Nyaraka mpya za Kagoda zawalipua Rostam, Manji

WAPE MASIKINI POMBE WALEWE WAZISAHAU SHIDA ZAO!!?? lakini usiwape waflume na watawala wahaharibu nchi!!??..hivi nchi ya TANZANIA inatawaliwa kwa staili ya KUOMBA MUNGU ILI KUTATUO MATATIZO yanayo sababiswa na watu wasilo litakia taifa hili mema AU KUNA SHERIA ZILIZO TUNGWA NA WATANZANIA wenyewe ili kulinda taifa lao na rasilimali zao!!??.NA KWANINI HAWA WATANZANIA wenye kununua utanzania wenye asili ya kieshia kila ufisadi wamo.???..Usually
when people are sad they don't do anything they just CRY over their
condition but when they gel Angry they bring about a change" (MALCOLM X)
 
Tatizo liko wapi hapo?

Kama DPP aliwataka Watanzania wapeleke ushahidi, na huyu bwana Msemakweli kapeleka "ushahidi" kwa mtazamo wake na aujuavyo yeye, tatizo nini?

Mpaka sasa sijaona "any incriminatory evidence" kwa RA wala kwa YM.

Swali: Kilichomfamya Msemakweli asifunguwe yeye mwenyewe kesi mahakamani ni nini?

Jibu: Anajuwa wazi kuwa hana "any incriminatory evidence" kuhusu RA wala Manji ndio maana akaamuwa kuupeleka "ushahidi" kwa DPP halafu kuu"leak" humu JF na kwingine ili ajipatie umaarufu kuonekana kuwa kafanya kazi kweli kweli.

Ukweli ni kwamba. huo anaosema "ushahidi" haupo wala hautoshelezi kumshitaki mtu. Na hiyo list aliyoitowa hiyo ilikuwa ni report ya audititors kuhusu madeni ya EPA.

Nawashangaa sana watu wanaoona hapo kuna ushahidi. Jamani, ule u "great thinker" uko wapi?
 
Safi sana Invisible Kutujuza na big up msema kweli kwa kua msema kweli,ngoja tusubirie hii ya shimbo kutoka kwa msema kweli.
 
Pole Kama ujaona,nakushauri pitia tena utauona tu...thanx

 
Feleshi ana uamuzi wa kufanya lakini asipofanya au kutaka kufanya atasaidiwa; si tayari tumeshasaidia taasisi nyingine kufanya kazi zao tena bure? Kilichodokezwa hapa ni kidogo sana kulinganisha na kilichopo. Sasa hivi tunaanza kuhesabia muda wa Feleshi kukataa kufungua mashtaka ili asaidiwe.
 

FF sipingi hoja yako kuu lakini Msemakweli atafungua kesi gani mahakamani na dhidi ya nani? Sidhani kama hapa kuna kesi ya madai. Hizi shutuma kama ni za kweli matokeo yake ni kufungua kesi ya jinai. Kesi za jinai huwa zinafunguliwa na kuendeshwa na Jamhuri. Sio watu binafsi kama akina Msemakweli.
 
Naomba Msemakweli apewe Ulinzi wasije wakamkolimba
 
Huyu Sanze naye mwanasheria gani anasign vitu bila utaratibu? Wanataaluma wa Tanzania wako hoi kwelikweli; si wahasibu, wanasheria, wahandisi, n.k Kama hii ndiyo aina ya wanataaluma tulionao hakika itaichukua Tanzania miaka lukuki kufika tunakoenda.

Mkuu hasa hawa wanasheria. Achana na Sanze ni mtu mdogo tu huyo, umeona pale kwenye ile document mojawapo imesainiwa na Dr. Ringo Tenga mmiliki wa Law Associates. Huyu ni msomi aliyebobea katika sheria na mtu maarufu sana na ndo alikuwa wakili wa Richmond pia. Jamaa ni tajiri wa kupindukia na pesa zake zinaishia kwa akina dada tu. Wako wadada kadhaa anawasomesha nje ya nchi na wengine huwakaribisha kwenda kunywa soda nje ya nchi atakako yeye (mdada).
 
Pole Kama ujaona,nakushauri pitia tena utauona tu...thanx

Nimepitia mara tatu kabla sijayaandika hayo. Kama wewe unauona ushahidi wa kumshitaki mtu bila kuwa na mashaka (without any doubt) tafadhali nioneshe.
 
hivi kuna thread yoyote ulishawahi kui-support? ukijitambua, utaweza kujua masuala mengine yanayokuzunguka.
 
Ushahidi mpya hapa ni bank statement ya Manji jinsi fedha zilivyohamishwa Kati ya Dec 2005 na Machi 2006 baada ya uchaguzi so hapo uongo wa kutumia kinga ya CCM haupo.

Pili ametoa CRDB Holand record kuonyesha Manji kadhamini waliofungua Kagoda so kama Kagoda imeiba Manji ndiye mwizi ama anawajua wezi na aliwadhamini ama awalete ama aende jela.

