Semere92
JF-Expert Member
- Oct 6, 2019
- 577
- 777
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
ameshindwa kuponyaKwahy yule nyoka kweny nembo ya WHO anaponya corona sio
Mh! ngumu sanaNyoka ni alama ya Tiba na Uponyaji ndo maana taasisi nyingi za Tiba hutumia nemboya Nyoka. Hata Shirika la Afya Duniani WHO linaumia nembo ya nyoka, waganga wa jadi wanafuga nyoka wa kutosha, hata kwenye nembo ya hospitali ya Muhimbili kuna chata ya nyoka, Noti ya shilingi mia tano pia ilikua na picha ya nyoka ikimaanisha uchumi imara unahitaji watu wenye afya.
Nyoka ni kiumbe pekee mwenye uwezo wa kijivua gamba, tafsiri yake ni kwamba kujivua gamba ni kuleta uhai mpya (Mgonjwa Kupona). Lile gamba la nyoka ukikutana nalo barabarani linatoa nuksi, lishike tu uondoe nuksi za ile rambirambi uliyokula. Hata vidonge vimeundwa kwa mfano wa mayai ya nyoka kuvipa uponyaji. Kumbuka madaktari wanatibu, uponyaji anatoa Mungu.
Mussa alitengeneza nyoka wa shaba akamweka juu ya mti na kila aliyegongwa na nyoka alipona kwa kumwangalia nyoka yule. Uamuzi wa Mungu kuweka uponyaji kwenye nyoka wa shaba hadi mwana wa israeli kupona ndio umefanya taasisi nyingi za tiba duniani kutumia alama iyo ya nyoka.
Mara nyingi ipo getini ili mgonjwa anapoingia getini tu amwangalie nyoka apokee uponyaji. Wazee wa zamani wanakuambia nyoka anajua dawa zoe za mitishamba, nyoka akipata jeraha hujitibu au hutibiwa na wenzake hadi apone walitumia mitishamba, ndo mana wazee wa zamani wakikutana na hali iyo waliwafuatilia nyoka na kuangalia wanachuma dawa kwenye miti gani? na kutumia miti hiyo kama Tiba.
Marekani walianza kutumia alama ya nyoka baada ya kuja Afrika na kujifunza siri hii kutoka kwa wazee wetu, wakati jeshi lao lilioamua kutumia nembo ya nyoka kama alama ya kikosi cha Tiba cha jeshi ambalo awali lilitumia alama ya msalaba. Hii inarahisisha kazi ya madaktari kwa sababu wanatibu mtu mwenye uponyaji teyari. Ndugu zangu hii dunia ni kubwa mno unachotakiwa ni kujifunza kwa bidii sana ili usiishie kutukana tu ati nyoka ni ushirikina.
Nyoka ni kielelezo cha udadisi na umakini, utamaduni wa kuhoji badala ya kukubali kila kitu kirahisi. Kitendo cha nyoka kumwambia Eva ale tunda kina tafsiri mbili. Wapo wanaoona kitendo hicho kama uongo na wengine kama udadisi. Tafsiri ya makala hii ni tujifunze utamaduni wa kuhoji, tusikubali kila kitu kama mazuzu na wakati tuna akili za kutosha.
Robert Gren anasema, mwandishi wa kitabu cha THE 48 LAWS OF POWER anasema,"Hatuna budi kumshukuru nyoka, nyoka alikua mwalimu mkuu wa kwanza duniani, mtetezi wa kwanza wa udadisi na utafiti, adui wa kwanza wa ujinga, mnong'onezaji wa kwanza kwenye sikio la mwanadamu wa kwanza ili ajikomboe." Hii inaitwa Mental Liberation.
Usipotuliza akili ukaenda kiroho sana utasema Gren alimkufuru Mungu na wakati bibilia inasema, "Nyoka alikua mwelevu kuliko wanyama wote wa mwituni aliowafanya Bwana." Soma Mwanzo 3:1.
Kumbuka hata yesu mwenyewe amewahi kukiri kuwa nyoka ni mwelevu sana na akawatuma wanafunzi wake wawe na busara kama nyoka. Hili ni funzo kubwa sana kwamba kila kitu kina ubaya na uzuri na ukijua hilo huwezi kumuua mke wako kwa sababu amekudanganya mana hata wewe ni muongo tena kumzidi mkeo.
