Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Mhh mkuu mwananchi yeye anataka barabara, hajalishi ni uchaguzi au hapana.
Sisi wananchi tunataka haki ya kuwa na barabara na sio sheria ya kuwa na barabara wakati usio wa uchaguzi.Afterall yanini kutumia hesabu mbovu wakati fika yule Magu ataendelea,tunamdanya nani.
 
Haya ndio madhara ya katiba yetu yaani huyo ni mgombea wa kiti cha urais wakati huo huo ni rais wa jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
 
Tume wako wapi?? Walikataza pilau kuku la Rungwe;kuna mtu amekuja na barabara.....
 
Watumishi kura kwa Lissu.Sio mbaka katiba
 
Huyu jamaa swala la aibu kwenye kutokufata sheria. Ninawaza sana wakurugezi watakaotangaza kura kuwa ameshindwa kwenye majimbo yao.
 

Huyu ni mgombea anaomba kura? Au rais kazini akitoa maagizo ya kiserikali? Au ni rushwa kwa wapiga kura?

Usawa kwa wagombea uko wapi?

Tume endeleeni kufumbia haya kuwa haya wahusu.
 
Yaani kwenye nchi ya demokrasia ya kweli, alipomaliza tu mazungumzo haya tume ya uchaguzi ingetangaza kumwengua huyu mgombea. Kama kutumia tu gari la serikali kwenye shughuli ya siasa ni marufuku sembuse kutumia haya madaraka. Eti, mimi ni Rais. Sasa kama ni Rais anapiga kampeni za nini?
 
Huyu jamaa swala la aibu kwenye kutokufata sheria. Ninawaza sana wakurugezi watakaotangaza kura kuwa ameshindwa kwenye majimbo yao.
"Nikununulie gari, nikulipe mshahara, nikupe nyumba halafu eti unamtangaza mpinzani kashinda! Hiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii" (Magu, 2019)
 
Huyu jamaa anavyopenda madaraka sidhani kama Atatoka madarakani kwa Njia ya kupiga kura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…