Nyoka aina ya Black Mamba mawindoni

Nyoka aina ya Black Mamba mawindoni

Kijiji kikiwa na Koboko huwa kijiji kinahama. Halafu uje utwambie mlikua mnawaua kwa mawe?
Kwanza wakishaona hatari huwa wanaanzisha msaka kwa kugawa himaya kwa kila mmoja kujimilikisha eneo la kutosha kwa ajili ya kulilinda
Ni vijiji vya waoga tu ndivyo vinavyoweza kuhama maskani yao ya asili na kuacha makaburi ya mababu zao nyuma eti kwa kukimbia nyoka!
 
Hicho Kijiji watakuwa wanaishi wanaume wa buza
Aisee hao wakiingiia kwenye vijiji kama ilivyotajwa hapa ni lazima kwanza watu wahama ili tatizo lishughulikiwe.
Uzuri wa Koboko ni mmoja, hapandi kelee na interactions. Wanapoona shughuli za kibinaadam zinaanza kuingia mahali basi watasababisha madhara na kuamua kuhama mazima.
Tabora ilowahi kutokea, Koboko walivamia viji, siyo kijiji, wakawa wanaua watu na mifugo. Shughuli za kilmo na kuchunga zikasimama, jambo likafika hadi bungeni ikaombwa Jeshi lipelekwe kupambana nao. Wakaambiwa hiyo siyo namna ya kupamba na Koboko, watahatarisha maisha ya asari wetu bila sababu, swala likashughulikiwa kwa sheria za asili likaisha. Haimaanishi kuwa haiwezekani kumuua, wakijichanganya huwa wanauawa kama kawaida, bu the risks na hasa wakishagundua wanawindwa

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji | JamiiForums Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji

Ni vijiji vya waoga tu ndivyo vinavyoweza kuhama maskani yao ya asili na kuacha makaburi ya mababu zao nyuma eti kwa kukimbia nyoka!
 
Ndugu Si ndio wale tulikulia polini, huyo Ni mwenyewe ndugu najua fikra yako inakwambia cobra, cobra huwa hatembei umbali mrefu kanyanyua kichwa, huwa akinyanyua kichwa Ni pale anataka kutema mate au kuangalia adui alipo, Lakin huyo unamuona alivyo tembea parefu amenyanyua kichwa chake,
Na hiyo Ni tabia ya koboko ili asipoteze focus Kwa adui
 
Aise! Yaani just kusikia hicho kiumbe tayari naogopa.
 
Kuna sehemu kuna mto nilikuwa nataka nioge,nikaanza kupiga uluzi huku najiandaa kuvua nguo,ghafla naona mwamba anatokea kwenye kichaka kichwa kiko juu anakuja kwangu fasta,ilinibidi nikimbie kuokoa maisha yangu.Ambacho sikujua,ni ule mluzi ndio ulimuita au aliniona kuwa natishia tu usalama wake akaamua kunitokea...
Labda alijua wewe baniani maana hao ndio uwaita kwa miruzi na kucheza nao ..
 
Aisee hao wakiingiia kwenye vijiji kama ilivyotajwa hapa ni lazima kwanza watu wahama ili tatizo lishughulikiwe.
Uzuri wa Koboko ni mmoja, hapandi kelee na interactions. Wanapoona shughuli za kibinaadam zinaanza kuingia mahali basi watasababisha madhara na kuamua kuhama mazima.
Tabora ilowahi kutokea, Koboko walivamia viji, siyo kijiji, wakawa wanaua watu na mifugo. Shughuli za kilmo na kuchunga zikasimama, jambo likafika hadi bungeni ikaombwa Jeshi lipelekwe kupambana nao. Wakaambiwa hiyo siyo namna ya kupamba na Koboko, watahatarisha maisha ya asari wetu bila sababu, swala likashughulikiwa kwa sheria za asili likaisha. Haimaanishi kuwa haiwezekani kumuua, wakijichanganya huwa wanauawa kama kawaida, bu the risks na hasa wakishagundua wanawindwa

Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji | JamiiForums Tabora: Nyoka Koboko amekunywa uji wa Moto, amkimbiza Mganga wa Kienyeji
Hivi Badala ya kumpelekea jungu la uji kwanini asipuliziwe sumu kwa kutumia kipulizi chenye nguvu kinachoweza kurusha dawa umbali mrefu ( mt 20-30)?
Na pia nyoka wote akiwemo koboko hawana uwezo wa kuhimili dawa za kuulia wadudu, petroli, mafuta ya taa na hata maji yaliyo changanywa na chumvi.
Vyote hivyo vikigusa mwili wa nyoka anakimbia mbali.
Nijuavyo nyoka wote humuogopa binadamu ingawa mara chache koboko huleta vurugu karibu na makazi ya watu.
Na pia hutokea mara chache kama mnakutana kwa bahati mbaya mkashtukizana kila mtu akipita zake anakung'ata ili kujihami.

Lakini mara nyingi Koboko aliyetulia kwenye territory yake hana madhara mpaka umchokoze maana yeye anaanza kukuona kabla hujamuona.

Hata hivyo wafrika (hasa watanzania) tunampa sifa kemkem koboko ambazo nyingi kati ya hizo hana.
Koboko hana uwezo wa kunywa uji wa moto kama ilivyo kwa binadamu.

Yule jamaa wa South Africa "Snake city" akisikiliza simulizi za watanzania hataingia majumbani kuwadaka koboko na Cobra.
Jamaa anawakimbiza na kisha kuwadaka kama mijusi.
Labda Tabora kuna aina tofauti ya koboko.
 
Nyoka yeyeto unaweza mdhibiti kwa kuvaa mavazi maalumu mfano kama yale ya kufundishia mbwa meno yeyeto hayapenyi plus helmet ngumu yenye miwani.
Aisee mavazi hayo yanapatikana wapi mkuu? Nayatafuta sana.
 
Back
Top Bottom