Nyerere angetuvusha kipindi kama hiki bila shida

Nyerere angetuvusha kipindi kama hiki bila shida

Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere angekuwepo kwenye Corona ndio angefanya nini?!.
Sisi tuliokuwepo baaa ya vita vya Kagera, ile 1979, ilitangazwa miezi 18 ya kakaza mikanda, unajua ilichotokea na hiyo miezi 18 ilikwisha lini?.
Mwacheni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere apumzike kwa amani, Tetemeko la Kagera alisababisha nani?, kivuko alikizamisha nani?, mafuriko ameleta nani, na sasa hii Corona kaleta nani?.
Kwa nchi masikini kama Tanzania ambayo wengi wa watu wake wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, ili wale ni lazima watoke, hivyo hakuna kuwajali watu hawa zaidi ya kuwakabidhi kwa Mungu, ndicho alichofanya rais Magufuli na ikitokea ukatokea mlipuko kama wa Italy au Marekani, then huo ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania.
P
Ama kweli Tanzania kuna watu wenye imani..... Nimependa movement ya mawazo yako..... Hakuna namna zaidi ya kuwakabidhi watanzania mikononi mwa mungu..... Yeye ndio anajua limekujaje.... Na litaondoka lini...

Nendeni msome biblia kuhusu nabii ELIYA.... Alifunga mbingu miaka mitatu na nusu.... Mungu aliruhusu..... Kitabu cha wafalme.... Corona kama imezuka kiushetani originally sisi hatuwezi pambana nayo....Mungu tu peke.... Tena ushike na usikie kwa makini....... Ni mungu pekee watanzania wenzangu.... Tusilaumiane.... Mimi ni daktari lakini naogopa pia..... Mungu awalinde wote..... Kama unaamini ulinzi kutoka kwa mungu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Najua ukweli unauma lakini lazima tuseme hata kama inauma mwaka 1978 kulitokea vita ambayo ilileta madhara makubwa kwa taifa kipindi hicho baada ya vita kulitokea hali mbaya sana kiuchumi na njaa kali ila mwalimu hakukimbia, hakukata tamaa alikuwa mtu wa watu hakuona aibu alienda nje na kuomba msaada ili kuwasaidia Watanzania na alifanikiwa

Leo ukiwatazama watawala wa leo hauoni haiba ya uongozi machoni mwao unaona wanaficha mambo unaona hawana plan za kuwasaidia watanzania ndani ya janga au baada ya janga,

Ushahidi ni janga la tetemeko kagera, kuzama kwa kivuko kule ukelewe, mafuliko na sasa janga la corona.

Ukiangalia kwa jicho la tatu huenda corona haitaua watu sana lakini itasababisha mtikisiko wa kiuchumi kwa watanzania wengine washaanza kupoteza ajira wengine mfano walimu wa private school mishahara yao imesimama je serikali inajua ni wananchi kiasi gani wameshapoteza kipato na jinsi ya kuwasaidia?

Baba wa taifa asingekubali, je watawala wa leo wanajali?.

Kalale nae uko kaburini akuvushe


Sent from my iPhone using Tapatalk
 
Back
Top Bottom