Nyama ya kenge

Nyama ya kenge

ndege JOHN

JF-Expert Member
Joined
Aug 5, 2015
Posts
21,643
Reaction score
51,642
Kijiji Cha mtakilachawa masasi njia ya newala wamenishangaza Sana asee yaani huku wanyama wa ajabuajabu huwaoni kuanzia paka, mbwa wanaliwa vibaya mno juzi watu wamemlamba kenge.

Sasa huu uchu unasababishwa na nini ni njaa tu au yaani watu kufikia Kula punda ama nyani ama panya
 
Kijiji Cha mtakilachawa masasi njia ya newala wamenishangaza Sana asee yaani huku wanyama wa ajabuajabu huwaoni kuanzia paka,mbwa wanaliwa vibaya mno juzi watu wamemlamba kenge Sasa huu uchu unasababishwa na nini ni njaa tu au yaani watu kufikia Kula punda ama nyani ama panya
Si njaa. Its our lovely culture.
 
Kijiji Cha mtakilachawa masasi njia ya newala wamenishangaza Sana asee yaani huku wanyama wa ajabuajabu huwaoni kuanzia paka,mbwa wanaliwa vibaya mno juzi watu wamemlamba kenge Sasa huu uchu unasababishwa na nini ni njaa tu au yaani watu kufikia Kula punda ama nyani ama panya
Yaweza kuwa huko wamewahi kuishi na watchina pamoja na wakorea
 
Mkuu ndege JOHN hakuna mnyama ambaye haliwi. Suala ni mnyama yupi analiwa na nani. Ukifika Nigeria au kwa wanaopakana na mbuga/misitu ndiyo utathibitisha ninachokwambia.

Kenge hata uzaramoni analiwa vizuri tu. Anajulikana kama mburu. Huko Mtwara wanaliwa panyapori, vyura wakubwa wanjano na kadhalika. Mbwa huliwa kimila uheheni, ubenani na uluguruni.

Sisi wangoni tunakula panyapori tunaowaita mbewa na wadudu wa aina mbalimbali. Upareni wanakula kobe na mayai yake; kilombero huko na kwawahadzabe wanaliwa ngedere na nyani na kadhalika na kadhalika.
 
Japo labda mapishi huenda yakawa tofauti, kuna wenzetu wanawala kenge vizuli tu.
Miaka ya 2010, tukawatembelea wafilipino huko Mwanza,sasa wao hupika na kubeba sufuria lao mpaka mezani,hakuna cha hotpots. Nyama ukiangalia,haieleweki. Ukiuliza, unaambiwa ula au acha. Tukaona isiwetabu, baada ya kula,kila mmoja anaosha sahani yake jikoni. Dah! Mkia,kichwa na miguu vimeshikana na ngozi viko hapo.
Unawaza kufa,kuugua tumbo au majanga mengine. Masaa,siku,wiki kumbe hakuna kisicholiwa.

Kosa labda kujua unachokula
 
Kijiji Cha mtakilachawa masasi njia ya newala wamenishangaza Sana asee yaani huku wanyama wa ajabuajabu huwaoni kuanzia paka,mbwa wanaliwa vibaya mno juzi watu wamemlamba kenge Sasa huu uchu unasababishwa na nini ni njaa tu au yaani watu kufikia Kula punda ama nyani ama panya
Punda hana noma.
 
Back
Top Bottom