Kwanza uongo unasaidia sana maana kuna ndoa bila kudanganya zingesha kusambaratika siku nyingi. Bila kudanganya kuna watu walishafukuzwa kazi siku nyingi. Kuna watu bila kudanganya wasingepata wachumba na wengine wasingeoa bila uongo. Kuna watu uongo umewaokoa na kifo, tatizo la uongo ukigundulika ndo utakoma.
Nyoka ni ishara ya kujipa muda wa kufikiri kabla ya kutenda (Kuwa Makini) kwa asili nyoka ni mtulivu hafanyi jambo bila sababu. Ni hatari kwa viumbe wengine ana sumu kali, hafanyi jambo bila kufanya mchanganuo wa hasara na faida. Nyoka anapenda kukaa sehemu yenye utulivu, anaweza kuingia ndani ya nyumba na kusepa bila mtu yeyote kujua. Wengi tumelala na nyoka sana tu, wakati wa kiangazi wanakunywa maji ndani kabisa, sema kwa sababu ya mahesabu huwezi kuwaona. Nyoka wanacheza sana na watoto wako na hawafanyi kitu chochote kwa sababu wanajua watoto hawana roho mbaya.
Kupitia nyoka tunajifunza kutofanya mambo bila kuangalia madhara na faida kama mjinga anayepima kina cha maji kwa miguu miwili. Tusiwe kama yule mama mkwe aliyetumia hisia kujaji, kisa cha mama mkwe, "Bwana mmoja alikwenda kutembea ukweni kwake ilipofika usiku aliamka kwenda kujisaidia lakini kwa bahati mbaya taa zote zilikua zimezimwa, wakati anapapasa ili kuwasha taa aliparamia vyombo vya chakula jikoni. Kipindi anajaribu kuviweka vizuri mara taa ikawasha na mama mkwe akamuona yule bwana ameshika vyombo na kumwambia. Baba kama hukushiba ungesema.
Mama mkwe alitumia hisia kujaji hakujipa muda wa kufikiri. Shida ya hisia inakupa majibu ya haraka ambayo yanaweza kukuletea shida. Unadhani yule bwana aliendelea kukaa ukweni? Ndo yaleyale unakwenda kutembea sehemu unasikia sisi humu ndani hatujwahi kuibiwa kitu kabisa. Kichwa kisipofanya kazi vizuri ya kufikiri utakuwa mtu wa kuchafua hali ya hewa kila siku. Nyoka anatukumbusha kujipa muda wa kufikiri zaidi.
Kwaiyo unapokutana na nyoka mara kwa mara basi rejea hizi tafsiri hapa lakini unapokutana na nyoka ndotoni hizi hapa tafsiri kutoka kwa mtaalamu wa mambo ya asili.
1. Ukiota umegongwa na nyoka ina maana kwamba unatakiwa kuwa makini kwenye mambo yako vinginevyo utaumia. Umezoea kupiga hela acha, una tabia ya kula ada acha, una tabia ya kula michango ya harusi acha, unahonga hadi hela ya rambirambi acha mara moja, una tabia ya kuchepuka acha usikamatwe na mchepukaji mwezako akakunyonga.
Siku hizi wanaume wanaua sana na hiyo ndo maana ya ndoto ya nyoka. Wazungu wanasema if you have a dream of a snake chasing you, this might mean that you need to look at the relationship in your life and see if you have sweapt any issues underneath malizia kwa kugoogle huo msemo ........
2. Ukiota unamuona nyoka maana yake ni kwamba utadanganywa na mkeo au mumeo. jaribu kumkumbusha uaminifu katika ndoa, najua atawaka kwa sababu umemtachi lakini usikonde kwa sababu kinga ni bora kuliko Tiba ya mapenzi.
3. Ukiota unapigana na nyoka ni ishara ya kuwashinda adui zako, lakini ukiota unakimbizwa na nyoka jua adui zako wanakumaliza. Jipange, kazi kwako kupambana na hali yako. Kazi ya nyoka ni kukupa taarifa tu.
4. Ukiota unafuga nyoka au unamiliki nyoka au nyoka anakumeza hiyo ni ishara ya kupata madaraka makubwa ya uongozi. Kama ulipanga kutia nia we tia tu usiache.
