Nyie wachora ramani waongo sana

Alivyopiga hesabu akaniambia tofauti 1100 tu mzigo Tayari unaisha!,nikasema maisha si ndio hayo najenga chap chap!nilichokutana nacho hizo tofali 1000 zimeisha tu kwenye msingi

Labda alikadiria tofali zenye ukubwa kama ule wa tofali za pyramids za Giza
 
Inategemea alimaanisha tofali za ukubwa gani na ww umetumia za ukubwa gani[emoji28]

Ukute alikuambia tofali za blocks ww ukatumia za kuchoma ( bricks) hapo lazima mgombane tu![emoji28]

Karibu nikusaidie kuifanyia makadirio upya kama hutojali
Mkuu nipatie ramani ta hii nyumba , idadi ya tofari pamoja na mabati
 
We ulidanganywa, mimi jamaa kanichorea ramani na kanipa BOQ ya kila kitu kaniambia tofali 940 za msingi na kila kitu. Fundi kaja kasema tofali 1200 na mimi nikanunua. Mwishi wa siku kaishia kutumia tofali 918 nyingne zote zimebaki. Nikaamini aliyechora ramani na kuandaa BOQ anajua.
Sasa hivi nafuata BOQ kununua materials zikipungua ndipo naongeza.
Wewe aliyekuchorea kanjanja.
Halafu pia inategema alimaanisha tofali za ukubwa gani mm kaniwekea tofali na idadi kwa ukubwa 3 tifauti.
 
Sasa ukikuta Huyo Civil/Archtecture Eng., wakiwa wanabishana na Tajiri na fundi mzoefu ambaye hajasoma mambo ya ujenzi, utacheka.

Fundi: Tajiri unajua mimi ndiye nafanya kazi hapa, wewe si unaona hao ni wasoma ramani tu, hata mwiko hawajui kushika.
 

Hata mimi niliona pesa niliyokuwa nayo ni nyingi sana kumbe hata msingi haitoshi
 
Sasa ukikuta Huyo Civil/Archtecture Eng., wakiwa wanabishana na Tajiri na fundi mzoefu ambaye hajasoma mambo ya ujenzi, utacheka.

Fundi: Tajiri unajua mimi ndiye nafanya kazi hapa, wewe si unaona hao ni wasoma ramani tu, hata mwiko hawajui kushika.

Kama vile ulikuwepo [emoji28]nilikuwa nabishana na mafundi kuwa msingi ni tofali 300 pekee matokeo yake zinaenda 1000 nashuhudia kwa macho yangu ,nilikuwa bega kwa bega hata kula siendi
 
Kikawaida chumba kinakula tofali 400 kwa chumba cha futi 10-12 . Mafundi wengi ni bababishaji, tulimwambia fundi hili eneo linatakiwa fance kiasi gani akatuyajia kumbe hata kupima hajapima, kuja kuweka imeishia kati ashukuru mm ckuwapo toka mwanzo

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
Nimetumia tofali za blocks mkuu sio za kuchoma [emoji28]jamaa ameniponza sana mahesabu yangu ilikuwa milioni 3 tu ngoma ishapendeza matokeo yake hata kifusi cha msingi sijamwaga

Yaan wewe nae Yan vyumba viwil tofar 1000 Acha utan broo
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ na ulimlipa bei gani im curious
 
Uongo huo mimi nyumba yangu kubwa na msingi wa Tofar sita imekula 1250

Chumba master

Vyumba viwil

Jiko store dinning sitting

Acha uongo et vyumba viwil msingi Tofar 1000 big no [emoji51]
 
Ni ngumu sana ukitumia vipimo kukosea labda mhusika awe hajawahi kufika ili afanye survey eneo lako.
 
Ha haa weww si huwa unasema watu wanaongeza masifuri? Haya fanya utubu. [emoji2][emoji2][emoji2][emoji2]
 
Kwani ukiambiwa mchoraji lazima awe mkadiriaji?
Kazi ya Quantity survayor (QS) ni nini?
 
Makadirio ya Nyumba yanatokana na Eneo husika na namna Msingi unavyotaka kujengwa.

Mfano , Mtu anae chimba Msingi wa futi 3 ni tofauti na Msingi wa futi 2 ama futi 1 na Nusu

Pia inategemea na Msingi wa hiyo Nyumba , mfano baada ya kuchimba kule China unatanguliza nini...so watu wengi hiki kitu hawakijui....all in all, Jitahidini kutafuta wataalam wawasaidie...
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