Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

mpk

JF-Expert Member
Joined
Sep 26, 2012
Posts
3,115
Reaction score
3,864
Mwl Nyerere atakumbukwa kwa mengi kama ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, Amani na upendo, lugha ya kiswahili, umoja wa kitaifa, ujamaa, ukombozi wa ardhi ya Tanzania toka kwa nduli Amin nk.

Hata hivyo hatutakusahau kwa kutuachia genge la mafisadi Ccm, na nina imani kama kuna dhambi unatumikia adhabu yake na inakuchelewesha pengine kutangazwa mtakatifu basi ni kutuachia hawa jamaa.

Kuanzia kuiba kura, kuua tembo wetu, kugawa rasrimali zetu, kutesa na kuua watu, madawa ya kulevya, kugawiana vyeo kindugu, kutuchonganisha kiimani, kubaka demikrasia nk nk. Sasa wamefikia hatua ya kughushi hata sahihi yako kuharalisha uharibifu wako!!!!

Upumzike kwa amani baba, tulio hai tutazidi kukuombea huruma ya muweza yote Amina!
 
Aiseeeeeeee!! Hvi kila mtu anaekufa anapumzika kwa amani ????
 
Mwl. Nyerere is a great man; hilo halina ubishi. Ana mengi mazuri aliyolifanyia taifa kama Kiongozi na Kamanda Mkuu. Hata hivyo, kama binadamu anayo mapungufu pia. Ukisoma kitabu cha Pius Msekwa (the former Clerk of the National Assembly, Clerk of CCM, VC of UDSM, Speaker of the National Assembly, Member and Chairperson of Boards of several institutions, etc.) kiitwacho "50 Years of Independence" cha Januari 2014, ambacho gazeti la MA.WIO la leo Aprili 3, 2014 limekichambua, unaweza kuona upande wa pili wa Nyerere hususan kuhusu Muungano. Naomba nisieleze zaidi, tafuteni hicho kitabu au gazeti msome ili kujua kwa undani aina ya muungano wa Nyerere tulio nao.
 
Mkuu hapa una hoja ya msingi.Na kitu kingine kufuta mfumo wa vyama vingi matokeoa yake leo watu wamekariri CCM licha ya udhalimu wao kwa watanzania.Ingawa baadae ndie alishauri mfumo wa vyama vingi uruhusiwe licha ya zaidi ya asilimia 80 ya watanzania kuukataa katika ripoti ya Nyalali,it was already too late.

Tungekuwa na mfumo wa vyama vingi tangu uhuru CCM leo isingetawala siasa za Tanzania.
 
Mwl Nyerere atakumbukwa kwa mengi kama ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, Amani na upendo, lugha ya kiswahili, umoja wa kitaifa, ujamaa, ukombozi wa ardhi ya Tanzania toka kwa nduli Amin nk.

Hata hivyo hatutakusahau kwa kutuachia genge la mafisadi Ccm, na nina imani kama kuna dhambi unatumikia adhabu yake na inakuchelewesha pengine kutangazwa mtakatifu basi ni kutuachia hawa jamaa.

Kuanzia kuiba kura, kuua tembo wetu, kugawa rasrimali zetu, kutesa na kuua watu, madawa ya kulevya, kugawiana vyeo kindugu, kutuchonganisha kiimani, kubaka demikrasia nk nk. Sasa wamefikia hatua ya kughushi hata sahihi yako kuharalisha uharibifu wako!!!!

Upumzike kwa amani baba, tulio hai tutazidi kukuombea huruma ya muweza yote Amina!

Mwalimu Nyerere waite wote hawa wajumbe wa bunge la katiba waje uliko uhojiane nao, ndilo suluhisho. Wapande ndege ya malaysia waje kwako muongee na muafaka utapatikana
 
Kimeletwa na wazee wa Kariakoo.
Nyerere, mwenyewe kakiri mara nyingi kuwa hajui kiswahili vizuri kafundishwa hao Wazee.

Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 kawakuta watu wanaongea kiswahili leo mnakuja na drama zenu za kumsifia Nyerere kila kitu.

Yaani mtu atoke Butiama aje kuwafundisha kiswahili wakazi wa ukanda wa Pwani.
 
Hahaha daaah aisee hii ndo
tanzania

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Nyerere, mwenyewe kakiri mara nyingi kuwa hajui kiswahili vizuri kafundishwa hao Wazee.

Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 kawakuta watu wanaongea kiswahili leo mnakuja na drama zenu za kumsifia Nyerere kila kitu.

Yaani mtu atoke Butiama aje kuwafundisha kiswahili wakazi wa ukanda wa Pwani.

Mbona mapovu? Kwani nimesemaje? Nimesema kimeletwa na wazee wa Kariakoo. Sisi wengine wakuja tu, Kiswahili ni chenu wazee wa mwambao; so what? Kiingereza chenyewe cha Mwingereza (England) leo hii mtumiaji mkuu duniani ni India na Marekani ndio uturingishie Kiswahili hata maneno fasaha ya kutongozea hakina. Kama vipi kiwekeeni hatimiliki tuelewe moja.
 