5. Ukiota umemuona nyoka anauliwa barabarani hiyo ni ishara ya kutokea vita au magomvi. unaweza kuzichapa kazini, nyumbani au popote pale hivyo jitahidi kuwa makini.
6. Ukiota shamba lako limejaa nyoka ni ishara ya kwamba utapata mazao mengi msimu huo tunza shamba lako vizuri na unapomuota nyoka amekufa ni ishara umeepushwa na uadui na shari yake. pengine ulikuwa unapiwa hadi kutolewa meno.
7. Ukiota joka kubwa linajizongazonga mwilini mwako ni dalili ya jini aliyeingia mwilini anatafuta sehemu ya kujificha ndani yako. Piga sana maombi.
8. Ukiota una nyoka shingoni mwako ukamkatakata maana yake unakwenda kutoa talaka kwa mkeo.
[emoji106]Na DaVinci XV
SEHEMU YA I
Masal kheyr wakuu,
MWANZO 3:1
Basi nyoka alikuwa mwerevu kuliko wanyama wote wa mwitu aliowafanya Bwana Mungu.
Binafsi tangu ningali mdogo nilikuwa na tatizo la Ophidio-Phobia (Fear of Snake) kikawaida mwanadamu yoyote anaweza kuwa na Uwoga juu ya nyoka ila ule uoga uliopitiliza juu ya kiumbe hicho ndio huitwa Ophidio-Phobia. Sikumbuki hili tatizo lilianzia wapi na kwenye tukio gani, japo Ubongo wangu ulikuwa unanisukuma kuamini vitu viwili ambavyo nadhani vilikuwa vichochezi vya hii kadhia niliyo nayo.
Mosi, Ni Movies ambazo zilihusisha kiumbe huyu kushambulia wanaadamu movie kama Anaconda na nyinginezo pengine ndizo zilichagiza mimi kwa kiasi kikubwa kuwa na mtazamo wa kuogofya juu ya kiumbe huyu, Lakini Pili ,Bibi yangu kipenzi ambaye pia alikuwa mlezi wangu alipoteza uhai kwa kuumwa na Kiumbe huyu ningali bado mdogo hivyo sikuwa na uhakika wa moja kwa moja juu ya phobia yangu imetokana na nini kati ya hivyo viwili.
Kadri nilivyozidi kukua ndivyo phobia yangu iliposhuka kwasababu nlitamani kumjua kiundani kiumbe huyu na kwanini nlikuwa na uoga nae usiomithilika kiu ya Kumsoma ikanijaa kadri nilivyozidi kukata miaka kujongea Utu uzima.
Rasmi nikaingia kwenye dimbwi la kumsoma kiumbe huyu kidini, kimazingira na hata kisayansi halafu mwishowe akabadilika kutoka kwenye kumuogopa hadi kuwa miongoni mwa Viumbe pendwa ninaovutiwa nao, kama ilivyo kwa mtu mwingine yoyote kuvutiwa na Mnyama Simba au Hata Chui, nami ilitokea Sana kumhusudu Nyoka kwa namna alivyo na mwenendo wake kama ningekuwa Msanii mwenye A.K.A za wanyama Basi ningejiita Nyoka [emoji28][emoji28][emoji28].
Nlitembelea karibuu zoo nyingi zinazotunza wanyama hawa na kujifunza aina tofauti tofauti za viumbe hawa ukiachana na kupitia majarida na facts mbalimbali kuwahusu.
Si mnakumbuka namna Mungu alivyomtumia nyoka katika visa tofauti tofauti ikiwemo pale Misri kwa Musa na Wachawi wa Firauni.
Lakini pia si mnakumbuka Nyoka alivyotumika na Ibilisi kumhadaa Mama yetu Hawa kule bustanini Eden, na Kwenye baadhi ya Mandiko nyoka akabaki kitendawili atasimama Upande upi wema au Ubaya.
Kwani ninyi hamkumbuki vita iliyowekwa kati ya kiumbe huyu na mwanadamu kwenye maandiko popote wakutanapo?
Nyoka akanenwa kwa Ubaya sehemu nyingi sana. Na kutokana na maandiko hayo ya mwanzo ambayo Mwanaadamu akikutana na Nyoka basi kinachofata ni vita haijalishi kiumbe huyo alikuwa anataka kudhuru au yupo katika Eneo lake.
