Tunakosa capital mkuu, hata kama ardhi yetu ina dhahabu na almasi kama mchanga, tunahitaji capital ili kunufaika na hizo rasilimali.
Lakini pia, siasa na uongozi kwa sasa tuna mapungufu makubwa sana. Connection kati ya uongozi na watu imekufa kabisa, kwa hiyo huwezi kufanya chochote.
Uongozi haupo tena kwa kunufaisha watu, na hivyo watu hawana mwamko wa kuendeleza nchi, bali kuangalia nchi inawezaje kuwaendeleza wao, iwe kwa kuiba au namna yoyote ya ufisadi. Ndio maana watu wanaiba hadi alama za ishara za barabarani, ili mradi tu waiibie nchi kitu fulani.