Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Uchaguzi 2020 Nyehunge: Dkt. Magufuli amuamrisha Mfugale atangaze ujenzi barabara ya Sengerema-Nyehunge (KM 46) kisha amuulize hela za kujengea

Hapa unajaribu kusemaje?Kuwa huwa mnashindwa uchaguzi ila mabavu yanawabakiza madarakani?
Tambua kuwa haki huinua taifa na kustawisha amani na utulivu!Unaweza usiwe mkomavu wa kutosha kuelewa haya,ila ikifika wakati wananchi wakadai haki yao kwa namna nyingine,ndio hapo majuta huwa mjukuu!Mifano ipo mingi na hai!Wale wanaodhulumiwa haki yao wakichoka huwa ni suala la muda tu,na ndio hapo hata maadui inakuwa rahisi kupenyeza mambo yao!Mtu akifikia breaking point,ukampa silaha unategemea nini?Uasi hujengwa taratibu,pigieni chapuo uovu ila tambueni kuwa wanaodhulumiwa nao wana kipimo cha uvumilivu!
Kama umenielewa vizuri nimekwambia acheni kelele za kila msimu wa uchaguzi dai katiba ya Jaji Warioba kwanza.
Vinginevyo rudisha chama kimmoja mpambane ndani kwa ndani kama zamani.
 
Kwani fedha ni zake, na ufalme ni wake, maguvu, na sasa utukufu pia ni wake milele na milele. Aaaamino!
 
Kama umenielewa vizuri nimekwambia acheni kelele za kila msimu wa uchaguzi dai katiba ya Jaji Warioba kwanza.
Vinginevyo rudisha chama kimmoja mpambane ndani kwa ndani kama zamani.
Unataka wadai hiyo katiba kwa nani?Huyu huyu Jiwe?Uko serious kweli?Tuna Rais mshamba kwahiyo hayo unayosema labda atoke madarakani!Au labda njia nyingine ni violence!
 
Am confused, rais ni rais au ni mgombea wa urais kupitia Chama cha Mapinduzi? Maana kampeni ikianza tume ndio inakuwa inaongoza nchi.
Mwenye kuelewa anieleweshe tafadhali
 
Unataka wadai hiyo katiba kwa nani?Huyu huyu Jiwe?Uko serious kweli?Tuna Rais mshamba kwahiyo hayo unayosema labda atoke madarakani!Au labda njia nyingine ni violence!
Kwa hiyo wewe umejikalia tu ukisubiri kula bila kunawa?
Au unataka vurugu bila kujua madhara yake.
 
Kwa hiyo wewe umejikalia tu ukisubiri kula bila kunawa?
Au unataka vurugu bila kujua madhara yake.
Ndio nakwambia kikichobaki ni hicho!Iwapo matokeo halali hayatatangazwa basi safari hii hatumuachii Mungu!Tutadai haki kwa namna yoyote,siwezi kupanga foleni masaa 6 halafu iwe ni geresha tu watu wanayo matokeo yao ya mfukoni!
 
Ahaaa wewe una chekesha sana acha akiba ya maneno,hao unaowapangia foleni utawakuta wameunga juhudi za Magufuli. Tumewaona akina Lowassa, tumewaona akina Lijualikali na hata yule Katambi.
Dai katiba ya Warioba ndio nguzo kuu ya mabadiliko ya kweli na haki.
 
Kura yangu ina thamani sana!So nataka iheshimiwe!!Isipoheshimiwa basi tutawakumbusha watawala kuiheshimu kwa namna ngingine!
 
Siyo rushwa kila wakati Magufuli akiona jambo haliko sawa hana subira,ni mtu wa vitendo bila kuchelewa.

Lakini pammoja na mihemuko ya uchaguzi wa uraisi,Magu the bulldozer hana mshindani bora arudi kwenye majukumu yake hadi 2025.
hivi unajua sheria na kanuni za uchaguzi kweli?
 
