Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Nyimbo za utotoni za zamani ambazo watoto wa leo hawazijui

Amina panda mlima
Siwezi kupanda
Kwann huwezi kupanda?
Naumwa na tumbo
Tumbo hilo kakupa nani?
Kijana hassan
Kwann usikatae ?
Naona utamu
Siku ya kwanza Utamu yes yes utamu
Siku ya pili utamu yes yes utamu
Siku ya tatu utamu yes yes utamu
Siku ya nne ng'aa ng'aa

Hivi akiyetunga nyimbo hii alifilia nn? [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hahahaha huo wimbo ilikua wakati wa kucheza kamba sasa kibinti kimeshabana sketi yake kipindi hicho nyonga imetanuka basi akiruka kijungu kinanesa nesa sasa wakifika kwenye siku ya kwanza utamu hahaha kiuno kinavyobinuliwa ni sheeedah..... lol
 
Hahahahaaa daaah ungekuwa Nyani Ngabu ningekwambia fcuk you. .... unajua kwanini......
We nahisi tulikaa mtaa mmoja au ulikuja kuhamia mtaa ambao sie tulihama hahahahhahahaaa

Hiyo ya yangeyange nipe kucha nyeupe nimefanya sana. Tena nikiwa na kaka zangu, tukienda kwa babu yetu Upanga mtaa wa Malik sijui ule karibu na kwa baba taibali jioni wanapita yangeyange weengiii. Basi tunaanza yangeyange nipe kucha nyeupee hahahahahaha na kweli.....

Huwezi amini hadi sass hivi kucha zangu kama sijapaka hina au rangi ya kucha hizo alama nyeupe zinaonekana daaah

Hahahahahahahahahahaaaa

Fcuk you Kasie Matata
 
Kinyuli nyulika mwanangwa wa Jumbe, kavaa nguo mbili, ya tatu kajifunika.Aliye juu aondoke.

Hapo mmefinyana nyumba ya viganja
images.jpg
 
Ha ha ha kwa baba Taibali break ya saa nne tubavuka barabara kununua Sun Vita! Nimekaa moja ya mtaa off Malik sikutajii.

A aahahahahahahahaa weeweeee kwa mwalimu Ndosi sio na Mama Batalingaya hahahahahahah Mama Nanaayakara ulimkuta?

Jamaniii San vita ya orange na blackcurrant hahahahahaha. I remember baba Taibali.......

Wee ufiche tuu huo mtaa kwenye hiyo Old School Re-union utautaja tuu hehehehehehehehe
 
Mama Nanayakara alikuwa mwalimu wangu wa darasa 7C....na kigugumizi chake. Kasie usiongelee tena mambo ya shule.
 
Mama Nanayakara alikuwa mwalimu wangu wa darasa 7C....na kigugumizi chake. Kasie usiongelee tena mambo ya shule.

Aaahahahahahhahahahahahaaa loooh looh looh duuuh inabidi nikufinye aiseeh hahahahahahahahahaaa

Haya basi wacha yaishie hapa aahahahahahahaaa

Hii ya mwisho.....

Wale mapacha 2 wanene weusi walikuwa wa kiume. Wanafanana halafu nywele zao kama zilikuwa zina dawa hivi unawakumbuka? Nakumbuka mmoja alienda Tambaza......

Ki RRONDO ulikuwa mdogooo wakati ule aahahahahahahaaa.
Basi siongelei tena hiyo ndo ya mwisho aahahahahahahahahhahahahahaaaaaa looh leo.
 
Sawa panapo majaliwa tutaonana ule mtaa wa pili naona upo na wazee wenzio ngoja niwapishe

Yaaani leo basi tuu hadi mzuka wa kunanihii umepanda jinsi nilivyo furahi kukumbuka zamani.

Kiukweli nashukuru Mungu utoto wangu haukuwa mbaya nilipata malezi yote mema na ulinzi wa wazazi na ndugu. Ndomaana hapa nina furaha sana hadi kiwi imepanda hehehehehee.

Kuna watu utoto wao ulikuwa mateso chuki na tabu kedekede na imewatokea hivyo sio kwa kupenda ni mazingira waliyoyakuta. ....

