Nyama Special Thread: Jifunze kupika mapishi mbalimbali ya aina tofauti za nyama

Nyama Special Thread: Jifunze kupika mapishi mbalimbali ya aina tofauti za nyama

Jinsi ya kupika kuku wa kupaka

poussin-chicken.jpg


Mahitaji


  • Kuku mmoja

  • 1 Kitunguu saum
  • 1 Tangawizi

  • 2 Pilipili hoho

  • 2 pilipili mbuzi
  • 2 Ndimu mbili au limao
  • 
Manjano nusu ki
jiko
  • Tui la nazi

  • 2 Vitunguu maji 

  • Chumvi vijiko viwili
  • 4 Nyanya
  • 1 Karoti

Jinsi ya kupika

  1. Katakata kuku katika vipade vya wastani kulinganana kisha msafishe katika maji safi hadi uchafu wote uishe na umweke pembeni.
  2. Chukua vitunguu saum, tangawizi, ndimu au limao, chumvi kiasi, pilipili na mafuta kijiko kimoja na uvichanganye pamoja na vipande vya kuku ulivyokwisha kata kisha acha kwa muda wa nusu saa ili viungo vichanganyike na kukolea vizuri katika nyama.
  3. Bandika sufuria yenye mafuta jikoni, kisha kaanga vitunguu maji mpaka vibadilike rangi, tia pilipili hoho, karoti na nyanya kisha endelea kukaanga mpaka viive kabisa.
  4. Baada ya kuhakikisha nyanya zimeiva, mimina tui bubu la nazi na uache lichemke hadi liive hadi mchuzi uwe mzito.
  5. Banika vipande vya kuku ulivyovikata kwa muda wa robo saa, huku ukivigeuzageuza ili viive kwa joto.
  6. Baada ya hapo vitakuwa tayari na weka kwenye sufuria, kisha miminia ule mchuzi mzito na ufunike halafu weka mkaa juu kama wali.
  7. Acha nyama ikauke vizuri kwa muda wa dakika kumi, hapo mlo wako utakuwa tayari.
 
Jinsi ya kuchoma nyama ya ng'ombe, mbuzi, kuku au kitimoto

kuku+choma.jpg


Mahitaji


  • Nyama ya ngombe kilo 1 (au kuku mzima)
  • Tangawizi 1
  • Soya sauce
  • Nyanya ya kopo
  • Kitunguu swaumu 1
  • Karoti 2
  • Ndimu au limao 1
  • Chumvi

Jinsi ya kupika

  1. Menya vitunguu swaumu, vitunguu maji na uvikate kate pamoja na tangawizi na karoti.
  2. Weka kila kitu kwenye blender. Saga kwa pamoja ili kupata uji mzito.
  3. Weka nyanya ya kopo na soya sauce kwenye mchanganyiko wako.
  4. Chukua nyama ya (Kuku, ng'ombe, mbuzi au kitimoto) kisha weka chumvi.
  5. Kamulia ndimu au limao la kutosha kwenye nyama na kisha changanya kiasi.
  6. Changanya nyama yako na mchanganyiko wa kwenye blender.
  7. Weka nyama kwenye jokofu kwa muda wa saa moja au mawili. Unaweza pika kuandaa usiku na kuiacha kwenye jokofu ilale hadi asubuhi.
  8. Andaa mkaa wako kwenye jiko la kuchomea, moto ukikolea vizuri, weka nyavu za kuchomea na tandaza nyama yako kwenye nyavu.
  9. Igeuze mara kwa mara ili iive vizuri pande zote.
  10. Ikishaiva vizuri iepue na tayari kwa kuliwa.
 
samaki wa foil namchomaje katika jiko la mkaa?
 
samaki wa foil namchomaje katika jiko la mkaa?

Unachoma kama hivi:

220.jpg


Tofauti hapo itakuwa ni kwenye nyama unayoichoma. Wewe utakuwa unachoma samaki ambaye yumo ndani ys foil na sio iliyo uchi uchi kama hiyo inayoonekana kwenye picha.
 
darasa zuri.
hivi kweli prawns ni haramu?
sawa na alivyo nguruwe?
mtume Muhammad s.a.w alipoulizwa hukusu maji ya bahari kama yafaa kuchukulia udhu alisema " maji ya bahari ni twahara na viumbe vyake (vilivyofia ndani ya maji) pia ni twahara(halal kwa kuliwa)"
so viumbe vyote vya baharini (samaki aina zote) ni halal. unless ukiwala wanakudhuru au wana madhara yaliyo wazi ie. samaki ajulikanaye kuwa ana sumu
 
Unachoma kama hivi:

220.jpg


Tofauti hapo itakuwa ni kwenye nyama unayoichoma. Wewe utakuwa unachoma samaki ambaye yumo ndani ys foil na sio iliyo uchi uchi kama hiyo inayoonekana kwenye picha.

Shukrani sana
 
Back
Top Bottom