Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Uchaguzi 2020 Nyalandu kwa Interview hii umepoteza uhalali wa kumkabili Dkt. Magufuli kwenye uchaguzi wa Oktoba 2020

Binafsi nimesikiliza kwa makini interview hiyo leo tena ikiwa live streaming. Nathubutu kusema Nyalandu ni type ya mwanasiasa anayeweza kupeperusha bendela na akafanya maajabu.

Sijaona dosari katika interview kiukweli kaelezea vizur masuala mbalimbali ya kisera, ni mpuuz tu mwenye chuki binafsi anayeweza kukosoa hoja za Nyalandu.
 
Imagine Nyalandu akiwa mgombea kwa tiketi ya Chadema kisha kwenye kampeni majukwaani aendelee kumuita kwa jina la "Baba yetu" uone kama hajaishia kupata kura za yeye na familia yake!

Zipo kauli za kuonyesha heshima lakini haipaswi kwa mgombea kutoa kauli zinazoashiria utiifu wa kupita kiasi kwa mgombea mwingine, akifanya hivyo automatically watu wanaresonate zaidi na yule anayepewa utiifu zaidi kuliko huyu anayejaribu kumchallenge!

Words are powerful!

You just don't use submissive words when you are challenging someone
Sasa si mpaka apate hiyo nafasi,,hujaona mtu anaoa mke mpole sana,,ndoa ikifungwa tu,,makucha yanafunguliwa,,
Lazima uwe strategic,,we mwenyewe umeona lisu anasubiliwa kwa hamu,,mbowe nae ana ishu ya kusema kavunjwa mguu,
Mpaka sasa watu wa uhakika mnao msigwa na nyalandu tu
 
Nimesikiliza mahojiano baina ya Mtia nia wa kugombea uraisi wa Chadema ndugu Nyalandu na kituo cha redio cha wasafi.
Nyalandu ameulizwa swali kuhusu Twiga waliokuwa wakitoroshwa nje ya nchi kwa kupandishwa ndege.
Katika majibu yake Nyalandu anaonyesha kujibu huku akimrefer raisi Magufuli kama "Baba yetu".

Sikutegemea kusikia mgombea uraisi mmoja akimuita mgombea uraisi mwingine, wa chama kingine, tena wanaokaribiana umri kama "Baba"

Kauli hii ukiitafsiri kiundani, unaona wazi kuwa Nyalandu kamwe hawezi kuita sepetu ni sepetu pindi kama akiteuliwa kuwa mgombea, Kiufupi imemuonyesha Nyalandu kama mtu mwenye nidhamu ya woga, laini laini sana kuweza kupambana na rafu za Magufuli kwenye kampeni.

Lakini kitu kingine ni dhahiri Nyalandu kwa kauli hii ya kumuita mshindani wake "Baba" kamwe hatoweza kumshughulikia kwa matendo yake ya kuvunja sheria na katiba na maamuzi ambayo kayafanya nje ya utaratibu wa majukumu halali ya uraisi pindi akitwaa dola. Je ni nani anayeweza kumpeleka baba yake mahakamani?

Pengine mtu unaweza kusema kuwa Nyalandu alikuwa akijaribu kuwa muungwana au kufanya siasa za kistaarabu, Jivi siasa za kistaarabu ndo umuite rais aliyeko madarakani baba yako?, Kama unamheshimu kiasi cha kumuona kama baba yako kwa nini sasa uchukue fomu kumtoa madarakani?

Hizi tabia za wanasiasa kuleta mambo ya ubaba na umama katika kazi ndiyo mwanzo na wenyewe wakishika madaraka kutaka wapewe ufather au waonekana kama mababa ambao maamuzi yao hayapaswi kupingwa. Ndiyo maana nashangaa Mtia nia wa kugombea urais wa Chadema ndugu Nyalandu anamuona raisi Magufuli ambaye ni mwenyekiti wa Chama cha mapinduzi kama baba!

Hata kwenye chama cha Mapinduzi, Rais na mwenyekiti wao hawamuiti baba huwa wanamuita ndugu, Iweje leo Mgombea wa Chadema ampe heshima ya ubaba mtu ambaye hata chama chake hakijawahi kumuita hivyo?

Nyalandu kama unamuita Magufuli ni baba yetu, ya nini sasa wewe utake kumchallenge baba?

Au unaogopa Magufuli asifukue madudu yako ulipokuwa serikalini akakushughulikia?

Mtu anayepaswa kumchallenge Magufuli ni mtu shupavu, asiye na nidhamu ya woga, mtu asiye softsoft, mtu mwenye kumuona Magufuli kama rais na siyo baba yetu.

Kwa sasa sijaona mgombea mwenye ujasiri huo wa kutosha kabisa kabisa kama Tundu Lissu na Bernard Membe

Sitegemei kumsikia Lissu au Membe wakimuita Rais Magufuli kuwa ni baba yao, kufanya hivyo ni nidhamu ya woga, kujilegezalegeza mbele ya mgombea wa chama kingine.

Nmekuelewa sana mkuu, sijaangalia bt kama kasema hivyo kapoteza sifa ya kugombea ukiacha hivyo CHADEMA hawawezi kurudia kosa kwa kumuweka tena mgombea toka CCM, wakimuweka tu NYALANDU au MEMBE sijui..sitofuatilia tena siasa za upinzani na ntakata kadi ya CCM na kuilipia mwaka mzima
 
Hii interview ambayo Nyalandu anamuita JPM ilinifanya nione huyu mheshimiwa kapwaya sana kupeperusha bendera ya upinzani
 
Back
Top Bottom