Tatu kulipa fedha amelipa kama Jeetu Patel na Maranda saa kwann Maranda afungwe na Farijala wake yeye na Rostam wapete?

Nne Msemakweli katuambia Rostam na ukoo wake na wafanyakazi wake Barat Goda na Tabu wamelipa sehemu ya fedha za Kagoda kupotia Exim bank wakitumia kampuni ya Afritainer ambayo ushahidi unaonyesha ni kampuni pacha na Kagoda...

And more more just read the doc carefully
 
Duh! Ndani ya magamba no one is right? Hivi Manji naye GAMBA?
 

Mbona watu wengi tu huenda kufunguwa kesi za jinai polisi? kama hana ushahidi wa kutosha hata huy dpp atamshitaki nani? wewe umeona kuna ushahidi hapo wa kumshitaki mtu ukashinda?

Besides, nakubaliana na wewe kuwa kesi za EPA si za jinai kama wengi wanavyotaka ziwe. EPA ni madeni na kesi zake ni za madai na si za jinai. Ukilielewa hilo hapo ndio utajuwa kuwa Kikwete alipowataka waliochukuwa hizo pesa wazirudishe wenyewe, alifanya jambo la maana sana. Kwani ni wazi kabisa hizo ni kesi za madai na ukizifanyia papara kuzipeleka mahakamani unaweza kujikuta kuwa kesi inakuwa dragged kwa muda mrefu sana kiasi kuwa inakutia hasara zaidi na mwisho wake fedha usizipate na kesi ukashindwa.

Haya ya Kumtafuta RA na YM ni majungu tu, hakuna kesi hapo ni wajanja wachache wanajitafutia umaarufu. Na wajinga wengi wanaamini hapo kuna kesi. Nashangaa sana.
 


Mkuu naona hukunielewa. Faiza ameuliza kilichomfamya Msemakweli asifungue yeye mwenyewe kesi mahakamani ni nini? Mimi nikamjibu Msemakweli hawezi kufungua kesi kwa sababu kama ikifynguliwa kesi itakuwa kesi ya jinai. Mwenye mamlaka ya kufungua na kuendesha kesi za jinai ni Jamhuri kupitia ofisi ya DPP. Sijaongelea masuala ya ushahidi.
 
hivi kuna thread yoyote ulishawahi kui-support? ukijitambua, utaweza kujua masuala mengine yanayokuzunguka.

Nyingi sana nimezi-support, zile zenye mantiki na si majungu ya waziwazi.
 
Huo wote ni ushahidi "circumstantial" na sio "solid" na ndio maana si Msemakweli wala Msemauongo wanaoweza kushitaki wao wenyewe na wanaupeleka kwa DPP, kwani wanajuwa kwa ushahidi kama huo, wakishindwa kesi! wanafilisiwa. Kwani hao watu unao "wapeleka" mahakamani dau lao ni kubwa.
 
Kuna mtu makini sana tena mwandishi anayeheshimika kaandika katka Bidii kwamba;

Naomba kusahihisha data humu;

Benjamin Mwang'onda wa Khatco iliyogonga mhuri wa Kagoda si mtoto wa Apson na fedha zilitoka benki kati ya Dec 25, 2005 na Machi 2006 sasa hapo uchaguzi wa wapi? Na zilienda nje ya nchi kutoka akaunti ya Yusuf Manji. Someni kwa makini na mtajua kazi ipo na Watanzania walioko Exim Bank, BoT,CRDB, Polisi, Usalama, DPP's office etc wameshatoa ushirikiano mkubwa na wataanza kumwaga data soon, kaeni mkao wa kula
 
Naona mkananganyiko unaendelea!
Mwaka huu kila mtu atasema lake!
 

Faiza kesi huwa hazifunguliwi polisi. Kesi zinafunguliwa mahakamani. Unapoenda polisi unaenda kuripoti au kulalamikia tukio ili polisi wafanye uchunguzi na kuchukua hatua zaidi. Wakishamaliza uchunguzi wao na kuona kuna ushahidi wa kumfungulia mtuhumiwa kesi mahakamani then wanapeleka faili kwa DPP ili afanye hivyo. Ukienda polisi kuripoti issue za madai sijui kama watakusaidia.

Umesema kuwa EPA ni madeni na kesi zake ni za madai na si za jinai. Sasa vipi mtu akigundulika kuwa alitumia jina au kampuni bandia kupata hela za EPA, utamfungulia kesi ya mada au ya jinai? Hata kama ingelikuwa tuhuma na kesi za EPA ni za madai, Msemakweli ataenda kushtaki kama nani? Anamdai nani?

Kuhusu swali lako kama naona kuna ushahidi wa kumshitaki mtu na kushinda, mie bado sijafika huko. Besides tumeambiwa kuna ushahidi zaidi ya uliowekwa hapa, so ni vigumu kutoa a definitive answer.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…