Nyerere akiwa na John Rupia na Suleiman Takadiri, picha ya enzi za kupigania uhuru

Nyerere akiwa na John Rupia na Suleiman Takadiri, picha ya enzi za kupigania uhuru

Nimevutiwa na picha za watu waliwekwa kwenye kitambaa cha meza yenye vikombe juu yake.
 
Hapo Nyerere ana miaka 33 tu. Sasa leo hii nitafutie vijana wenye miaka 33 au zaidi miongoni mwa watu wetu kwenye siasa. Kwenye inshu kama hizi za kupambana na ukoloni mamboleo utawasikia "tutashtakiwa MIGA".
Zim...
Abdul Sykes alichukua uongozi wa TAA 1950 akiwa na umri wa miaka 26.

Alikuwa na fikra ya kuunda chama cha siasa kupigania uhuru wa Tanganyika akiwa na umri chini ya hapo.
 
Waislamu hawawezi kukubaliana na wewe juu ya hili.

Cc Mohamed Said
Mail...
Kujaribu kuandika historia ya TANU na kukwepa mchango wa Waislam hilo ni tatizo kubwa kwa kuwa matokeo yake utaishia bila ya kuwa na historia.

Chuo Cha CCM Kivukoni imejaribu "ujanja," huu na matokeo yake hakuna asiyeyajua.

Wakachapa kitabu ambacho Abdul Sykes hayumo, Sheikh Hassan bin Ameir na masheikh wenzake walioijenga TANU wote hawamo.

Wakabaki na historia ya Julius Nyerere ambayo bila Abdul Sykes na Hamza Mwapachu inakuwa haieleweki hata chembe.

Sasa nilipokuja mimi kuandika historia ya TANU kupitia Nyaraka za Sykes kishindo chake hakikusemeka.

Leo zaidi ya miaka 10 tuko hapa JF tunajadili historia hii na wasomaji wakitaka yakini wananiuliza mimi nitoe majibu.
 
Same story. Same results. Ni hivi, wa mbili havai moja. Tuachieni Tanzania njema isiyo na upendeleo wala matabaka. Haya mambo ya kufikiri nani zaidi, hayaijengi Tanzania. Makosa yaliyofanyika sisi mbona tunataka kuyarudia na kupitiliza badala ya kurekebisha?
Ila Mwenyezi Mungu ni fundi. Kila tukipanga upuuzi wetu, yeye anapangua. kama hatujajifunza hilo, tujiandae kuzikwa na masikitiko.
Rogo...
Ningesema kama unavyotaka wewe kuwa, "tuache," mimi ningekuwa nimewafanyia wazee wangu dhulma kubwa sana.

Wazee wangu ndiyo walioasisi African Association na hii African Association ndiyo iliyokuja kuzaa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, TAA kisha TANU.

Yote haya wamefanya Tanganyika iwe huru ili haki na usawa katika jamii ipatikane.

Uhuru umepatikana na kwa bahati mbaya sana historia yao ikafutwa na yale waliyopigania hayakufikiwa.

Mimi nimenyanyua kalamu kuandika historia ya watu hawa ili iwe mwongozo kwa kizazi cha sasa kuondoa hii dhahma.

Kama nisingeandika ungejuaje historia ya kweli ya TANU?
 
Du ni kitambo sana.inaonekana jiwe bado alikuwa chini ya ardhi na mawe menzake
 
Kamilisha bibliografia kwa kuweka:

Jina la mtunzi (mwaka), jina la kitabu (mji kilikochapishwa: kampuni ya uchapaji, mwaka wa uchapaji).
Mama...
Nimeacha makusudi ili kijana ahangaike ikiwa hawajui waandishi hawa.

Ikiwa hawajui hakuwa na sababu ya kutaka kufanya mjadala wa somo hana ujuzi nalo.
 
Mama...
Nimeacha makusudi ili kijana ahangaike ikiwa hawajui waandishi hawa.

Ikiwa hawajui hakuwa na sababu ya kutaka kufanya mjadala wa somo hana ujuzi nalo.
Heko msomi mwanahistoria,M.Saidi Nakupongeza, Kwa kujitahidi kuweka mambo wazi.

Tanzania itakulilia sana siku utakapotoweka na wakatambua makosa yao ya kutokuikusanya historia ya Tanganyika na Kuiandiak kiusahihi.

Lakini mimi nadhani kama ''Kuna kaji system kinadhibiti ukweli huu usijulikane vile! na si juikwa maslahi ya nani! ''

Shk .Mohamed Una lolote unaweza kusema juu ya hili ?
 
