GoldDhahabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2023
- 7,189
- 10,375
Kwenye Biblia, kuna habari ya Mhubiri aitwaye Yona kumezwa na "samaki" mkubwa na kisha kutapikwa siku ya tatu. Sijui kama kuna tukio jingine kama hilo Iilishatokea karne hii!
Mwaka 2021, raia wa Marekani, Michael Packard, alinusurika kuwa kitoweo cha nyangumi baada ya kujikuta ndani ya kinywa chake kwa sekunde zisizopungua thelathini. Mwanzoni alifikiri ni papa, lakini baada ya kutokuhisi meno ya papa, akajua kuwa ni nyangumi. Alifichwa kinywani mwa nyangumi kwa kutangulizwa kichwa, kwa hiyo hakuwa akiona chochote zaidi ya giza totoro. Aliingia kinywani mwa nyangumi na vifaa vyake vya kupigia mbuzi, ila inawezekana kiwiliwili kilibaki nje ya kinywa cha nyangumi.
Nyangumi aliyembugia alikuwa "mstaarabu". Hakulazimisha kummeza wala kumbinya kwa kinywa chake, badala yake, "alijongea" mpaka juu ya maji na kumtema hewani juu ya maji na kisha kuendelea na "mishe" zake.
Kwa mujibu wa wataalamu, nyangumi anao uwezo wa kumwua mwanadamu akiamua kufanya hivyo, ingawa hana asili ya uchokozi.
Uwezo wa kuu anao, ila sina uhakika kama anaweza kummeza mtu aliye hai. Inasemekana umio wake hauna uwezo wa kumeza kitu kikubwa kama mwili wa binadamu.
Ukweli ni upi? Nyangumi wa siku hizi wangali na uwezo wa kummeza mtu aliye hai kama ilivyokuwa wa kipindi cha Yona?
Mnusura ni huyo hapo chini.