SI KWELI Nyerere ni baba mzazi wa Freeman Mbowe

SI KWELI Nyerere ni baba mzazi wa Freeman Mbowe

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Wakuu kwema?

Kuna sehemu nilisikia wana wanasema hili kuhusu Mbowe kuwa na uhusiano wa damu na Hayati Mwl. Julius Nyerere, wakawa wanasema hata jinsi Mbowe alivyofanana na Nyerere kwamba kuna uhusiano zaidi ya familia zao kuwa marafiki lakini kweli ni kwamba Mbowe ni mtoto wa Nyerere.

Eti jamani hili kweli? Kuna kaufanano hapa?

julius-nyerere.jpg
mbowe.jpg

 
Tunachokijua
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alikuwa Rais wa kwanza wa Tanzania. Alizaliwa Butiama, mkoani Mara pembezoni mwa Ziwa Nyanza tarehe 13 Aprili, 1922. Alifariki dunia 14 Oktoba, 1999. Aliiongoza Tanganyika na baadaye ikaitwa Tanzania (Tanganyika na Zanzibar ziliungana mwaka 1964 na kuwa Tanzania) toka mwaka 1961 hadi mwaka 1985. Nyerere alipigania uhuru wa Tanganyika toka kwa mkoloni na Tanganyika kuwa huru 9,12,1961.
images

Picha: Mwalimu Julius Kambarage Nyerere

Freeman Aikaeli Mbowe amezaliwa 14 Septemba 1961 Wilaya ya Hai mkoa wa Kilimanjaro ni mwanasiasa Mtanzania, mwanachama na mwenyekiti wa Chama cha kisiasa cha Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA).

Alikuwa mmoja wa waasisi wa CHADEMA mwaka 1992. Freeman Mbowe alikuwa mbunge wa Jimbo la Hai lililopo mkoa wa Kilimanjaro tangu mwaka 2000 hadi 2020.

images

Picha: Freeman Aikael Mbowe
Familia ya Mbowe
Freeman Mbowe alizaliwa na wazazi Aikael Alfayo Mbowe na Mama Aishi Ephraimu Shuma akiwa mtoto wa 10 kwa baba yake na mtoto wa 9 kwa Mama yake, ivyo yeye kuwa mtoto wa mwisho kwa baba na Mama.

241824745_2207375176070628_1977814343269786168_n.jpg

Picha: Aikael Mbowe pamoja na Aishi Mbowe wakiwa na mtoto wao Freeman Mbowe

Freeman Mbowe alibatizwa 09,12,1961 siku ya Uhuru wa Tanganyika na kupewa jina Freeman maana yake mtu huru. Baba wa Ubatizo wa Freeman Mbowe alikuwa Mwalimu Nyerere.

Nilizaliwa mwaka 1961 mwaka ambao nchi yetu ilipata uhuru tarehe 14/9/1961 na nikabatizwa siku ya 9/12/1961 siku bendera ya mwingereza yaani (Union Jack) inashushwa na mimi nikabatizwa siku ya uhuru kwa maana 1961 nikapewa maji ya uzima ya ubatizo na ndio sababu nikapewa jina la Freeman ikiwa na maana mtu huru kwa sababu nilibatizwa siku ya uhuru baada ya kuzaliwa mwaka wa Uhuru.Alisema Mbowe kwenye kipindi cha Speaking out with Tundu Lissu

Uhusiano wa Mwalimu Nyerere na familia ya Freeman Mbowe ulianzia wapi?
Kwa mujibu wa Freeman Mbowe kwenye Mahojiano kati ya Tundu Lissu na Freeman Mbowe yaliyofanyika katika kipindi cha Speaking out with Tundu Lissu, alisema kuwa Julius Kambarage Nyerere na Aikael Alfayo Mbowe walikuwa na mahusiano ya karibu sana na mahusiano yao yalianzia kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

Lissu: Hebu tuambie Mzee Mbowe alikuwa na connection gani na Mwalimu Nyerere au na mambo ya kisiasa, siasa za TANU?

