Nyerere, Mwinyi na Mkapa walipewa udaktari wa heshima lakini hawakutumia kunani hawa wanaoutumia?

Nyerere, Mwinyi na Mkapa walipewa udaktari wa heshima lakini hawakutumia kunani hawa wanaoutumia?

Ni kawaida kwa marais wa Kiafrika kupewa udaktari wa heshima japo ni nadra kwa marais wa nchi za magharibi. ingawa rais Barak Obama anaweza kuvunja rekodi ya kuzipokea lakini asijiite dokta hata mara moja.

Je, ni kwanini? Je ni ile hali ya kutaka sifa, kutojiamini, kupenda ujiko bila kuusotea au je tutajuaje kama wahusika wananunua shahada husika? Je anapopewa shahada ya heshima rais ni mali yake au mali ya nchi?

Je, ilikuwaje mfano, Jakaya Kikwete akajiita daktari wakati hata master's hana? Je na Samia naye atakuwa limbukeni kama Kikwete aridhike na kuitwa daktari wakati hana hata shahada moja inayotambulika aliyoipata kihalali? Je ilikuwaje wasomi bobezi kama Nyerere na Mkapa hawakutumia shahada nyingi za heshima za uzamivu walizopewa? Naomba kutoa hoja.
...Maswali Mazuri. Ogopa Viongozi wa Kiafrika Wanavotaka kujikweza bila kukutolea Jasho kujikweza huko !! [emoji57][emoji57]
 
Kabla ya Kuwalaumu Kutumia Au Kutotumia Ingependeza Utujulishe Nini hasa kusudio la Kuwatunuku Ili iweje Ili Baada ya Kuwatunuku waweje ,au wafanyeje namaanisha Hivi
Kuwaita au kutowaita

Nikiwa na Maana Inawezekana Badala ya Kuwalaumu Kwa kulitumia neno Dr,
Pengine Tulipaswa kuwapongeza Kwakuwa Wameitendea haki Thamani ya tunu waliyotunukiwa

Au Pengine Hao wasiotumia Uliowaorodhesha Inawezekana hawakuitendea haki Thamani waliyopewa

Nirudie Tena Tupeni Maana halisi au kusudio halisi la Hiyo tunu ya Udaktari Baada ya kupewa Ili wafanyeje

Au wakitumia tunafaidikaje au tunakosa Nini na wasipotumia tunapata au tunakosa Nini.

Na Kwa Maelezo Yako inavyoonyesha Kuwa si Vizuri Kuzitumia Kwakuwa sio Udaktari wa kusomea
Kwa Maana PhD ya darasani ni Kitu kikubwa Sana.

Huu Udaktari wa heshima ni Kitu ambacho Hakina maana sana au ni Kitu kikubwa sana tofauti na Watu hao waliotunukiwa

Kwamba kama wanapewa Bila stahili au Kwa upendeleo Fulani tu au Hawana mchango unaostahili katika jamii Hivyo hawakipaswa kutunukiwa au Hata Kutumia hawakustahili.

Katika Hili nastahili kuelimishwa.
Hawaatahili na hawana sifa Za kuwafanya waswahili
 
Najua unamsema mbunge wako Dr Taletale mzee wa kuongea kwa mapozi Namaanisha ki Phd na kupinda kiuno kidizaini.

Shikamoo Mh Mb. Dr Taletale
 
Back
Top Bottom