Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Nyani Ngabu Mjengoni! Interview: Mapenzi, Utajiri&Mali, Marafiki na Maisha ya ugenini.

Nyama ya Bata mzinga imeisha?

Limebaki paja moja na kipapatio!

Ila glazed ham bado ipo bwerere na cornbread stuffing ya kumwaga.

Kama hutumii shampeni basi kuna gallons mbili za apple cider.

Karibu tumwangalie Dak Prescott na Dallas Cowboys wakichuana na LA Chargers..
 
Shukrani mkuu! Hilo li turkey leg limoja ni dinner tosha kabisa. Hawa Dallas acha tu wafungwe leo na Chargers. Huyo Jerry Jones mambo yake hayaeleweki siku hizi! Inabidi tu hao wamiliki wa timu zingine kwenye NFL wamuondoe tu kwenye hiyo club!
 
Dah nimesoma mahojiano yote!

Heshima yako Nyani Ngabu. Nimejifunza mengi kupitia majibu yako!

Nilikuwa nakuona uko arrogant sana na mkorofi lakini baada ya muda nikagundua siyo hivyo, nikaona hupendi kupindisha mambo. Mtu akiharibu unampa ukweli wake pasipo unafiki...I like that! Tangu nimejua hilo, napenda kusoma comments zako hata kama ni za maoni tofauti na mawazo/imani yangu!

Safi sana Ngosha!
Uko kama mimi, kati ya watu mwanzoni nilikuwa siwaelewi humu jf basi ni huyu Nyani Ngabu, kuna uzi mmoja ulinifanya nimuelewe vyema kabisa. Na kubadilisha vile nilikuwa namchukulia awali.
 
Hahhaaa! Hapo utakuwa umemaliza kabisa.

352860C0-2D0C-4A96-B52B-C5C4AE029805.jpeg
 
Kwangu bora ni kuwa na marafiki wachache lakini wenye ubora.

Kuwa na marafiki wengi ni kukaribisha kila aina ya matatizo tu kwenye maisha yako.

Hivyo binafsi napendelea kuwa na marafiki wachache walio ma ubora.

Wengine waliobaki ni washikaji [acquaintances].



Hapana kwa kweli.

Hakuna rafiki hata mmoja ambaye amewahi kuwa msaada kwangu kwenye msala wowote ule.

Hiyo ni kwa sababu mimi ni mtu mwenye kupenda kujitegemea mwenyewe.

Pia nina uwezo mkubwa sana wa kuvumilia hali ngumu.

Uwezo huu ndo hunifanya nisitegemee misaada ya aina yoyote ile toka kwa watu.
Hii point imenifanya nisipatwe na vidonda vya tumbo na kujiamini zaidi
 
Huyu jamaa na mfaham vzr sanaaa ila yy hanijui, kuna siku tulikua kwenye bas nikaona ana log in JF ni mzee wa makamu muhun muhun tuu yaani wale wazee vijana ana mambo ya kisela sanaaa
Aisee
 
Back
Top Bottom