Mbona wakina six9ine, lil nax, Card B, wanaimba matusi, video zao zimejaa picha chafu na tuzo wanachukuwa na hizohizo nyimbo zao na mkwanja wanaingiza zaidi ya hao unaodhani wapo sahihi. Kwanini mnalazimisha basata wamfungie Diamond!
Kazi ya sanaa ni kuelimisha na kuburudisha, yeye kachagua kuburudisha tena kwa kutumia tafsida. Maana ya kitu ipo kichwani mwako, wewe ndio unatafsiri matusi. Neno "Rungu la kipepe, unavyoidaka, kuinyonya, ukiinama" sio matusi.
Hata wakisema wamfungie hawawezi tena anaweza kuwashtaki na akashinda kesi.
Vitabu vingi vya riwaya, tamthiliya vimejaa maneno ya ukakasi kama hayohayo ya Diamond na vinatumika mashuleni, kwenye majarida magazeti, sijawahi kusikia BAKITA wakilalamika.
Tamthilia kwenye Luninga tena bilashaka unaangalia kwenye luninga yako, zimejaa picha zinazo amasisha ngono lakini TCRA wapo, kwa nini Diamond?
Leo karibia nchi zote za Africa wanatengeneza video za Ngono, na zipo kwenye tube mbalimbali na wanajulikana, na mamlaka ziko kimya. Diamond anachoimba ni afadhali kuliko wengine na uimbaji huohuo ameendelea kuwa nominated kwenye tuzo mbalimbali Duniani na nyingine kushinda.
Dunia ya sasa inapenda nyimbo hizo na ndizo zenye hela ndefu. Hapa bongo karibia 70% wanaimba viashiria kama Diamond, msikilize Gnako, Maua sama, Mabantu nk
Ni vizuri kukijenga kizazi chako katika maadili unayo ona ni sahihi. Dunia ya sasa ilisha chafuka na ndiko hela rahisi zilipo.