Na si mnakumbuka Pale zamani wazee walipotuhadithia mengi sana kuhusu kiumbe huyu wakatutisha kwamba ukiota ndoto za Nyoka basi majini wanakuwa wanashughulika nawe kwa namna moja au nyingine,
Mungu alimuumba nyoka kwa namna ya tofauti sana na kumpa uwezo wa kipekee mno, si unafahamu ya kwamba nyoka kila muda huzaliwa upya pale anapojivua gamba na hii imefanya wengi kuamini kwamba nyoka huwa hawazeeki,na hii ndio kielelezo cha jamii nyingine kumtumia nyoka kama alama ya kuzaliwa upya.
Tukamuona Nyoka katika nembo nyingi sana ikiwemo kwenye Tiba na Afya mahospitalini, waganga wa jadi , Mahekalu na Madhabau, Vikundi vya siri , pete na mikufu ya Watu wakubwa, makanisa, mashirika makubwa makubwa duniani na Logo tofauti tofauti.
Na wengi wakahitimisha kwamba mashirika hayo yapo chini ya Shetani pengine kwasababu tu Alama ya nyoka katika nembo Bila kufahamu haswa chanzo chake ni nini.
Kuna karibu species zaidi ya 3000 za nyoka na karibu species 600 tu ndio nyoka wenye Sumu duniani. Nyoka huishi sehemu tofauti ikiwemo kwenye mchanga, Majangwa, Mapango na Miamba mikubwa, kwenye Maji, vichaka na nyasi ndefu na kuna wanaoishi kwenye miti mirefu.
Nyoka wengi hula Mijusi, Ndege, vyura na Wadudu wengine wadogowadogo.
MTAZAMO WA NYOKA KULINGANA NA JAMII ZA KALE
Huko misri ya kale ambapo dunia ya sasa kuna wanaomini, ilikuwa ni kitovu cha maendeleo na Utamaduni wa kistaarabu na Elimu iliyo pana sana katika ulimwengu basi kwao Alama hii ya Nyoka ilitumika kama uponyaji na Uhai lakini pia Nyoka alikuwa kama kiumbe anaewakilisha Miungu wengi kama ilivyo utamaduni ule wa kale wa Misri kuwakilishwa na miungu wengi.
Moja ya uwakilishi wa Alama hii ya nyoka katika jamii hiyo iliyostaarabika ya Wamisri wa kale, kumwakilisha Mungu wao aitwaye Autum mungu huyu wa wamisri, ambaye aliikuwa alama ya Uhai maana wao waliamini yeye ndiye mwenye uwezo wa kutoa Uhai. Wamisri wale wa kale waliwakilisha uhai wa milele na alama ya Nyoka.
Mungu mwingine ni Amuun naye aliwakilishwa na alama ya nyoka huyu mungu wa wamisri wa kale aliwakilishwa na Alama nyoka alikuwa Mume wa Mungu wa kike wa zama hizo ambaye aliitwa Mut , ambaye kwa pamoja walizaa mtoto wao aitwaye khonsu,ambaye alifanya watengeneze Utatu Mtakatifu.
Na utatu huu mtakatifu wa miungu hawa uliwakilishwa na Alama ya Nyoka.
Na ukisoma hadithi zao za Misri ya kale utaona kazi za miungu hawa wanaowakilishwa na nyoka ni zile zile zinazoendana ambazo ni Uponyaji na kutoa Uhai wa Milele.
Hivyo kutupa picha kidogo juu, Ya Alama hii ambayo kwa Asilimia kubwa ni imani uponyaji na Uhai. Kuna miungu wengine kama Geb, Thermuthis, Wadjet na Buto wao pia ni miungu katika jamii za wamisri wa kale ambao ni wema kwao.
Hao ni miongoni mwa Miungu wa misri ya kale ambao kwao na Mujibu wao walikuwa ni miungu wazuri. Ukirudi upande wa pili kuna miungu wabaya ambao miongoni mwao ni Apophis , huyu alikuwa mpinzani mkuu ambaye nae aliwakilishwa na nyoka yeye alikuwa nyoka wa giza kama wao wamisri walivyomwita.
