Nyie! Cadillac Escalade inakuaje Uber?

Nyie! Cadillac Escalade inakuaje Uber?

Uber ni Uber tu haijalishi ni luxury au vyovyote taxi ni taxi tu
Of course, hata Landmark ya pale Ubungo Riverside (kama bado ina-exist) na Serena ya pale Ohio, zote ni hotel tu, na kwahiyo hotel ni hotel tu! Sasa endelea kujiona mpo sawa kati yako unayepeleka demu Landmark Hotel na mwenzako anayepeleka demu Serena Hotel!!!
 
Haya majamaaa yananishangaza kweli eti mtu anaona dollar 70k ni kidogo
Hv kweli mtu ana gari mbili za 70k unaona napo hela ndogo aisee
Mzee, tena huwezi kusema $70K kwa sababu hiyo ni bei ya kununulia!! Cadillac ipo kwenye kundi la luxury cars, na kodi yake ile ni zaidi ya Sh. 100M! Kwa maana nyingine, ile gari hadi inaingia barabarani itakuwa inakaribia 400M. Sasa ni mwehu tu ndie anaweza kukejeli gari ya 400M. Ile gari ukiileta Bongo halafu ukaiingiza showroom, wa kuinunua wanahesabika.
 
Sasa akiachana na Almas, manake haongelewi tena .Yy wanyonge wake walikuwa Magu, Makonda, Diamond na familia yake.

Magu Mungu kamchukua, Makonda anapiga mitikasi mengine,so sasa yy ana Diamond.

Yeye kazi yake kuweka bando na kujifungia ndani basi ana deal na Diamond pamoja na famila yake.Kaenda US miaka kibao hata kazi ya kuuza mgahawa hana, halafu kuna watu wanamuona Genius utawasikia "akili kubwa......dada wa taifa.......Da Mange kasema ",kumbe yupo yupo US anazurula na unaweza ukakuta hata uwezo wa kununua bando hana anaseleleka na WI-FI za bure US.
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Off course kuishi kule unapata exposure huwezi kudanganyika kiboya Kama kuishi kwenye dunia ya tatu
Ndo ukweli wenyewe, ambao wabongo hawataki kuusikia, hasa domokaya team [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Zipo mpaka Ferrari, Lamborghini and the likes ambazo ziko kwenye category ya luxury Uber, hivyo Escallade kuwa Uber haimaanishi ni sawa na Toyota Corolla Uber.
All in all let's say Escallade ni gari cheap kuanzia kuinunua, ushuru hadi maintenance je ni wangapi wanazo Bongo? Msilete reference za Marekani kwani ni nchi mbili zenye tofauti kubwa mno ya standards za maisha.
Kwa USA huwa wanapenda vyao ila duniani luxury cars karibia zote katika top 10 zinatoka Germany na ndio maana nje ya USA huwezi kuta watu maarufu wanaendesha hizi gari za US. kikwetu hapa ni zile gari unanunua bei kubwa na ukitaka kuuza unapata bei kubwa na hiyo ni Toyota Landcruiser tu zingine thamani inaunguka ikitoka showroom tu na naongelea zero KM gari mpya kabisa sio used.
 
Utakuta anaipondea Cadillac Escalade ilihali hapa alipo hana hata kiwanja mjini.
Mi nasema hivi! Mange hata kama gari yenyewe anayo basi ni ya Kijapan ya $4500 kwahiyo anaona aibu hata kui-post! Mange anavyopenda mapicha picha, na angekuwa na gari iliyoenda shule, angeturushia hadi mapicha akikatiza mitaa ya LA!!
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Kwa usupastaa wa Diamond hivyo inabidi iwe ni vitu vya kawaida..
Sikatai lakini mkuu si diamond ana escalade mbili lile la lexanimotors si 250k USD au nalo ni la kawaida kwa uchumi wake
Halafu tukiangalia sisi watanzania tunahanagaika mno
Diamond hajaongea kitu mzee
Wala hajajisifu
Kuna siku kwan ameshayaongelea magari yake???
Lakini watanzania kelele nyingi hata kitu ambacho hajaongelea muhusika tutamlazimishia.....

I respect the guy's hustle six cars mkuu
2 v8's
1 prado
1 bmw x6
2 escalades
Ahhh mzeee ukijumlisha hapo ndugu tunaondoka na half a billion kwenye magari tu
Hata angenunua crown sina shda nae
Pesa anayo
 
Mi nasema hivi! Mange hata kama gari yenyewe anayo basi ni ya Kijapan ya $4500 kwahiyo anaona aibu hata kui-post! Mange anavyopenda mapicha picha, na angekuwa na gari iliyoenda shule, angeturushia hadi mapicha akikatiza mitaa ya LA!!
Huwa anapost kavaa viskini taiti huku akidolishia spoku zake, hata kununua wigi la kubadilisha anashindwa.
Mchunguze vita vyake huwa ni dhidi ya watu wanaopambana na kufanikiwa.
 
Ila Diamond kwa hela aliyonunulia hayo magari ni bora angevuta Cullinan au Urus
 
New boss
Ile ya pili ila ile ya kwanza
Ni kama 250k new maana ni lexani luxury wameipamba ndani
Hizi gari zinatengenezwa na makampuni mawili tofauti moja inatengeneza copy na nyingine og! Og bei yake imesimama na ndiyo ile ya kwanza ambayo kuijua mpaka uone ndani ina lound usd 350,000 mpaka 500,000
Screenshot_20210626-171643.jpg
 
Hizi gari zinatengenezwa na makampuni mawili tofauti moja inatengeneza copy na nyingine og! Og bei yake imesimama na ndiyo ile ya kwanza ambayo kuijua mpaka uone ndani ina lound usd 350,000 mpaka 500,000View attachment 1830854
unachanganya madesa mkuu
gari hizo zina tengenezwa na kampuni ya General Motors
ila hao jamaa wakuitwa Lexan wao wana zinunua kisha wana zi Customize au wana zipimp mule ndan na kuubadilisha kabisa muonekano wake ndo maana hata bei zake una kuta zime simama hizo ambazo zinatoka kiwandan na kuuzwa ndo zina price range ya 75k USd
 
  • Thanks
Reactions: Qwy
Mtu anaishi kwa Child Support halafu anaaminika ni akili kubwa. Magari yenyewe Diamond hajayazungumzia chochote.

Hiyo migari wanayotaka anunue ili aonekane tajiri haifai kwa bongo itaishia kukaa yard tu. Kwa barabara zipi unaendesha LAMBORGHINI? Itakuwa ni uharibifu wa hela aliyoitafuta kwa shida.

Unanunua kitu unakipenda na kinachokupa uhuru wa kukitumia sio gari kutoka nalo linakupa mawazo!

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom