Nyerere Day: Julius Nyerere, Dossa Aziz na Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam 1958

Nyerere Day: Julius Nyerere, Dossa Aziz na Ujenzi wa Chuo Kikuu Cha Dar-es-Salaam 1958

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
NYERERE DAY: MWALIMU NYERERE NA DOSSA AZIZ WALIPOKUBALIANA KUJENGA CHUO KIKUU WAKIWA WAMEEGESHA GARI MLIMANI

Viongozi wa TANU walikuwa na kawaida wakimaliza mkutano wa hadhara Mnazi Mmoja watakatiza barabara kwa miguu kuja Princess Hotel wakafanya tathmini ya mkutano, kula chakula na kunywa.

Mwenye hoteli hii alikuwa Muhindi mmoja jina lake Ommy.

Hapa ni sehemu moja ambayo Dossa Aziz alipopatia jina lake la utani, ''The Bank.''

Hapo labda zitaunganishwa meza mbili tatu na vijana wote viongozi wa TANU wakuwapo hapo - Julius Nyerere, Dossa Aziz, Abdul, Ally, Abbas Sykes, Zuberi Mtemvu, Steven Mhando na vijana wengine kwa kuwataja wachache.

Hapo wakila na kunywa watazungumza mkutano ulikuwaje na mahudhurio yalivyokuwa nk. nk.

Bili ikitoka Dossa Aziz anaomba apewe yeye.

Hii ilikuwa kawaida yake.

Baada ya kumaliza Dossa atamchukua Nyerere katika gari yake kumrudisha nyumbani kwake Pugu.

Jua linakuwa limeshatua.

Njia ya zamani kwenda Pugu ilikuwa inapita kilipo leo Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam.

Siku moja wakiwa wanapita njia hiyo kwenda Pugu Dossa akasimamisha gari yake wakatoka nje kidogo kupunga upepo kabla ya kuendelea na safari yao.

Dossa na Nyerere wakawa wanautazama mji wa Dar es Salaam kutoka Mlimani na taa zake zinavyowaka.

Dar es Salaam ilikuwa inapendeza kwa zile taa.

Nyerere akafungua kinywa chake anamwambia Dossa, ''Dossa tukipata uhuru wetu hapa mahali tujenge Chuo Kikuu.''

Ndoto hii ya marafiki hawa wawili TANU ilikamilisha uhuru ulipopatikana mwaka wa 1961.

Lakini mchango wa kujenga Chuo Kikuu ulianza mwaka wa 1961.

Soma hapo chini majina ya wazalendo waliochangia ujenzi wa Chuo Kikuu:

WALIOCHANGIA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM 1958
1. Salum Abdallah
2. DPK Makwaia
3. JK Nyerere
4. Juma Mzee
5. Ibrahim Bofu
6. Schneider Plantan
7. Abdallah Said
8. Athman A’rahman
9. Jayanti Stores
10. Ali Chande
11. Kondo Salum
12. Athuman Azun
13. Lucas Masungwa
14. Mahadi Mwinyijuma
15. Abbas Sykes
16. Makatta Mwinyimtwana
17. Elias Millinga
18. Abbas Max
19. Salum Athmani
20. Kasongo Juma
21. Alli Mohamed
22. Mohamed Seif
23. Messers Thankers
24. Hamis Hassan
25. Hassan Tambwe
26. Sultan Dibega
27. Yusuf Abdallah
28. M.Selemani
29. Rajabu Athumani

Wangapi wanayajua haya?
 
Mmmm una uthibitisho wahusika hao uliowataja ambao 22 kati yao ni Waislamu ndiyo walichangia ujenzi wa chuo kikuu?!

Unaweza taja gharama halisi za ujenzi wa udsm?
 
Back
Top Bottom