Tunaweza kuthibitisha kwamba, kutokana na uthibitisho wa namna tofauti tofauti kama huo kutokana na hadithi nyingi, nyoka alisimama kwa wema wa hali ya juu na vile vile uovu kati ya Wamisri wa kale, na kwamba taswira ya nyoka ilihusishwa bila ubishi na maisha ya baada ya kifo, ufufuo,uponyaji na umilele.
Pia utamaduni wa kale wa Mesopotamia wababiloni na Wasumeria unaonyesha uwili unaohusishwa na Alama ya nyoka sawa na ule unaopatikana katika jamii za WaMisri.
Miungu wao wengi Akiwemo Tamuzi, pia muda mwingine aliwakilishwa na sanamu ya nyoka. Yeye na mama yake waliwakilishwa na Nyoka kwa baadhi ya vielelezi.
Miungu hawa waliwapa uponyaji wale wote waliowatii na kuwaabudu
Katika mitazamo ya ulimwengu ya Wasumeri na Wababiloni, nyoka alikuwa ni mfano wa sifa ya kuzaliwa upya na uponyaji wa Walimwengu.
Kwa hiyo, Wasumeri na Wababiloni waligeuza mambo haya ya asili kuwa miungu maalum ya nyoka kama walivyofanya kwa miungu wengine.
Na si ajabu kukuta milango mingi ya mahekalu ya wakati huo wa tawala za Babyloni kuwa na Alama za nyoka, hasa kipindi cha mfalme nebchadneza katika milki ya Babiloni (605 - 562 K.K)
Kuna hadithi ilikuwepo miongoni mwa wababiloni kwamba, kuna mmea ulikuwepo ambao ulikuwa ukiutumia basi, huwezi kufa lakini alitokea Mungu muovu Ahriman na kutengeneza Nyoka ambaye alifanya uharibifu juu ya Mmea huo.
Lakini pia kuna hadithi ya nyoka wakubwa ambao watafanya mashambulizi dhidi ya Miungu ya kweli ya Babiloni kwa Mujibu wao. Hivyo maandishi ya Wababiloni pia yanaonesha pande mbili za Nyoka kama ilivyo katika Hadithi za Wa Misri.
Vivyo hivyo hata katika jamii za wagiriki Miungu yao Eshimun na Asclepius ambao pia walikuwa miungu ya Dawa, Tiba na uponyaji, kama itatokea mtu amekutana na Maradhi au sumu mwilini mwake basi, hawa walihusika katika Uponyaji na Ujuzi wa Dawa za kutatua matatizo mengi mengi kwa Watu wao.
Ingawa mifano inaweza kuongezeka hapa, lakini yatosha kusema kwamba kuna uthibitisho wa kutosha ili kuonyesha wazi kwamba ibada na Alama ya nyoka kwa namna moja au nyingine ilipatikana kotekote katika eneo la kale la Mediterania, hasa miongoni mwa jamii kubwa kubwa za wakati huo ikiwemo maeneo ya karibu zaidi na Israeli.
Hadithi zinazojulikana za Mashariki ya kale hudhihirisha mapambano ya mwanzo kati ya nguvu za mema na mabaya, zote mbili ambazo mara nyingi huwakilishwa na nyoka.
Akiwa mleta wokovu na mtoaji wa uzima wa milele nyoka alifanyika upande wa kimungu. Kama msafirishaji wa kifo nyoka akawa mwili wa pepo wachafu.
Kinyume na hali ya uwili huu tunageukia sasa kwenye maandiko matakatifu, ambapo tunapata habari muhimu ili kutusaidia kuelewa kwa ukamilifu zaidi na kufahamu upana wa maelezo na ulinganifu.
INAENDELEA SEHEMU YA II
NYOKA ALAMA YA UKOMBOZI AU UPOTOFU KWA MUJIBU WA MAANDIKO MATAKATIFU.
Da VINCI XV
Sawa sawa karibuu mkuuNimeweka kambi hapa nijifunze.
Japo kwangu Ophidio-Phobia imegoma kuniachia
Shukraaani[emoji106]
Naam,Nyoka.....
Pamoja na kutajwa kuwa MUOVU/ANATUMIKA NA WAOVU....lakini tunamuona akitumiwa na NABII MUSA(mtu mwema) mbele ya farao kuyameza yale majoka ya "wana mazingaombwe"......
*****************
#Never give wisdom to unworthy because it's unfair to the knowledgeable
Kareebu sanaSawa Sawa Elimu Haina Mwisho