Hiyo ni rushwa alitakiwa awe ameijenga siku nyingi, hata kutoa ajira 13000 na kutoa bima ya afya wakati wa kampeni ni rushwa pia.

jamaa anawafunga kamba sana watanzania wasio na elimu,leo amesema ametoa ajira 6million ,akatoa mfano wa daraja analojenga pale kamanga, yani anajua kabisa wale wananchi hawana akili ya kujua zile ni ajira za muda project ikiisha watu wanabaki hawana ajira !!
 
Kura yangu ina thamani sana!So nataka iheshimiwe!!Isipoheshimiwa basi tutawakumbusha watawala kuiheshimu kwa namna ngingine!
Una uhakika gani wakati kura huzihesabu,kazi yako ni kupiga kura na kuondoka?
 
Kinyago walichokichonga,, leo kinawatisha wenyewe
 
DKT. Magufuli akiwa anaendelea na kampeni za uchaguzi 2020, amepita kijiji cha Nyehunge akiwa anaelekea Geita ambapo kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46. Alisimama kuongea na wananchi waliokuwa wakimsubiri barabarani, wakati anaielezea barabara hiyo ghafla aliomba simu yake na kumpigia mtu ambae baadae alijulikana ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS, Injinia Mfugale na mazungumzo yao yalikuwa hivi.

Magufuli: Hallo, Chief executive

Mfugale: Naam mheshimiwa Rais

Magufuli: Hujambo

Mfugale: Sijambo mheshimiwa

Magufuli: Uko wapi?

Mfugale: Niko Dar es Salaam TANESCO tunazungumzia habari ya Nyerere dam.

Magufuli: Haya, sasa mimi niko Nyehunge, kutoka Sengerema mpaka Nyehunge ni kilomita 46, hii barabara tumeshaifanyizia feasibility study na detail design, nimesimama hapa na wananchi, nataka hii barabara, mimi si ndio Rais?

Mfugale: Ndio mheshimiwa(Wananchi kicheko cha furaha)

Magufuli: Nyehunge Oyee, Unanielewa Chief? Basi hii barabara uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Huu ni mwezi wa ngapi? (Mfugale: Mwezi wa tisa). Haya uandae document zote kabla ya mwezi wa 12 haujafika na kandarasi apatikane, niulize hela nitazitoa wapi. Sawa Mfugale?

Mfugale: Nimekuelewa mheshimiwa Rais

Magufuli: Umenielewa, mueleze na Waziri kwamba hayo ni maagizo yangu wala yasibadilike, Asante sana.

MWISHO WA MAONGEZI

Mambo niliyotoka nayo kwenye mawasiliano hayo ya simu ni:

1. Tumeishaifanyia feasibility studu.
2. Uitangaze kwa ajili ya kuijenga kwa kiwango cha lami.
3. Uandae documents kabla ya mwezi wa 12.

Katika wachangiaji, wapo wanaoashiria kwamba hii inafanyika kuwarubuni wapiga kura. Jee, hii ni kweli? Flyovers mbili zimejengwa Dar; daraja la Salender linajengwa; Terminal 3 uwanja wa Nyerere imejengwa. Ikulu imejengwa Dodoma. Sasa tuseme haya yote ni kwa ajili ya uchaguzi? Barabara hii ni muendelezo tu wa 'Hapa Kazi' kama mifano niliyoitaja. Zaidi ya hayo, umesikia feasibility study tayari imekwisha kamilika. Hii ni taarifa tosha kwamba mradi huu hauhusiani na uchaguzi. Au unataka miradi yote sasa isimamishwe mpaka uchaguzi utakapopita? Zaidi ya hayo, anayeagizwa anaambiwa akamilishe documents kabla ya Mwezi wa 12. Uchaguzi utakuwa umemalizika tayari. Hivyo kuhusisha mradi huu na uchaguzi siyo sahihi.

Mchangiaji mwingine anazungumzia rushwa na 10%. Kama suala hilo lingekuwepo, jee Mfugale angeagizwa autangaze mradi huo? Mambo si yangekuwa kimya kimya tu, unaamka unaona contractor yuko kazini. Hisia za rushwa ni mawazo binafsi tu anayokuwa nayo mchangiaji. Amekosa pa kuyatolea. Hivyo anayamwaga po pote tu.
 
Back
Top Bottom