Battawi,
Tatizo la kuwa na historia ya TANU lilianza mapema baada ya uhuru wa Tanganyika.

TANU yenyewe ilitaka kuandika historia hii na kazi hii walipewa Abdul Sykes na Dr. Wilbard Kleruu.

Hii kazi haikukamilika na inaelekea tatizo alikuwa Abdul Sykes.

Abdul alianza kuandika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika na maisha ya baba yake alipoasisi African Association mwaka wa 1929.

Hili ndilo tatizo ambalo limedumu hadi leo.
 
John Rupia anaonekana alikua mtoto wa mjini sana, ana kibri flani hivi mjuaji na haogopi chochote,pia anaonekana alikua na exposure na amekulia kimjinimjini mzee wangu mohamedi nisaidie kama nimekosea maana nimemuangalia muonekano tu
 
Hatujiulizi historia ya kanisa katoliki before 1961 ikoje??Mbona kama hakuna kabisa?
Wala hakuna historia ya kanisa kupigania uhuru licha ya kuwepo kama taasisi decades kadhaa kabla ya Uhuru..

Something very fishy
Labda Kanisa enzi hizo ni part and parcel ya colonial machinery.
 
Watu wa pwani ni wapenda haki na uhuru, wakati waislam wanapambania uhuru wengi wa wakatoliki walikuwa wamejificha huko vichochoroni kwa woga na uzwazwa.

Mifano uko hai tawala za Mwinyi, JK na sasa Mama Samia zinajitanabaisha kuwa za angalay kuwa na uhuru na amani tofauti na wengine
Lakini Mkatoliki mmoja mahiri, akili kubwa ailiwaunganisha
 
Rogo...
Ningesema kama unavyotaka wewe kuwa, "tuache," mimi ningekuwa nimewafanyia wazee wangu dhulma kubwa sana.

Wazee wangu ndiyo walioasisi African Association na hii African Association ndiyo iliyokuja kuzaa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika, TAA kisha TANU.

Yote haya wamefanya Tanganyika iwe huru ili haki na usawa katika jamii ipatikane.

Uhuru umepatikana na kwa bahati mbaya sana historia yao ikafutwa na yale waliyopigania hayakufikiwa.

Mimi nimenyanyua kalamu kuandika historia ya watu hawa ili iwe mwongozo kwa kizazi cha sasa kuondoa hii dhahma.

Kama nisingeandika ungejuaje historia ya kweli ya TANU?

Nasoma kitabu cha PAUL BJERK. Hakuna ambaye hajatendewa haki. Ilikuwa haiwezekani kuenda next stage kwa TAA kama wasingewaalika wajanja wa enzi hizo kukaa viti vya mbele.

Sasa hivi Wazee wanaandika vitabu vyao. Wanapunguza haya mambo ambayo mengine hayabebi ukweli na uhalisia uliokuwepo enzi zile wakati baadhi ya matukio yanatokea. miujiza tena na tena isiyokauka
 
Mzee wetu Mohamed Said kilio chake kikubwa ni kutoona abdul sykes hatajwi
Kwenye historia

Ova
 
John Rupia anaonekana alikua mtoto wa mjini sana, ana kibri flani hivi mjuaji na haogopi chochote,pia anaonekana alikua na exposure na amekulia kimjinimjini mzee wangu mohamedi nisaidie kama nimekosea maana nimemuangalia muonekano tu

Angekuwa Ustadhi Mzee wetu Mohamed Said angemremba na kumpamba kwa mashairi lukuki.
 
Mzee wetu Mohamed Said kilio chake kikubwa ni kutoona abdul sykes hatajwi
Kwenye historia

Ova
Ni huyo tu? Hivi Abdul ndio alimshawishi Kambona kujiunga na TANU? Pengine historia iboreshwe...hao watu waandikwe. Na roles zao zitajwe. Ili tusiandikie mate wakati wino upo.

Nilikuwa naangalia historia ya mashahidi wa Uganda. Wale walioteswa na ufalme wa Buganda sababu ya kuupokea ukristu. Mwanzoni walikuwa 22. Nafikiri namba yao kwa sasa ni 24 kama sikosei. Hakuna lililoharibika.
Tunatumia muda mwingi na njia chafu kufanya kitu ambacho sio xha nguvu nyingi kama tunavyotaka umma uamini. Tunapoteza muda.
 
Back
Top Bottom