ilikuwa ni "Baba" ya geresha je? Hiyo hukuiwazia?

Anyway, bado sijasikiliza hayo aliyosema Nyalandu, lakini naona umefyatuka kivyako tu katika hili.

Nitajitahidi kufuatilia aliyosema Nyalandu, na kuona uzito wa hiyo "baba" iliyokuondoa wewe kwenye reli, ili nami nijiridhishe juu yake.

You just don't get it!

The main point hapa siyo kwamba Nyalandu ameportray heshima kwa rais bali ameportray uogauoga kwa Magufuli, na uoga huzaa unafiki na unafiki. huzaa uharibifu katika nchi!

Hatuhitaji mtu muoga muoga kusimama kumchallenge Magufuli kwenye uchaguzi wa October 2020

Unaweza kuimagine Biden amuite Trump "our father Trump"?

Nakuhakikishia Lissu kamwe hawezi kusimama na kutoa heshima ya nidhamu ya uwoga kama hiyo ya kumuita Magufuli Baba!

Kauli ya Nyalandu is too timid, too lame, hypocritical. Na hizo siyo sifa zinazomfaa mtu kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania!
 
Jiwe hawezi kushindana na Nyalandu. Huyu jamaa anajua kujenga hoja tofauti na jiwe.
 
Back
Top Bottom