Mbowe:Kwa kweli nikiri tu kwamba wakati Mzee anaanza kufanya mambo ya siasa na akina Mwalimu na wazee wenzake mimi nilikuwa bado ni mtoto mdogo sana lakini historia nimeikuta simulizi nimezipata maandiko nimeyakuta, Mzee alikuwa na mahusiano ya karibu sana na Mwalimu Nyerere na mahusiano yao yalianzia kwenye harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika.

images

Picha: Mwalimu Nyerere akiwa nyumbani kwa Mzee Aikael Mbowe
Mzee Mbowe alikuwa na umashuhuri katika Tanganyika kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Kaskazini ya Kilimanjaro, Arusha na Manyara na alikuwa na uhusiano na watawala wa kiasili, kuanzia Mangi Maruma wa Rombo, Mangi Shangali wa Machame, alikuwa karibu nao kutokana na umashuhuri wake kabla ya uhuru.

Katika mazingira kama hayo baba alikubaliana na wenzake kadhaa kuhamasisha harakati za kutafuta uhuru wa Tanganyika katika kanda ya Kaskazini kwa kuwa watawala wa jadi walikuwa na nguvu sana na walihitaji mtu ambae alikuwa na ushawishi mkubwa sana na waliweza kuingiza TANU kanda ya kaskazini hasa sehemu ya Kilimanjaro na hapo ndio mahusiano ya familia ya Mwalimu ilipoingia kwenye familia yetu na alikuwa na ukaribu hata na Oscar Kambona na wazee wengine kadha wa kadha ambao walishiriki katika harakati za uhuru wa nchi kwa hiyo historia ya Mwalimu na baba ilikuwa hivyo.


236390015_3700913423342698_1527663344093574438_n.jpg

Picha: Aikael Mbowe akisalimiana na Mwalimu Nyerere
Je, ni kweli Mbowe ni mtoto wa damu wa Nyerere?
Kwa mujibu wa historia ya mahusiano kati ya Nyerere na familia ya Mbowe hakuna ushahidi wowote unaoweza kuthibitisha kuwa Mbowe ana uhusiano wa damu na Nyerere.

Uhusiano wao unabaki kuwa wa urafiki wa familia pamoja na Kiimani kwa kuwa Nyerere ni baba wa ubatizo wa Freeman Mbowe.

Hawa ndio Watoto wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Mwalimu Nyerere alikuwa na watoto 8 nao ni:-
1.Andrew Burito alizaliwa mwaka 1953. Andrew ni jina la rafiki wa Mwalimu na Burito ni jina la baba yake
2.Anna Watiku alizaliwa 1954, Hili ni jina la bibi wa Mwalimu Nyerere.
3.Anselm Magige, jina limetokana na baba yake Mama Maria
4.John Guido alizaliwa 1957; Alipata heshima ya kupewa jina la babu yake yaani Nyerere
5.Charles Makongoro alizaliwa 1959; Alizaliwa mwaka ambao chifu Makongoro alifariki
6.Godfrey Madaraka, Alizaliwa mwaka ambao Tanganyika ilipata Serikali ya madaraka kamili.
7.Rosemary; Huyu alipewa majina matatu moja wapo ni Huria yani "Uhuru Year" kwani alizaliwa mwaka wa
Uhuru 1961.
8.Pauleta; Hakuwa mtoto wa Mwalimu(Wa Kumzaa) ila walishi naye, akaitwa Nyabanane maana ni wa
nane.
Jamiiforums, imejiridhisha kuwa suala la Mbowe kuwa na uhusiano wa damu na Hayati Mwl. Julius Nyerere, ni la kinadharia, halina uhalisia wowote.
Wakuu kwema?

Kuna sehemu nilisikia wana wanasema hili kuhusu Mbowe kuwa na uhusiano wa damu na Hayati Mwl. Julius Nyerere, wakawa wanasema hata jinsi Mbowe alivyofanana na Nyerere kwamba kuna uhusiano zaidi ya familia zao kuwa marafiki lakini kweli ni kwamba Mbowe ni mtoto wa Nyerere.

Eti jamani hili kweli? Kuna kaufanano hapa?

View attachment 2699799View attachment 2699801
Kwenye huo huo ukaribu wa kifamilia hakuna chochote kisicho cha kawaida kilichotokea hapo. Manake mashemeji zetu hawa hana.
 
Back
Top Bottom