Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

Hizo sifa za Nyerere ulizompa zote za uongo.

Amani na upendo ulikuwepo kabla ya ujio wake na hata alipotoka kwao kuja Dar alikaribishwa kwa amani na upendo na akapewa chumba, kula, kulala na akina Sykes, vijana wa mjini Dar enzi hizo.

Kuhusu Ukombozi wa Afrika Kusini, hilo ni changa la macho, si yeye, ilimbidi awepo kwenye mkumbo akipenda asipende. Wakimbizi kutokea Kusini kwenda Kaskazini wakimbilie wapi bila ya kuja Tanzania na kabla ya hapo Tanganyika?

Ni mfano wa Kenya na Somalia leo hii, Wasomali wengi wapo Kenya leo hii kuliko nchi nyingine yeyote duniani baada ya Somalia kwenyewe, kwa kuwa ndio wa karibu na ndipo kwenye ndipo kimbilio la karibu.

Kuhusu Ujamaa, atakumbukwa sana kwa kuwa huo ujamaa wake ndiyo uliifanya hii nchi kuwa masikini kukliko wote duniani.

Kiswahili, alikikuta kikiongewa Afrika Mashariki nzima, na yeye mwenyewe kakiri kuwa alikuwa hakijui vizuri akafundishwa na vijana wa Dar wa enzi hizo, kwa sasa tunawaita wazee wa Dar.

Umoja wa Kitaifa, Tanganyika ilikuwa na umoja wa Kitaifa toka enzi hizo, ndiyo maana Mzanaki akaweza kuja Dar na kupokelewa na kuishi bila bughdha.

La Idi Amin, hili lina mjadala mrefu sana wa kiitikadi za kidini.

Kwa kifupi sikioni cha maana cha kumsifia Nyerere ispokuwa kimoja tu, ni kweli kabisa anastahili kila sifa kwa kulikuza Kanisa Katoliki Tanzania na kulifanya ndiyo lenye kuhodhi ardhi kubwa Tanzania baada ya Serikali na kulifanya kanisa katoliki na wakatoliki kuwa wa mwanzo kwa kila jambo katika Tanzania. Kwa hili sibishi, ambalo wewe umelisahau hujaliweka kwenye sifa zake.

We bibie ukianzisha bendi ya taarabu utaimudu vizuri sana. Kipaji unacho. Hongera sana kwa kujaaliwa hicho kipaji. Ni ushauri tu......
 
Wanaomchukia Nyerere kwa chuki za kidini kama FaizaFox hawana hoja kabisa. Anasema wakimbizi wa kusini mwa Afrika walitakwa waje Tanzania kwani ni karibu. Yaani mtu aruke Namibia, Msumbiji, Zimbabwe, Zambia, Botswana aje Tanzania alafu useme Tanzania ndo karibu???

Kuhusu Amin sijui mna hoja gani kwamba kuna suala la udini, mi natokea Kagera na nina ndugu Uganda. Sitaki mkaririshwe vitu vya ajabu! Uganda ni moja ya nchi ambazo watu wake hawabaguani kidini kama ilivyo kwetu, waislamu Uganda ni chini ya asilimia 15 lakini wanaheshimika sana. Ukatoriki ni dini kuu kule kwa sababu ya historia ya mashaidi wa Uganda lakini kuna umoja wa hali ya juu.

Baada ya kupinduliwa Amini nchi alipewa Prof Yusuf Rule ambaye ni mwislamu ingawa waliokuwa wanaoongoza mapambano ni wakristo akina Milton Obote na Yoweri Mseveni! Katika matukio makubwa ya kikatiri kufanya Amin aliwahi kumuua kwa mkono wake Askofu Luwumu. Pamoja na umaarufu wake mpaka kuna mtaa unaitwa Luwumu Street haikuwahi kuchukuliwa mauaji hayo kama ya kidini nchini Uganda.