Inshallah panapo majaaliwa kama Islamabad basi tutaonana.
 
Waalaah wakiacha hizo party wanazoandaaga clouds kuzunguka nchi yote halafu wana mziki ndo wanakuwa wanaimba live, wangeandaa tamasha hili la nyimbo za zamani na watuachie tuimbe na kucheza wenyewe. Mbona mngeburudika hahahahaha maana nyimbo zote ningesema na marede yote ningecheza hadi mpira wa tobo bao ningecheza. Hahahahahaa bado zile sarakasi za kuning'inia kwenye bomba halafu unabiringita unatokelezea upande wa pili bila kuachia mikono. Hii niliifanya sana kutokana na kukua na kaka zangu.
Utaweza sasa na hii miili ya utuuzimani...maana utotoni unabimbirika kama mwanasarakasi hahahhaha
 
Yaaani leo basi tuu hadi mzuka wa kunanihii umepanda jinsi nilivyo furahi kukumbuka zamani.

Kiukweli nashukuru Mungu utoto wangu haukuwa mbaya nilipata malezi yote mema na ulinzi wa wazazi na ndugu. Ndomaana hapa nina furaha sana hadi kiwi imepanda hehehehehee.

Kuna watu utoto wao ulikuwa mateso chuki na tabu kedekede na imewatokea hivyo sio kwa kupenda ni mazingira waliyoyakuta. ....

Inshallah panapo majaaliwa kama Islamabad basi tutaonana.
Mhhhh kwani kuna muda mzuka wa kunaniii unashuka? Muda wote unanyevua tu asalaleeee utanipa shida hapa inshallah tutakutana Islamabad Mungu akijalia
 
Utaweza sasa na hii miili ya utuuzimani...maana utotoni unabimbirika kama mwanasarakasi hahahhaha

Aiseeh Kasindeee ni mbishii. .... wanaonijua watakuhakikishia. Mie mwili wala haunizuii kufanya chochote, navaa swimming costume kwa raha zangu atayeshangaa na kusonya shauri yake.

Likiandaliwa hilo tamasha, ukimuona mbibi kila wimbo na mchezo yupo ujue ndo Kasie heheheheheheee
Halafu niko mtata na kwenye michezo ni mzulumishi balaa hehehehehee.

Kasie Matata.
 
Mhhhh kwani kuna muda mzuka wa kunaniii unashuka? Muda wote unanyevua tu asalaleeee utanipa shida hapa inshallah tutakutana Islamabad Mungu akijalia

Hahahahahahahahaa kumbe unajua eeeh, mzuka kwa Kasie hujawahi kushuka aiseeh. Sijui sababu ya ubishi.... na ugagula huu lakini bado kiwi iko palepale na show ikianza nasimama mwanzo mwisho wala sitegei hahahahahhahaa

Shida yake nikitoka hapo lazima nitembee na gongo langu laasivyo mtatembea migulu baja.

Halafu nimekumbuka huu wimbo tulikuwa tynawaimba kundi la watoto..... utasikia

Migulu baja migulu bajaa haiwezi kucheza na sisi.
Hapo mshawafunga magoli kibao hehehehe.
Hivi RRONDO unakumbuka kumegeana sun vita. ... Ai weewee naomba nimegee kidogoo aahahahahaaa mabungo jeeeh.
Je mchezo wa kiskio pooh.... na ule wa BP ukikutwa hujaandika sehemu yoyote mwilini unawanunulia wenzio bigG na pipi. Na mwingine Gosha poo ukiwahiwa Gosha poo unabinya vidole vilie kama siku hiyo j3 basi vilie mara 3. Usiombe Mungu uwahiwe ijumaa halafu vidole vinagoma kulia maana hapo uviminye vilie mara 7 hahahahaa nilivua hadi viatu kubonyeza vidole vya miguuni hahahahaa. Ukishindwa kama ndo ijumaa unakula makonzi saba hahahahahaha michezo ya kitoto banaa daah.

See yaah @Intanbul too heheheheheheh (Yamak)
 
Back
Top Bottom