Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

Nyerere tutakukumbuka na kuenzi kila kitu isipokuwa CCM!

Teh teh teh!!! msome tena hapa chini kiduchu.

Hakuna aliyekataa kuwa alikuwa siyo msomi hawa wazee walikuwa waungwana sana pamoja nyie kuwatukana kuwakejeli lakini angalia alivyokuwa wanaishi na hawa wazee, wala hawa wazee walikuwa hawaitaji sifa walikuwa wanaishi nae kama kijana wao tu, haya maneno Nyerere kayesama mwaka 1985 wakati wengi hawa wazee walikuwa wameishatangulia mbele ya haki, sasa hizi falsafa unazotuambia alikuwa anamwabia nani.

Tatizo lako Ritz unataka ushinde kila kitu hata kwa kuchakachua ni jadi yako sikulaamu ni msimamo wenu haya mkuu najiandaa kuingia kwenye malumbano ya hoja.
 
Hili la Kikwete kuifanya lugha ya Afrika silifahamu!!,,najua kiswahili kimeanza kukubalika Afrika lakini siioni role ya Kikwete katika kufanikisha hilo.

Jisomee: Viongozi APRM wametambua lulu ya Kiswahili, tukidumishe - Tunu Yetu - mwananchi.co.tz

Kwa ufupi
Baada ya Rais Kikwete kuwasilisha ripoti yake, alipongezwa na viongozi mbalimbali wa Afrika kuhusu utawala bora na umoja wa kitaifa uliopo, huku ikitajwa kwamba lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa kichocheo kikubwa cha amani na utulivu, ambapo viongozi wengine wa Afrika walisisitiza kuiga kutoka kwa Tanzania.
 
Tatizo lako Ritz unataka ushinde kila kitu hata kwa kuchakachua ni jadi yako sikulaamu ni msimamo wenu haya mkuu najiandaa kuingia kwenye malumbano ya hoja.

nuruyamnyonge

Wala mie sijabishana naeleza hali halisi wala sijachakachua kitu hayo maneno yapo kwenye hotuba ya kuwaanga aliyoitoa Nyerere, mwaka 1985 Dar es Salaam.
 
Last edited by a moderator:
Ulitaka atuachie nini mkuu? Hivi wewe ukiwa na watoto ukawalea kwa maadili mema lakini kwa wendawazimu wao tu wewe ulipoondoka wa kaanza kuwa wehu, unataka jamii ikihukumu wewe baba Yao kwa makosa yawatio wako?

kabla hajafa aliuona upuuzi wa ccm lakini hakufanya lolote , japo alikuwa na uwezo hata wa kuifutilia mbali .
 
Mmezoea kumpa sifa ambazo hana mnamuona mtukufu wakati hana lolote alikua mdini tu. Ndo muasisi wa udini nchi hii
 
ni kweli kabisa ulichokisema. ila leo hii natamani angetangaza kiingereza ndo lugha ya taifa.

Ni kweli Kiswahili ni lugha ya PWANI ikiwa ni mchanganyiko wa kibantu na kiarabu. Ni kweli Nyerere alikuja mjini Dar akiwakuta watu wa PWANI wakizungumza kiswahili lakini mchango wa Nyerere kukipaisha Kiswahili haupingiki hata kidogo.
Nyerere baada ya kuchukua nchi akatangaza Kiswahili iwe lugha rasmi ya nchi, hata sisi wa vijijini tukalazimishwa kutumia lugha rasmi ya Kiswahili, tulishaandika vitabu kwa lugha zetu lakini Nyerere akatupiga stop, ndio maana anabidi apewe sifa kwa kuwafanya mamilioni ya watu waishio mbali na PWANI ya Tanzania kuzungumza Kiswahili. Asilingelifanya hili labda Kiswahili kisingekuwa maarufu kama kilivyo leo hii

Rekebisha, Nyerere alikuja Dar es salaam (Mzizima) akitokea Edinburg University sio Butiama.
 
