Nyani Ngabu
Platinum Member
- May 15, 2006
- 94,296
- 122,540
Nyani Ngabu
Kabla ya kufika USA ulikuwa unavuta picha gani kichwani ambayo ulipofika ulikuta ni tofauti kabisa?
Uzuri wangu ni kwamba tokea nikiwa mdogo kabisa nilipata fursa ya kutembelea nchi mbalimbali za Ulaya.
Pia, nikiwa mdogo niliwahi kuishi Uingereza kwa miaka kadhaa.
Mshua wangu alisomea Marekani...shahada zake zote. Nyumbani tulikuwa tunaletewa majarida kibao ya Kimarekani kama vile Reader's Digest na Time Magazine, almanac ya CIA World Fact Book, World Book Encyclopedia, na kadhalika.
Kwa hiyo, ukijumlisha mimi kusafiri nikiwa mdogo, kuishi Uingereza, na kusikiliza stori za mshua kuhusu Marekani, kusoma hayo majarida na hivyo vitabu,picha ya Marekani niliyokuwa nayo kabla sijaenda ndo hiyo hiyo niliyoiona nilipofika. to Hakukuwa na surprise yoyote kabisa.
Halafu majirani zetu tulipokuwa tunaishi walikuwa Wamarekani. Kwa hiyo sikupata culture shock yoyote ile.
So I took to the USA like a duck to water🙂.
Na katika maisha yako ya ugeni ni kitu gani kilikuwa kinakusumbua mwanzoni?
Mwanzoni kusema ukweli nilikuwa homesick sana.
Kumbukua, nilienda USA nikiwa mdogo kwa kweli.
Kwa hiyo huo udogo, umbali, na ukizingatia kwamba mimi sina kaka wala dada, kuna nyakati nilikuwa najikuta napakumbuka sana nyumbani.
Sawa, baba na mama nilikuwa nao na ningeweza kuchukua tu simu na kuwapigia ili kuongea nao, lakini bado mazungumzo ya mtoto na wazazi wake ni tofauti na mazungumzo ambayo mtu unaweza kufanya na kaka au dada zako au hata marafiki zako.
Hivyo homesickness ndo ilinisumbua sana hapo mwanzoni mwanzoni.