Nyie fresh graduates, please msiwaibie mabosi wenu. Waoneeni huruma. Kuanzisha biashara mpaka ikue ni kazi nzito sana

Nyie fresh graduates, please msiwaibie mabosi wenu. Waoneeni huruma. Kuanzisha biashara mpaka ikue ni kazi nzito sana

Hapa Kuna mmoja ananizingua nimemkuta anachumba ngombe nimempaisha mpaka Sasa ananiona Kama ananisaidia ...Kuna kosa nilifanya....Ila siku si nyingi ntammwaga mavi
 
Wadogo zangu ambao ni fresh graduates mnaokaribia kuanza kazi au mpo kazini ila ni wachanga hapo ofisini, kamwe usimuibie boss wako. Hiyo ni laana.

Kama unaona mshahara pamoja na bonuses zingine hazitoshi, please acha kazi kisha uende ukatafute kwingine kwenye maslahi mazuri zaidi ya hapo ofisini kwenu.

Wadogo zangu fresh graduates, kuanzisha biashara from scratch mpaka kuja kuwa kubwa ni mtihani mkubwa mnoo. Waoneeni huruma bosses wenu.

Wakati ninafanya kazi Tunduma mwaka 2014, nilikuwa ninalipwa mshahara take home roughly 700,000/= pamoja na bonuses 200,000/= lakini still kuna watu wa level yangu bado walikuwa wanacheza dili za kuiba spaner pamoja na spare tyre ilhali ni fresh graduates, hana mke wala mtoto. Yupo yeye kama yeye tuu.

Jenga picha katika kundi kubwa la vijana wapatao 20 waliofanya interview, ameaminiwa yeye tu mtu mmoja. Sasa inakuwaje unamuibia mtu aliyekuamini na kukukabithi mali yake uisimamie aisee??

Leo yangu mimi ni hayo tu. Mimi ni graduate wa tangia mwaka 2012. Nimeyaona mengi sana huko ofisini wadogo zangu wa 2000.

Ni mimi,

Muuza Maembe.
Wewe unadhani aliyeanzisha au huyo mwajiri wako hakuwa mwizi? Yawezekana aliiba kwa kalamu au kuua ili apate hiyo biashara. Kwa Tanzania hii? Ahh bhagosha.
 
Unakutana na mibuyu na wewe ni maotea wanakwambia percent Yako kiasi Fulani... Kuna pahala ni majaribu mno mno....
 
Back
Top Bottom