Hili la Kikwete kuifanya lugha ya Afrika silifahamu!!,,najua kiswahili kimeanza kukubalika Afrika lakini siioni role ya Kikwete katika kufanikisha hilo.
mkuu role ya kikwete huwezi kuiona maana hamtaki kusikia jema lolote la kikwete. maana mpo tayari hata lami zilizojengwa na kikwete mzibomoe kisa tu ya chuki zenu kwa jamaa.
 
kabla hajafa aliuona upuuzi wa ccm lakini hakufanya lolote , japo alikuwa na uwezo hata wa kuifutilia mbali .
mkuu kweli unahasira na ccm. ninahasira na ccm ila siwezi kuacha kukubali kuwa kikwete katusongeza mbali sana kutoka alipotukuta katika nyanja mbali2 za maendeleo.
 
Kumlinganisha Kikwete na Nyerere ni sawa na kumlinganisha Prof Maji Marefu na Obama!
 
mkuu role ya kikwete huwezi kuiona maana hamtaki kusikia jema lolote la kikwete. maana mpo tayari hata lami zilizojengwa na kikwete mzibomoe kisa tu ya chuki zenu kwa jamaa.

Kwani ana 'nyota' ya kuchukiwa? Huwezi kumchukia mtu bila sababu..kama role yake ipo tuwekee hapa utuelimishe badala ya kutushambulia.
 
Jisomee: Viongozi APRM wametambua lulu ya Kiswahili, tukidumishe - Tunu Yetu - mwananchi.co.tz

Kwa ufupi
Baada ya Rais Kikwete kuwasilisha ripoti yake, alipongezwa na viongozi mbalimbali wa Afrika kuhusu utawala bora na umoja wa kitaifa uliopo, huku ikitajwa kwamba lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa kichocheo kikubwa cha amani na utulivu, ambapo viongozi wengine wa Afrika walisisitiza kuiga kutoka kwa Tanzania.

Sasa role ya kikwete ipo wapi hapo? Ni kweli kiswahili nin kichocheo kikubwa cha utulivu na amani hapa kwetu, na kwa hilo tutamkumbuka nyerere alieona mbali. Wewe unataka kutuonesha kwamba kiswahili kutumika tz imekuja automatic, kwa taarifa yako tu ni kwamba kiswahili kilikuwa kinatumika mwambao wote wa afrika mashariki ikiwa ni mpaka Mombasa, Lamu, mogadishu etc,,sasa mbona hizo nchi zingine hakikuenea mpaka bara??
 
Ninaposema katokea Butiama namaanisha alipozaliwa, chukuwa darsa kiduchu kutoka kwa Ritz

Nyerere, kwa mara ya kwanza kufika Dar ni mwaka 1952 alikuja kwenye mkutano wa TAA kama mjumbe kutokea Tabora.

Na mtu aliyempokea ni Aziz Dossa.

Mwaka 1954 ndiyo alikuja rasmi Dar na kupokelewa na Abdulwahid Sykes pamoja na wazee wa Dar.

Mara nyingi Butiama hutumika kwa madhumuni maalumu, wakati fulani Mohamed Said katika jitihada zake za kupingana na kivuli cha Nyerere alipata kusema ..haiwezekani nyerere atoke Butiama aje kuunganisha watu wa mjini, ilihali yeye ni wa kijijini/mkoani (mshamba), sasa kasahau kuwa alikuwa akitokea Ulaya kwenye majiji makubwa na yenye wasomi sana zaidi ya Mzizima yetu

Kumbe Sykes na Dosa bdio waliomtafutia kazi St Franciss (Pugu sekondari)????

Nyerere alikuja akawakuta watu wa PWANI wamepoteza lugha zao za asili baada ya kuchangamana na lugha za wakoloni wa kiarabu na kutengeneza Kiswahili. Kwa busara zake zakutaka sote tuwe uniform basi akasema na sisi tuache lugha zetu ili tuungane kuisema na kuiandika lugha ya Kiswahili japo influence ya Uarabu ilikuwa sio kubwa sana kwa sisi wa vijijini/mkoani
 
Sasa role ya kikwete ipo wapi hapo? Ni kweli kiswahili nin kichocheo kikubwa cha utulivu na amani hapa kwetu, na kwa hilo tutamkumbuka nyerere alieona mbali. Wewe unataka kutuonesha kwamba kiswahili kutumika tz imekuja automatic, kwa taarifa yako tu ni kwamba kiswahili kilikuwa kinatumika mwambao wote wa afrika mashariki ikiwa ni mpaka Mombasa, Lamu, mogadishu etc,,sasa mbona hizo nchi zingine hakikuenea mpaka bara??

Kusoma hujui? hiyo ripoti aliiwasilisha nani na unajuwa ilikuwa ya nini?
 
Jisomee: Viongozi APRM wametambua lulu ya Kiswahili, tukidumishe - Tunu Yetu - mwananchi.co.tz

Kwa ufupi
Baada ya Rais Kikwete kuwasilisha ripoti yake, alipongezwa na viongozi mbalimbali wa Afrika kuhusu utawala bora na umoja wa kitaifa uliopo, huku ikitajwa kwamba lugha ya Kiswahili ni miongoni mwa kichocheo kikubwa cha amani na utulivu, ambapo viongozi wengine wa Afrika walisisitiza kuiga kutoka kwa Tanzania.

Huwa nakubali uwezo wako lakini udini ndo tatizo!
 
mkuu kweli unahasira na ccm. ninahasira na ccm ila siwezi kuacha kukubali kuwa kikwete katusongeza mbali sana kutoka alipotukuta katika nyanja mbali2 za maendeleo.

aliyoyafanya JK hata wewe ungeweza kuyafanya , kwani WEWE HUWEZI KUTEUA MAWAZIRI HATA KAMA MARA 5 KWA MWAKA AU KUKAGUA GWARIDE NA KUPOKEA HATI ZA MABALOZI WAPYA ?
 
  • Thanks
Reactions: mpk
aliyoyafanya JK hata wewe ungeweza kuyafanya , kwani WEWE HUWEZI KUTEUA MAWAZIRI HATA KAMA MARA 5 KWA MWAKA AU KUKAGUA GWARIDE NA KUPOKEA HATI ZA MABALOZI WAPYA ?

Na kuhani misiba huku unacheka!
 
Upende usipende mwl.Nyerere alitoa mchango mkubwa sana kutuunganisha kwa kutumia lugha ya kiswahili.

Embu tazama hapo nilipo-BOLD kwenye hiyo bayana yako!

Sasa mbona watumia lugha za mabavu na ujuba kwenye majadiliano tu kiduchu, ya staha na kuelimishana!?

Au ndo umerithi toka kwa yule Babako wa Taifa!? Daah! Teeh! Teeh! Teeh!

Kwa kifupi...kitaaluma na kiungwana,ulitakiwa ujibu zile hoja zangu!

Nyerere,mchango mmojawapo alotoa ni kudunisha ile lugha ya Kiswahili na ati kuitafisha/kuwanyang'anya wale wenye lugha yao...na ati kuwaambia yakua hii lugha naifanza ni ya Taifa zima!? Ebo!

Khalaf,akazidi kuweka mikakati yake ya kinyama/dhuluma ili kurejesha nyuma kwa makusudi yale maendeleo japo kiduchu,aliyoyakuta kwenye yale maeneo yakaliwayo/waishiyo Waswahili/Wana Mwambao kwa wingi!

Mara nyingi yule Nyerere, alitumia wakti na khutba zake kadhaa ati kuwabeza Waswahili!...yeye ndo alokua kinara mkubwa/instigator wa kutumia lile neno "Mswahili" as a derogatory term...khasa zile "enzi za Mwalimu"! Daah!

Salaam zao!

Ahsanta.
 
mkuu role ya kikwete huwezi kuiona maana hamtaki kusikia jema lolote la kikwete. maana mpo tayari hata lami zilizojengwa na kikwete mzibomoe kisa tu ya chuki zenu kwa jamaa.

Duuh! Teeh! Teeh! Teeh!

Basi Watanzania mna safari ndefu mno! Daah!

Ahsanta sana Mkuu!
 
Back
Top Bottom