Jamaa alianza kuyumba muda mrefu kidogo. Lakini sio yeye tu, almost wasanii wote. Ukiona mtu anafanya vibaya na bado ana trend jua kabisa hata competitors wake hawana afadhali. I think kuna kitu hakipo sawa kwenye industry ya mziki wa hapa nyumbani.
Sijui ni ukosefu wa ubunifu/ elimu ya mziki ndio ugonjwa wa wasanii wetu au ulimbukeni wa mashabiki wetu wa mziki!
Saivi inaweza ikapita hata miaka mitatu hujaskia kwanja ya maana hata moja. Hapa ndipo tulipofika na kwa bahati mbaya wajomba wa tuzo kubwa Africa na Duniani hawana huruma na kazi mbovu. Wako radhi wampe tuzo mtu mmoja hata mara mia as long as anafanya kazi nzuri.
Kwa kweli saivi hatupo vizuri halafu ni kama Africa nzima imeshatushtukia kuwa mziki wetu ni wa ujanja ujanja. Mambo ya ku copy, edit na paste.
Content za nyimbo nyingi ni very poor to the extent kunatumika nguvu nyingi na gharama kubwa sana kwenye shooting ili tu kulazimisha mashabiki waangalie nyimbo youtube. This is sad. Prime purpose ya mziki ni to be listened to, na sio to be watched. Feli kwenye kumfanya mtu apende kusikiliza ngoma yako and you are done for good.
Kwa kweli we need reformation kwenye mziki kama ilivyo kwenye mpira, not good enough!
Btw, Nigerians are very good at this craft. We should sit down and take notes.
Mbona wakina six9ine, lil nax, Card B, wanaimba matusi, video zao zimejaa picha chafu na tuzo wanachukuwa na hizohizo nyimbo zao na mkwanja wanaingiza zaidi ya hao unaodhani wapo sahihi. Kwanini mnalazimisha basata wamfungie Diamond!
Kazi ya sanaa ni kuelimisha na kuburudisha, yeye kachagua kuburudisha tena kwa kutumia tafsida. Maana ya kitu ipo kichwani mwako, wewe ndio unatafsiri matusi. Neno "Rungu la kipepe, unavyoidaka, kuinyonya, ukiinama" sio matusi.
Hata wakisema wamfungie hawawezi tena anaweza kuwashtaki na akashinda kesi.
Vitabu vingi vya riwaya, tamthiliya vimejaa maneno ya ukakasi kama hayohayo ya Diamond na vinatumika mashuleni, kwenye majarida magazeti, sijawahi kusikia BAKITA wakilalamika.
Tamthilia kwenye Luninga tena bilashaka unaangalia kwenye luninga yako, zimejaa picha zinazo amasisha ngono lakini TCRA wapo, kwa nini Diamond?
Leo karibia nchi zote za Africa wanatengeneza video za Ngono, na zipo kwenye tube mbalimbali na wanajulikana, na mamlaka ziko kimya. Diamond anachoimba ni afadhali kuliko wengine na uimbaji huohuo ameendelea kuwa nominated kwenye tuzo mbalimbali Duniani na nyingine kushinda.
Dunia ya sasa inapenda nyimbo hizo na ndizo zenye hela ndefu. Hapa bongo karibia 70% wanaimba viashiria kama Diamond, msikilize Gnako, Maua sama, Mabantu nk
Ni vizuri kukijenga kizazi chako katika maadili unayo ona ni sahihi. Dunia ya sasa ilisha chafuka na ndiko hela rahisi zilipo.