Nyerere alipofungua ‘Dance’ Msondo Ngoma

Nyerere alipofungua ‘Dance’ Msondo Ngoma

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2012
Posts
5,108
Reaction score
10,191
Nyerere alicheza Msondo, wewe nani usicheze?

Miaka 56 iliyopita, nazungumzia mwaka 1964, bendi mbili kubwa za Wilaya ya Ilala jijini Dar es Salaam, zilipiga dansi maalumu la kuchangia chama cha TANU.

Bendi hizo ni NUTA Jazz, Msondo Ngoma ambao mpaka sasa bado wapo katika ulimwengu wa muziki, na Dar Jazz Band wana Mundo au Majini wa Bahari.

Mgeni rasmi katika dansi hilo alikuwa Rais wa Tanzania wakati huo, Mwalimu Julius K. Nyerere. Soma tangazo, angalia na kiingilio kilikuwa Sh. 3 kwa mtu mmoja na Sh 5 kwa double.

Kwa ujeuri tangazo lipo kwa kiingereza, na kipindi hichi kiingereza ndio ilikuwa usomi.
1.jpg
 
Wakati huo Utunzi wa Mziki ulikuwa unalenga kuelimisha na kuhamasisha jamiii kuondokana na Maadui wa Taifa UJINGA, UMASKINI, na MARADHI na burudani kwa mbaaaali.
Enyi vijana Sikizeni, mnapokuwa masomoni......

Lkn sasa ni matusi matusi ua ngono tuuuu

.
 
Wazee Hawa Ni kuwaenzi hakika. Wamekua viongoz haswa. Uongozi Ni pamoja na kuwa "Social" a.k.a kujichanganya.
 
Ni kweli Babu alisoma darasa la 8 la mkoloni.
alikuwa anaongea kiingereza vizuri.
maana walikuwa wanafundishwa na wazungu na lugha ya kufundishia kilikuwa ni kiingereza.
Kiingereza ni lugha Kama lugha nyingine Kama haufanyi mazoezi ya kuongea na kuandika lazma utapotea
Kigalatia hakikuwa changamoto enzi hizo, tumeharibu kuanzia miaka ya 90. Tumebaki na ze ze ze
 
Ni kweli Babu alisoma darasa la 8 la mkoloni.
alikuwa anaongea kiingereza vizuri.
maana walikuwa wanafundishwa na wazungu na lugha ya kufundishia kilikuwa ni kiingereza.
Kiingereza ni lugha Kama lugha nyingine Kama haufanyi mazoezi ya kuongea na kuandika lazma utapotea
Exactly, watu wa darasa la 4 walikuwa wanagonga English vizuri tu. Lugha ni lugha tu, upate mwalimu mzuri ukiongeza na mazoezi, mambo yanakuwa bam bam. Lakini tumedharau sana masomo ya lugha; walimu wenyewe kiingereza hawajui, watamfundisha nani, tukirudi mtaani; hata maigizo yote yametafsiriwa kiswahili, tutajifunza wapi.
 
tatizo la kiingereza naona lipo kwenye shule za serikali.
Ila za English medium walimu wake wanajitahidi Sana
Nakutana na watoto wanapiga kiingereza kule beach na wazazi wao Hadi raha.
Mtoto anajengewa uwezo mapema.
Akikuwa ATAWEZA kujieleza vizuri.
Kuna watu wana degrees lakini kujieleza kwa kiingereza hawajui

Hadi miaka ya 2000 tv za tz ikiwemo itv, tbc zilikuwa na taarifa za habari za kiingereza

Ila kadri siku zinaenda hizo habari kwa lugha hizo zimefutwa

Kiswahili kimekuwa kwa kasi kuliko kiingereza
Kiswahili kinakuwa kwa kasi sana hata mataifa Jirani, yaani ni sana
 
tatizo la kiingereza naona lipo kwenye shule za serikali.
Ila za English medium walimu wake wanajitahidi Sana
Nakutana na watoto wanapiga kiingereza kule beach na wazazi wao Hadi raha.
Mtoto anajengewa uwezo mapema.
Akikuwa ATAWEZA kujieleza vizuri.
Kuna watu wana degrees lakini kujieleza kwa kiingereza hawajui
Na wtt wa hivyo hadi majumbani mwao wanaongeleshwa English.
 
Back
Top Bottom