Kwa hayo, mfahamishe mleta mada kuwa anapotosha anapoweka Kiswahili kama kama moja ya sifa za Nyerere.
 
fanya kutafakari maandiko kwanza!! jamaa wala hakusema nyerere kaanzisha kiswahili ila kama ukituliza ubongo wako vizuri nadhani jamaa alimaanisha alienzi kiswahili, ukimchukia mtu uwe na sababu
 
Hakuna mahali popote nilipomuunga mkono wala sio jukumu langu kufanya unachotaka nifanye.
 
fanya kutafakari maandiko kwanza!! jamaa wala hakusema nyerere kaanzisha kiswahili ila kama ukituliza ubongo wako vizuri nadhani jamaa alimaanisha alienzi kiswahili, ukimchukia mtu uwe na sababu

Mkuu hili genge lina chuki za ajabu.
 
Mwl Nyerere atakumbukwa kwa mengi kama ukombozi wa nchi za kusini mwa Afrika, Amani na upendo, lugha ya kiswahili, umoja wa kitaifa, ujamaa, ukombozi wa ardhi ya Tanzania toka kwa nduli Amin nk.

Hata hivyo hatutakusahau kwa kutuachia genge la mafisadi Ccm, na nina imani kama kuna dhambi unatumikia adhabu yake na inakuchelewesha pengine kutangazwa mtakatifu basi ni kutuachia hawa jamaa.

Kuanzia kuiba kura, kuua tembo wetu, kugawa rasrimali zetu, kutesa na kuua watu, madawa ya kulevya, kugawiana vyeo kindugu, kutuchonganisha kiimani, kubaka demikrasia nk nk. Sasa wamefikia hatua ya kughushi hata sahihi yako kuharalisha uharibifu wako!!!!

Upumzike kwa amani baba, tulio hai tutazidi kukuombea huruma ya muweza yote Amina!

Hizo sifa za Nyerere ulizompa zote za uongo.

Amani na upendo ulikuwepo kabla ya ujio wake na hata alipotoka kwao kuja Dar alikaribishwa kwa amani na upendo na akapewa chumba, kula, kulala na akina Sykes, vijana wa mjini Dar enzi hizo.

Kuhusu Ukombozi wa Afrika Kusini, hilo ni changa la macho, si yeye, ilimbidi awepo kwenye mkumbo akipenda asipende. Wakimbizi kutokea Kusini kwenda Kaskazini wakimbilie wapi bila ya kuja Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika?

Ni mfano wa Kenya na Somalia leo hii, Wasomali wengi wapo Kenya leo hii kuliko nchi nyingine yeyote duniani baada ya Somalia kwenyewe, kwa kuwa ndio wa karibu na ndipo kwenye ndipo kimbilio la karibu.

Kuhusu Ujamaa, atakumbukwa sana kwa kuwa huo ujamaa wake ndiyo uliifanya hii nchi kuwa masikini kukliko wote duniani.

Kiswahili, alikikuta kikiongewa Afrika Mashariki nzima, na yeye mwenyewe kakiri kuwa alikuwa hakijui vizuri akafundishwa na vijana wa Dar wa enzi hizo, kwa sasa tunawaita wazee wa Dar.

Umoja wa Kitaifa, Tanganyika ilikuwa na umoja wa Kitaifa toka enzi hizo, ndiyo maana Mzanaki akaweza kuja Dar na kupokelewa na kuishi bila bughdha.

La Idi Amin, hili lina mjadala mrefu sana wa kiitikadi za kidini.

Kwa kifupi sikioni cha maana cha kumsifia Nyerere ispokuwa kimoja tu, ni kweli kabisa anastahili kila sifa kwa kulikuza Kanisa Katoliki Tanzania na kulifanya ndiyo lenye kuhodhi ardhi kubwa Tanzania baada ya Serikali na kulifanya kanisa katoliki na wakatoliki kuwa wa mwanzo kwa kila jambo katika Tanzania. Kwa hili sibishi, ambalo wewe umelisahau hujaliweka kwenye sifa zake.
 
fanya kutafakari maandiko kwanza!! jamaa wala hakusema nyerere kaanzisha kiswahili ila kama ukituliza ubongo wako vizuri nadhani jamaa alimaanisha alienzi kiswahili, ukimchukia mtu uwe na sababu
Kupingana na utotoshaji ndiyo kumchukia Nyerere.
 
Mbona mapovu? Kwani nimesemaje? Nimesema kimeletwa na wazee wa Kariakoo. Sisi wengine wakuja tu, Kiswahili ni chenu wazee wa mwambao; so what? Kiingereza chenyewe cha Mwingereza (England) leo hii mtumiaji mkuu duniani ni India na Marekani ndio uturingishie Kiswahili hata maneno fasaha ya kutongozea hakina. Kama vipi kiwekeeni hatimiliki tuelewe moja.
Povu lipo wapi, hizo drama zako mueleze mleta mada.
 
Nyerere hakuwa mswahili alifika Dar akiwa amevaa kaptula. Waswahili hawavai kaptula.
 
Nyerere, mwenyewe kakiri mara nyingi kuwa hajui kiswahili vizuri kafundishwa hao Wazee.

Nyerere kaja Dar es Salaam mwaka 1952 kawakuta watu wanaongea kiswahili leo mnakuja na drama zenu za kumsifia Nyerere kila kitu.

Yaani mtu atoke Butiama aje kuwafundisha kiswahili wakazi wa ukanda wa Pwani.

Hebu jaribu kufikiri kwa upana zaidi sidhani kama amemaanisha Nyerere ndo kawafundisha Watanzania Kiswahili.

Sent from my BlackBerry 9800 using JamiiForums
 
Nyerere hakuwahi kuvaa manguo ya CCM ila aliwahi kuvaa magwanda ambayo yanafanana na nguo wanazovaa chama fulani
 
Back
Top Bottom