Nyama ya Kitimoto Imedoda Kipindi Hiki cha Mfungo

Kajeba

JF-Expert Member
Joined
Oct 15, 2020
Posts
1,057
Reaction score
2,364
Ni wazi kwamba kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani biashara ya kitimoto imedorora. Jana na leo bucha nyingi hazina wateja kabisa, nyama zimenin'g'inia tu bila mnunuzi. Hali hii inatufanya sisi wenye mabucha ya kitimoto kuumia sana, maana hakuna mzunguko wa pesa.

Bucha yangu ipo hoi! Kawaida, mida hii ningekuwa na pilikapilika nyingi kuhudumia wateja, lakini sasa niko tu nimekaa nikitazama nyama ikipoteza ule mvuto wake.

Hivi karibuni nitafikiria mbadala wa biashara, labda nichinje mbuzi au kuku ili angalau nipate kipato kidogo. Lakini ukweli ni kwamba, kwa sisi wafanyabiashara wa kitimoto, Ramadhani ni kipindi cha uvumilivu na maombi.
 
🙇🙇🙇 kwaiyo ulitaka kumaanisha nn?
 
Ngoja waje WATUHUMIWA wakujibu waisijekufungulia tu ukasomewa surrath ksrbioo
 
Na supu mkuu inalipa sana HATA ukiweka makongoro ya ngroo kujulikana NGUMU ukijaza viungoo
 
Sio kweli..
 
Wateja wako swaumu 😁
 
Hii story inajirudia Kila mwaka kwa lengo lile lile!
Hakuna aliyekulazimisha kula kitimoto kula na oga mafuta yake hakuna shida!

Ila kulazimisha Kila mtu awe na mawazo madogo madogo kama yako ni dalili ya ushoga live!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…