Nyerere alijenga vyuo vingapi? Watu wa mwanzo wamewarahisishia watu wa sasa

Nyerere alijenga vyuo vingapi? Watu wa mwanzo wamewarahisishia watu wa sasa

lee Vladimir cleef

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
9,571
Reaction score
35,485
Nchi yetu ina maendeleo kidogo sana ukilinganisha na rasilimali zetu, maliasili zetu, hali ya hewa yetu na utulivu wetu.

Hata hivyo maendeleo haya madogo yameletwa na kila mtu kwa nafasi yake,
Hata hivyo walioleta Maendeleo mwanzo wamesababisha wa leo kuendeleza kwa vile huwezi kurudia kufanya jambo lililokwisha fanywa.

Mfano Nyerere alijenga Muhimbili, Mwinyi akajenga kitengo cha macho, Mkapa akajenga kitengo cha mifupa MOI, Kikwete akajenga kitengo cha Moyo. Magufuli atajenga kitengo cha......

Nyerere alijenga Tazara, Mwinyi JKN Airport, Mkapa akajenga daraja la Mkapa na mabarabara na uwanja bora kabisa wa mpira kusini mwa jangwa la Sahara.

Kikwete daraja la kigamboni, uwanja wa ndege unaoendelea, mwendo kasi, UDOM nk.

Mfano mwingine Nyerere alijenga vyuo vingi sana vikubwa na vidogo.Kwa uchache: UDSM, IFM, Mzumbe,TMA,CCP,VETA nk.

Maana yangu ni kwamba kama tungekua tumepata Uhuru leo tungeanza na Nini? Kupanga ni kuchagua na kuchagua ni vipaumbele (priorities) aliyejenga mwanzo kamrahisishia anayejenga leo, waliojenga kale walikuwa wanaangalia umuhimu kwanza na uhitaji.


Wazo langu.
 
Back
Top Bottom