Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere angekuwepo kwenye Corona ndio angefanya nini?!.
Sisi tuliokuwepo baaa ya vita vya Kagera, ile 1979, ilitangazwa miezi 18 ya kakaza mikanda, unajua ilichotokea na hiyo miezi 18 ilikwisha lini?.
Mwacheni Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere apumzike kwa amani, Tetemeko la Kagera alisababisha nani?, kivuko alikizamisha nani?, mafuriko ameleta nani, na sasa hii Corona kaleta nani?.
Kwa nchi masikini kama Tanzania ambayo wengi wa watu wake wanaishi kwenye lindi la umasikini uliotopea, ili wale ni lazima watoke, hivyo hakuna kuwajali watu hawa zaidi ya kuwakabidhi kwa Mungu, ndicho alichofanya rais Magufuli na ikitokea ukatokea mlipuko kama wa Italy au Marekani, then huo ndio mpango wa Mungu kwa Tanzania.
P