Kuhusu kiswahili sikusema Nyerere alileta kiswahili, namaanisha alikifanya kuwa lugha ya taifa. Kwa kauli yake umesema alikuwa hajiu kiswahili, ndiyo! kama angetaka lugha ya kiswahili iwe kizanaki nani angekataa? Ndugu zetu mmeaminshwa kwamba Nyerere alikuwa mbaguzi na aliukuza ukatoriki! Kama kweli angetaka alikuwa na nafasi hiyo na saa hizi mgekuwa mnalia na kusaga meno!
Halafu eti wasomali ni wengi Kenya kwa vile hizi nchi zimepakana,hivi Somalia haipakani na nchi nyingine zaidi ya Kenya huyu demu haeleweki.
 
Humu kuna great thinkers kweli na wamehusha nondo hasa ingawa kuna harufu ya udini pia!
 
Halafu eti wasomali ni wengi Kenya kwa vile hizi nchi zimepakana,hivi Somalia haipakani na nchi nyingine zaidi ya Kenya huyu demu haeleweki.
Siyo kupakana tu ila kuna mikoa ni wasomali watupu na wala hawajahamia kama vile Mandera, Wajir, Isiolo, Garissa na Ijara. hivyo hapo wabunge, madiwani na hata mchimba mtaro ni msomali.

 
Hapana
Amezaliwa Butiama, lakini wakati akija Dar alikuwa akitokea Edinburg University Uingereza (UK) baada ya kuhitimu shahada ya uzamili (Masters degree).
Kwa hiyo Nyerere tunayemjadili hapa ni Mzanaki au Mzungu?
 
Ni kweli Kiswahili ni lugha ya PWANI ikiwa ni mchanganyiko wa kibantu na kiarabu. Ni kweli Nyerere alikuja mjini Dar akiwakuta watu wa PWANI wakizungumza kiswahili lakini mchango wa Nyerere kukipaisha Kiswahili haupingiki hata kidogo.
Nyerere baada ya kuchukua nchi akatangaza Kiswahili iwe lugha rasmi ya nchi, hata sisi wa vijijini tukalazimishwa kutumia lugha rasmi ya Kiswahili, tulishaandika vitabu kwa lugha zetu lakini Nyerere akatupiga stop, ndio maana anabidi apewe sifa kwa kuwafanya mamilioni ya watu waishio mbali na PWANI ya Tanzania kuzungumza Kiswahili. Asilingelifanya hili labda Kiswahili kisingekuwa maarufu kama kilivyo leo hii

Rekebisha, Nyerere alikuja Dar es salaam (Mzizima) akitokea Edinburg University sio Butiama.
Nirekebishe nini mkuu, Nyerere kwa mara ya kwanza kukanyaga Dar ilikuwa mwaka 1952 akitokea Tabora.
 
Nirekebishe nini mkuu, Nyerere kwa mara ya kwanza kukanyaga Dar ilikuwa mwaka 1952 akitokea Tabora.

Huoni umemerekebisha?? mwanzo uliandika alikuja akitokea Butiama, sasa hivi umesema alikuja akitokea Tabora. .
 
Kwani mtoa mada kasema kimeletwa na Nyerere? Au amesema tutamkumbuka kwa mengi ikiwamo kiswahili? Kubali au ukatae Nyerere anao mchango wake hasa kisera kwenye kukifanya kiswahili kutumika kama lugha rasmi Tanzania

Kwani kabla ya Nyerere kilikuwa hakitumiki rasmi? ni nani alikudanganya, nilikuwepo kabla ya Uhuru na ndiyo lugha ikitumika Tanganyika.
 
We bibie ukianzisha bendi ya taarabu utaimudu vizuri sana. Kipaji unacho. Hongera sana kwa kujaaliwa hicho kipaji. Ni ushauri tu......



Punguza kashfa! Hapo Mkuu FaizaFoxy amekupa hoja nzito...nakhis huna uwezo wa kumjibu kwayo,au!?

Hii iwe fundisho/somo kwa wale wafia Unyerere wangine woote wasio na hoja zenye mantik!

Wakiongozwa na yule garasa lao kuu!...yaani yule kilaza ajiitae ati Mwanakijiji! Daah!

Huo ushauri wako baki nao tu, au kampe yule msukule wa Kihehe aka Yericko Nyerere!

Ahsanta.
 
Back
Top Bottom