Nyama ya Kitimoto Imedoda Kipindi Hiki cha Mfungo

Nyama ya Kitimoto Imedoda Kipindi Hiki cha Mfungo

Kitimoto ingekuwa inaliwa kama ng'ombe; huyo mnyama angekuwa ametoweka.
 
Ni wazi kwamba kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani biashara ya kitimoto imedorora. Jana na leo bucha nyingi hazina wateja kabisa, nyama zimenin'g'inia tu bila mnunuzi. Hali hii inatufanya sisi wenye mabucha ya kitimoto kuumia sana, maana hakuna mzunguko wa pesa.

Bucha yangu ipo hoi! Kawaida, mida hii ningekuwa na pilikapilika nyingi kuhudumia wateja, lakini sasa niko tu nimekaa nikitazama nyama ikipoteza ule mvuto wake.

Hivi karibuni nitafikiria mbadala wa biashara, labda nichinje mbuzi au kuku ili angalau nipate kipato kidogo. Lakini ukweli ni kwamba, kwa sisi wafanyabiashara wa kitimoto, Ramadhani ni kipindi cha uvumilivu na maombi.
Kwa hiyo bwashee una maana hao wakristo waliofunga ndiyo wateja wakubwa wa kitimoto?
 
Mhm .. Sijafanya utafiti inaweza ikawa kweli ama la
Ina ukweli sio wakati mzuri wa biashara ya mdudu kwa sasa.

Wengine wanaamini Waislamu ndio walaji wakubwa. Ni kweli wapo wanaokula ila ni wachache na kwa kificho. Tena wale ambao imani haijakita mizizi ambao kiuhalisia hatuwezi sema ni Waislamu.

Lakini huenda sababu kubwa inayofanya biashara hii isetembee ni mazingira. Mikoa ya pwani ambako Uislamu umekita mizizi ni ngumu biashara hii kwenda kwa kuwa watu wengi ambao ni wakristo wala mdudu wanaheshimu imani ya wengine na hawataki kuwakwaza ndugu, jamaa na marafiki kwa kula kitimoto. Hivyo mwezi huu wakristo wengi wala kitimoto husimama pia kutumia mdudu.

Lakini ukienda nyumbani kwetu Mwakaleli mdudu wa kwenye makalai anapigwa kwa kwenda mbele kwa kuwa mazingira yale hayana Waislamu kabisa.
 
Campany yangu wote wamefunga sa niende mwenyewe kweli
 
Unataka kusema wa upande wa pili ndio wateja wakubwa w mdudu😅
 
Back
Top Bottom